Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa, Prof. Method Samwel Semiono, amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Iringa kutunza miundombinu mipya ya Chuo. Ameyasema hayo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, alipofanya ziara yake Chuoni Mkwawa kuangalia maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mipya.
#MUCE #Iringa #HigherEducation #HEET #SamiaSuluhu #ElimuKwanza #ProudlyMUCE
Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa kiko tayari kukupokea wewe mwanafunzi unayetarajia kujiunga na Chuo kwenye Mwaka wa Masomo 2025/2026. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, amethibitisha hayo wakati wa ziara yake Chuoni hapo, leo 28 Agosti 2025.
#MUCE#Iringa#HigherEducation #HEET #SamiaSuluhu #ElimuKwanza #ProudlyMUCE
Menejimenti ya Chuo cha Mkwawa yapongezwa kwa usimamizi makini wa miradi ya ujenzi ya Serikali inayojengwa chuoni Mkwawa. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, amesema hayo kwenye ziara yake Chuoni hapo leo 28 Agosti 2025.
#MUCE#Iringa#HigherEducation#HEET#SamiaSuluhu #ElimuKwanza #ProudlyMUCE
β¨ Inaugural Issue of EJTL is Out! β¨
We are thrilled to announce the first issue of the Education: Journal of Teaching and Learning (EJTL) β Volume 1, Issue 1 (June 2025), published by the University of Dar es Salaam.
This issue features outstanding contributions from scholars shaping the future of teaching and learning in Tanzania and beyond. ππ
π₯ Visit our website π https://t.co/XsrGjSPgr0 to view and download your copy today!
π #EJTL #UDSM #MUCE #TeachingAndLearning #EducationJournal
Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kimehudhuria Kikao Kazi cha Watendaji Wakuu wa Taasisi na Wenyeviti wa Bodi kilichofanyika jijini Arusha, tarehe 23β26 Agosti 2025.
Kikao hicho kilifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Philip Isdory Mpango, na kufungwa na Naibu Waziri Mkuu, Mh. Doto Biteko.
π Katika mafunzo hayo, washiriki walijengewa uwezo kuhusu:
Β· Uboreshaji wa huduma π‘
Β· Usimamizi bora wa fedha π°
Β· Miongozo ya kitaifa na kimataifa π
Β· Kubadilishana uzoefu kati ya taasisi π€
MUCE iliwasilishwa na:
π Prof. Method S. Semiono β Rasi wa Chuo
π Prof. William A. L. Anangisye β Mwenyekiti wa Bodi
Kikao Kazi hicho kiliitishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa taasisi zote zilizo chini yake.
π #MUCEUpdates #Leadership #CapacityBuilding #Arusha2025
π€ Wanajumuiya wa MUCE Wako Tayari Kukukaribisha!
Wanajumuiya wa MUCE kutoka nje ya Chuo wanatuma salamu zao: βKaribu MUCE β hapa ndipo mahali pazuri pa kujenga ndoto zako!β
π Dirisha la Udahili bado liko wazi hadi 10 Agosti 2025!
π Usisite kuwasiliana nasi kwa msaada wa kujiunga:
+255 753 469 546 | +255 764 875 468
#MUCE #KaribuMUCE #ChuoChaWote #WanajumuiyaWaMUCE #Udahili2025 #PazuriPaKusomea #JiungeNaMUCE
Leo tarehe 5 Agosti 2025, MUCE imepata heshima ya kutembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Mhe. Benjamin Sitta, katika ziara yake ya kufahamiana na viongozi wa taasisi za Serikali zilizoko ndani ya Manispaa ya Iringa.
Katika mazungumzo yake na uongozi wa Chuo, Mhe. Sitta alipata fursa ya kupata taarifa kuhusu historia ya MUCE, maendeleo ya sasa, mipango ya baadaye pamoja na changamoto mbalimbali zinazolikabili Chuo.
Rasi wa Chuo, Prof. Method S. Semiono, alimpongeza Mhe. Sitta kwa uteuzi wake na kuaminiwa na Mheshimiwa Rais. Pia alimhakikishia ushirikiano wa karibu baina ya Chuo na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya katika kusukuma mbele maendeleo ya elimu na jamii kwa ujumla.
π€ MUCE inathamini ushirikiano huu kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
#MUCE #IringaMjini #ElimuBora #SerikaliNaElimu #UshirikianoWaMaendeleo #MkwawaCollege #WilayaYaIringa
π Jifunze Kiingereza Kutoka kwa Wataalamu Waliobobea!
MUCE inawakaribisha wanafunzi wanaotamani kuwa walimu bora wa lugha ya Kiingereza na wataalamu wa mawasiliano ya kimataifa. Tunao wataalamu mahiri wa Isimu na Mbinu za Kufundisha Lugha ya Kiingereza, akiwemo Dkt. Philpo John, ambao wamepata mafunzo kutoka taasisi za kimataifa na wana uzoefu mkubwa wa kufundisha kwa ufanisi darasani na nje ya darasa. Pia, Dkt. John ni moja ya matunda ya MUCE na tunajivunia yeye kuwa sehemu ya taasisi yetu.
Wataalam wetu katika eneo hili wanakuandaa:
β Kuelewa muundo na matumizi ya lugha ya mbalimbali, ikiwemo Kiingereza
β Kumudu mbinu bora za kufundisha Kiingereza kwa wanafunzi wa ngazi tofauti
β Kuwa mhamasishaji wa ujifunzaji wa lugha kwa njia shirikishi na jumuishi
Unapojifunza hapa MUCE, unapata mchanganyiko wa maarifa ya nadharia na vitendo, unaoendana na mahitaji ya soko la ajira na mabadiliko ya kisasa ya lugha na mawasiliano.
