Wiki iliyopita niliandika Habari ya shule ya advance huko UGANDA.
Elite High School Entebbe.
Ambayo ilizua Gumzo kwa wanafunzi wa shule hiyo kwenda kwenye Prom party na Magari ya kifahari pamoja na HELICOPTER.
Angalia vizuri shule hiyo na tukio hilo chini
Video kwa Comments👇🏾
Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika imekamilisha huku timu 8 zikifuzu hatua ya robo fainali
Kundi A
1. 🇿🇦 Sundowns — 13
2. 🇨🇩 TP Mazembe — 10
Kundi B
1. ,🇨🇮 Asec — 11
2. 🇹🇿 Simba — 9
Kundi C
1. 🇦🇴 Petro — 12
2. 🇹🇳 Esperance — 11
Kundi D
1. 🇪🇬 Al Ahly — 12
2. 🇹🇿 Yanga — 8
Tanzania ni Taifa pekee kuingiza timu mbili kwenye robo fainali Simba SC na Yanga SC.
Hakuna uwezekano wa wawili hao kukutana kwenye hatua ya robo fainali baada ya kila mmoja kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi lake.
Kinara wa Kundi moja atakutanishwa na mshindi wa pili wa Kundi lingine na hakuna uwezekano kwa timu zilizotoka Kundi moja kukutana kwenye robo fainali.
Kwa maana hiyo Yanga Sc hatakutana na Al Ahly na Simba SC haitakutana na Asec Mimosas.
Uwezekano wa droo ya robo fainali kwa Simba na Yanga upo hivi:
Simba Sc
• vs Mamelodi Sundowns
• vs Al Ahly
• vs Petro Atletico
Yanga Sc
• vs Mamelodi Sundowns
• vs Asec Mimosas
• vs Petro Atletico
✍️ Unafikiri Watani watapangwa dhidi ya nani robo fainali?
#KitengeUpdates
Hongereni sana Klabu ya Simba kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mafanikio yenu si tu furaha na fahari kwa mashabiki na wanachama wa Klabu ya Simba, bali pia kwa Taifa na Watanzania wote.