Epuka sana kukaa na watu mnaofanana mawazo na kujizungushia uzio dhidi ya wale wengine msiofanana nao mawazo. Mtaishia kuumua ujinga wenu na kuzalisha ujinga wa kikundi. Ukiwa kwenye kundi lisilo pishana mawazo, ama lenye mwanakundi hata mmoja msiofanana nae, hama. Utachina!
Biashara ya Mobile Money imekuwa chungu sasa. Mambo ya Lipa hapa na ubunifu wote wa vijana unakwenda kupotea kwa ongezeko la makato makubwa.
Sikatai kutafuta vyanzo vya pesa ili kuleta maendeleo, ila kwa upande huu uliochaguliwa unaua vyanzo vingi vya mapato.
Inaanza na fikra💡 Lakini fikra nzuri huhitaji utekelezaji makini!
//
It starts with an idea, but remember, a good idea requires better execution! #throwback
Usichague kazi kwasababu hujaisomea au hauna ‘passion’ nayo.
Utafanyia kazi ‘passion’ yako kwa ufanisi zaidi ukiwa na uhakika wa kula.
Tofautisha ulazima na hiari.
Kabla hujamkatia mtu rufaa kwa Mungu, jiridhishe ikiwa umetimiza sehemu ya wajibu wako dhidi ya unayemshitaki, unalolishtakia, na kuwa nafsi yako ni safi juu ya hilo unalolishtakia kwake, ama sivyo sehemu ya hukumu yake kwake inaweza kukuhusu na wewe mlalamikaji. Haki ni msumeno!
Anayetaka kuzozana na wewe, anaamini bado suluhu yaweza kufikiwa kwa mazungumzo. Jadiliana nae. Ni heri kutofautiana mdomoni kuliko kila mmoja kujichukulia maamuzi yake kivyake moyoni. Yanayotatulika ni yale yanayojadiliwa. Wanaozungumza, hawagombani. Hakuna lisilozungumzika!
Je unajua kuwa alama za vidole ni za kipekee kwa KILA BINADAMU (hata mapacha hawafanani) na alama hizi hazibadiliki na umri?
Kama alama hizi zilivyo za kipekee ndo ujue karama, vipaji na riziki yako ni za kipekee - zitumie vizuri!
Na usijilinganishe na mwingine #TembeaNjiaYako
Ogopa zaidi mtu anayekukalia kimya ukimkasirisha. Ukimya wake si lazima iwe ni ishara ya kusalimu amri, bali waweza pia kuwa ni tahadhari na onyo kwako au aweza kuwa anakutafutia fursa na muda (timing) wa kukushushia hasira yake. Kuwa mwepesi wa kusoma ukimya wa uliyemkasirisha!
Kuna watu wanatembea na mizigo ya Matatizo na majonzi moyoni mwao, Ukipata nafasi ya kumjulia hali mtu mjulie, Ukipata nafasi ya Kumsaidia msaidia msaidie
Haupungukiwi kitu 📌
Kuwa makini sana na marafiki pia wanaokufariji wakati wa shida inawezekana wao ndio wakawa chanzo cha shida zako, mtegemee sana Mungu maana yu mwema wakati wote atakupigania kwa kila unaekutana nae...😔