π Dirisha la Udahili bado liko wazi hadi 10 Agosti 2025!
π Piga simu sasa kwa msaada wa kujiunga:
+255 753 469 546 | +255 764 875 468
#MUCE #IsimuNaMbinuZaKufundisha #EnglishEducation #LughaZaKigeni #Udahili2025 #SomaMUCE #WalimuWaKesho #JiungeNaMUCE
βΏ Elimu Inayomjali Kila Mwanafunzi β Hii Ndiyo MUCE!
Katika kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma, MUCE inajivunia kuwa na wataalamu waliobobea katika Elimu Maalum β wakiwemo walimu na watafiti wenye ujuzi wa hali ya juu katika kushughulikia mahitaji ya wanafunzi wenye changamoto mbalimbali za ujifunzaji.
Mmoja wa wataalamu wetu katika Kitengo cha Elimu Maalum, Bw. Samwel Madale, yuko tayari kuhakikisha kuwa mazingira ya ujifunzaji yanakuwa jumuishi, salama, na yanayowezesha kila mwanafunzi kufikia malengo yake ya kitaaluma bila vikwazo.
π― MUCE ni Chuo kinachokuandaa kuwa:
β Mwalimu au mtaalamu anayejua namna ya kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum
β Mshauri katika elimu jumuishi
β Mtoa huduma anayejali usawa katika ujifunzaji
Tuna vifaa, miundombinu rafiki, na wataalamu sahihi β kwa hiyo kama unataka kusoma au kufundisha kwa kuleta tofauti kwa jamii, karibu MUCE!
π Dirisha la Udahili linaendelea hadi 10 Agosti 2025!
π Wasiliana nasi kwa msaada wa kujiunga:
+255 753 469 546 | +255 764 875 468
#MUCE #ElimuMaalum #WoteWanawezaKujifunza #Udahili2025 #ChuoChaUjumuishi #JiungeNaMUCE #ElimuBilaMipaka
π§ Elimu Bila Uelewa wa Saikolojia ni Nusu Tu ya Safari
Hapa MUCE, tunao Wataalam Wabobezi, wakiwemo Wahadhiri Wandamizi katika fani ya Saikolojia ya Elimu wenye uzoefu mkubwa katika kufundisha na kufanya tafiti kuhusu ujifunzaji, tabia za wanafunzi, na maendeleo ya kisaikolojia ya wanafunzi wa rika mbalimbali.
Mhadhiri mwandamizi katika fani hii, Dkt. Christina Mbilinyi, anashirikiana kwa karibu na wanafunzi si tu darasani, bali pia kuwashauri masuala ya kitaaluma na kuwajengea uwezo wa kuwa waelimishaji bora, wanaojua namna ya kuwasiliana, kuelewa na kusaidia wanafunzi wao kwa ufanisi.
π― Ukiwa na ndoto ya kuwa:
β Mwalimu mwenye uelewa wa kina wa ujifunzaji
β Mshauri wa kielimu
β Mtaalamu wa maendeleo ya mtoto
MUCE ndiyo mahali sahihi kwa safari yako ya kitaaluma.
π Dirisha la Udahili bado liko wazi hadi 10 Agosti 2025!
π Wasiliana nasi kwa msaada wa kujiunga:
+255 753 469 546 | +255 764 875 468
#MUCE #SaikolojiaYaElimu #WanataalumaWandamizi #ElimuBora #Udahili2025 #SomaMUCE #JiungeNaMUCE #ChuoChaWalimuBora
π MUCE ina Wataalamu ambao ni Wahitimu wa MUCE Waliofikia Ngazi za Kimataifa!
MUCE inajivunia kuwa na wataalamu waliokulia, kusomea na sasa kufundisha hapa chuoni β mfano hai ni Dkt. Japhace Poncian, Mtiva wa Kitivo cha Insia na Sayansi za Jamii, mtaalamu mahiri wa taaluma za Maendeleo na Siasa, ambaye pia ni mhadhiri na mtafiti mwenye kutambulika kitaifa na kimataifa, na muhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Leeds (Uingereza) na Newcastle (Australia).
Akiwa ni mmoja wa wanataaluma waliopitia MUCE na sasa anashika nafasi ya juu ya kiuongozi, anaonesha wazi kuwa MUCE ni mahali ambapo vipaji huibuliwa, huendelezwa, na huishia kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii.
Unapochagua kusoma Masomo ya Maendeleo au Sayansi ya Siasa hapa MUCE:
β Unafundishwa na wataalamu wenye uzoefu wa ndani na mtazamo wa kimataifa
β Unajifunza kwa kuzingatia changamoto na fursa halisi za jamii
β Unajiandaa kuwa kiongozi wa kesho katika maendeleo ya kijamii na utawala bora
π Dirisha la Udahili linaendelea hadi 10 Agosti 2025!
π Wasiliana nasi kwa msaada wa kujiunga:
+255 753 469 546 | +255 764 875 468
#MUCE #WanataalumaWetu #MaendeleoNaSiasa #HomeGrownExpert #ElimuYaKimataifa #Udahili2025 #JiungeNaMUCE #ViongoziWaKesho