Mungu Kwanza. Uzima wa milele upo na moto wa jehanam upo tumrudie Mungu kwa toba, kufunga na kusali naye atatusamehe makosa yetu na kutupa mwanzo mpya.
Jinsi ya kumtaka Roho Mtakatifu atuombee ipasavyo;
1.Jisalimishe kabisa kwa Mungu.
2. Omba kwa unyenyekevu na imani.
3.Soma NENO LA MUNGU
4.Tafuta utulivu na usikie sauti yake ya ndani.
5. Omba hata kama hujajua nini cha kusema. Acha Roho Mtakatifu achukue nafasi.
Mbinu anatusaidia Roho Mtakatifu kuomba ipasavyo;
1.Kuomba kwa kunena kwa lugha kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
2.Kutuombea kwa mambo yasiyoweza kusemeka.
3.Kutufundisha mapenzi ya Mungu.
4.Kutupa nguvu na ujasiri wa kuomba.
5.Kutufundisha kujisalimisha kwa Mungu.
Namna ya Kuomba wakati hujui kuomba ipasavyo(Warumi 8:26 - 28)
Huu mstari hauzungumzii jinsi ya 'KUOMBA' ila unazungumzia jinsi ya 'KUOMBA IPASAVYO' kwa kipimo cha MUNGU sio kwa kipimo chetu.
~ Mwl Mwakasege
Binafsi Mwalimu Christopher Mwakasege nimemjua zamani sana, kipindi ambacho huduma yake bado haijakua kuifikia nchi nzima, akifanya huduma Arusha na Kilimanjaro (Alifika mpaka vijijini, Mbaga-Msindo, early 1990โs), tangu miaka hiyo hadi leo hii kitu hajapoteza ni UNYENYEKEVU๐๐ผ๐๐ผ.