"Masuala ya kampeni za mapema. Na hapa ni kuwaasa wale wanaojipanga kwenda kugombea. Masuala ya kampeni za mapema tunayakemea. Tayari tumeshapa malalamiko nina ushahidi wa picha za watu ....,” Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo amesema wamejipanga vyema kuhakikisha sikukuu ya mwaka mpya 2025 inasherehekewa kwa amani na utulivu, kwa kuzingatia kuwa kutakuwa na mkesha wa siku tatu katika Jiji la Arusha.
@nyotaraystv
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza leo Disemba 27.2024 katika eneo la Usagara limeendea kudhibiti hali ya usalama barabarani kwa kufanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye magari yanayobeba abiria kwenda mikoani kwa lengo la kuzui ajali zinaotokana na uzembe wa madereva.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza leo Disemba 27.2024 katika eneo la Usagara limeendea kudhibiti hali ya usalama barabarani kwa kufanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye magari yanayobeba abiria kwenda mikoani kwa lengo la kuzui ajali zinaotokana na uzembe wa madereva.
Uongozi na Wana Familia Wote wa Nyotarays Company na @nyotaraystv_ unawatakia watanzania wote Heri ya Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya 2025. Karibuni sana Nyotarays tuwape huduma Bora zaidi mwaka 2025.
Tufuate Tu follow @nyotaraystv_ @nyotaraystv_
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Leo Desemba 21, amewasili Mwanza kwa ziara ya kikazi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa tenki la kuhifadhi maji la Kisesa, ikiwa ni Mpango wa muda wa kati wa kuboresha huduma ya maji na unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 3.54.
Baadhi ya Wasafirishaji mkoani Geita wamesema kuelekea katika Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya hali ya kifedha si nzuri kwani asilimia kubwa ya watu wanatembea kwa miguu.
@nyotaraystv_
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza DCP Wilbroad Mutafungwa amesema watafanya operesheni kali ya kukamata watu wanaofanya ramli chonganishi na kuchochea uhalifu ikiwa ni pamoja na mauaji yatokanayo na imani za kushirikina.
@nyotaraystv
Ni rasmi Sasa Tundu Lissu anawania nafasi ya uenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambayo kwa Sasa inashikiliwa na Mhe. Freeman Mbowe.
Lissu amechukua fomu hiyo Leo Jumanne Desemba 17,2024 Jijini Dar es salaam kwenye ofisi za Chama hicho.
@nyotaraystv_
Kupitia mradi wa TDS (Talents Development Scheme) ulioanzishwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) chini ya Mkurugenzi wake Asernal Wanger na kusimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mkoa wa Geita umeshiriki katika mradi huo wa kusaka vipaji vya vijana.
@nyotaraystv
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kwamba Profesa Mohamed Janabi atakuwa mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika katika uchaguzi utakaotangazwa na shirika hilo.
Amesema hayo leo Desemba 10, 2024 baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali.