Si lazima nielewe kila kitu ambacho Mungu anafanya ili niendelee kumwamini.
Mawazo yake ni makubwa kuliko yangu, na njia yake inaweza kuwa bora kuliko niliyoipanga.🙏🏼
Wakati unaanza kuona mambo yako yananyooka, Top of your game, ndipo shetani hapo hapo anaanza ku engineer downfall yako.
Hii uwa hatua ya kuwa makini sana, haswa kujikweza.
"Maneno machungu huacha makovu katika moyo wa mtu. Ukilazimika kuyatumia dhidi ya mtu, basi yatumie kikamilifu mara moja kisha uachane nayo. Kuyarudia rudia ni kutonesha makovu na maumivu yake huishia kujenga chuki na ikiwezekana kisasi. Usiyarudie maneno machungu, buni mapya!"
Dunia imejaa walimu na wahubiri wengi ambao wanachofundisha au wanachohubiri hawajawahi kukiishi.
"Hand knowledge" will always beat head knowledge back to back time and time again. 🙏
"Maisha ni bundle unaishi kwa kulipunguza si kibubu kwamba unaishi kwa kuongeza. Ukishazaliwa,siku zako za kuishi haziongezeki tena bali zinapungua kutoka kwenye jumla ya siku zako za kuishi duniani.Kesho si nyongeza bali ni makato.Usihesabu zimebaki ngapi bali zimepungua ngapi."
Ukisikia story za Wazee ambao wamewahi kuacha familia walizoanzisha na kwenda kuanza maisha mapya, probably built a better family kuliko ya Mwanzo, hii ni ishara unaweza kuanza tena, unaweza kujisahihisha, unaweza ku win tena after a couple of loses.
USIOGOPE.
Bwana Mungu wangu, nakuja mbele zako nikikiri kwamba wakati mwingine nimepoteza mwelekeo, nimelegeza nidhamu na nimeacha baadhi ya mambo yaliyonijenga.
Lakini leo sitaki kubaki hapo.
Nataka kurudi kwenye njia sahihi.
Nipe nguvu mpya ya kuanza tena.
Amina 🙏🏼
Mifumo ambayo inatufanya tuishi bila kujitafakari kwa kina ni mingi na ina mizizi haswa.
1. Mfumo wa kupenda attention
2.Mfumo wa Kujilinganisha
3. Mfumo wa Materialism na Consumerism
4. Mfumo wa Distraction.
Kila kitu kinakunasa humo sio bahati mbaya.
Kuna siku hutajisikia kuomba.
Kuna siku hutakuwa na nguvu ya kufanya kazi.
Kuna siku utataka kurudi kwenye tabia zako za zamani.
Ndipo unapohitaji nidhamu kuliko hisia.
Usisubiri motivation kila siku.
Jenga utaratibu ambao utaendelea hata siku ambazo hujisikii.
Brotherhood imetuokoa watu wengi sana.
Sometimes unahitaji maneno mawili matatu kutoka kwa mtu ambaye hakuhumu, anaelewa maisha kwa mtoto wa kiume kuna muda yanavuruga sana.
Eeh Mwenyezi Mungu, Baba yangu, ninakuja mbele zako kama nilivyo.
Nisaidie kuanza upya bila kukata tamaa kwa sababu ya yaliyopita. Nifanye upya katika mawazo yangu, nidhamu yangu na mwenendo wangu.
Nirudishe katika maombi, katika Neno lako na katika bidii ya kazi.
BRO TO BRO
Siku moja utamwelewa Baba yako zaidi ukiwa Baba mwenyewe
Utagundua kwamba kulea mtoto si rahisi
Utagundua kwamba wakati mwingine mwanaume anatabasamu mbele ya familia huku ndani akiwa anapitia maumivu makali.
Msamehe Kisha Jifunze kuwa baba bora kuliko alivyokuwa
Wakati mwingine unaweza kudhani watu ni bitter uncles au bitter aunts.
Lakini ukweli ni kwamba, tabia zako zinawakumbusha makosa yao, matokeo yasiyobadilika na majuto wanayoishi nayo.
Ndiyo maana matendo yako pekee unaweza kuwapa moto bila hata wewe kujua.
Hapa tulipo hatujafika kwa bahati mbaya
"Safari yetu ilikuwa na maumivu makali sana, tumepoteza muda kufika hapa, safari ambayo imekuwa na masimango mengi “Kukatishwa tamaa na kudharauliwa. Tulipo hapa ni MUNGU tu, mkishindwa kutuombea basi msitudhuru.
•GOOD MORNING:• ❤️
Wakikupenda watasema UNAJIAMINI.
Wakikuchukia, watakuita mwenye MAJIVUNO.
Kuna tusi linamaanisha we mkali, Kuna sifa zinamaanisha kejeli.
Muda mwingine si kile unachoambiwa, bali ni sababu nyuma ya kauli zao.
Take notes..👍
Mafanikio ya Mtu hayategemei Maoni,Chuki,Wivu au kibali cha Watu wengine.Kubali kwamba kila Mtu ana Safari yake
Mafanikio ya Mtu mwingine hayahitaji Ruhusa yako,na Baraka za Mungu hazitolewi kwa kura za Watu
Watu watafanikiwa tu iwe unawapenda au huwapendi
Mungu si Mjomba wako.
Kila Asubuhi mpya ni ushahidi kwamba Mungu bado hajamalizana na wewe. Shukuru kwa uhai, ombea nguvu, na tembea kwa imani.
Neema ya Mungu ikutangulie leo 🙏🏼