This is not mine. This is yours. This is ours.
From all the players, staff and everyone involved in the club, to you guys who supported us every single day of the season.
Grateful for your love and support ❤️
Ukatili hauanzi kwa tendo kubwa la mwisho, huanza kwa ukimya mdogo unaorudiwa. Jamii inaposhuhudia maumivu ya mwingine na kugeuza macho, si kwamba imekubaliana waziwazi, bali imeanza kuzoea. Na mazoea ndiyo hatari zaidi, kwa sababu huondoa mshangao, huua huruma, na polepole hubadilisha kilichokuwa kisichokubalika kuwa cha kawaida.
Kuna mvutano wa kimaadili kati ya hofu na wajibu. Mwanadamu ana haki ya kujilinda, lakini pia ana wajibu kwa wengine. Tunapochagua kimya kwa sababu ya hofu, tunakuwa tumelinda nafsi zetu kwa muda mfupi, lakini tumeweka hatarini utu wa pamoja kwa muda mrefu. Hapo ndipo jamii huanza kupoteza mwelekeo, si kwa sababu watu waovu ni wengi, bali kwa sababu wema umechagua kukaa pembeni.
Hata hivyo, si sahihi kuwalaumu wote kwa uzito mmoja. Wapo wanaopaza sauti, wanaotafuta haki, na wanaobeba gharama ya kusema ukweli. Hawa ndio chembe za dhamiri ya jamii, ukumbusho kwamba utu haujafa, umejeruhiwa tu. Swali la msingi si nani alaumiwe zaidi, bali ni kwa kiwango gani kila mmoja yuko tayari kubeba sehemu yake ya wajibu.
Haki si tukio, ni mchakato unaohitaji ujasiri wa kudumu. Ikiwa ukimya ndio ulioruhusu ukatili kuota mizizi, basi sauti hata ndogo ndiyo itakayouondoa. Na pengine hapo ndipo tumaini linapoanzia, katika uamuzi wa mtu mmoja mmoja kukataa kuzoea kile ambacho hakipaswi kuwa kawaida. Kifo hiki kinasikitisha sana, lakini imekuwa kawaida kwa Nchi yetu.
HE IS A PATHOLOGICAL LIAR !!!
He damn sure knows that they killed more than 500, and it was under their own orders.
Illegitimately claimed the presidency & parliamentary house, and Issues that shrewd committee of inquiry in attempt to sanitize themselves after realizing the truth is out in spite of their internet shutdown, media coercion & public threats.
Pathetic !!
Uwepo wa Majaji Wakuu wawili wastaafu katika tume hiyo, ungetakiwa kuleta utimamu wa kisheria na kuziba mianya na mapengo ya kisheria. Ni bahati mbaya sana, hata raia wa kawaida wameyaona mapengo mengi.
Tume za uchunguzi wakati mwingine hufanya kazi kwa mujibu wa hadidu za rejea (terms of reference). Hata hivyo, ikiwa matokeo ya tume hiyo yanaathiri haki, mali, au sifa ya mtu, lazima kanuni za haki ya asili zitumike.
Ni jambo la kushangaza kuona mchakato wa kisheria au wa kijaji ukikwepa misingi ya kisheria na haki ya asili (natural justice), hususani unapoongozwa na watu wenye uzoefu mkubwa na ubonezi wa juu katika sheria.
Katika ulingo wa sheria ya ushahidi, haki ya kuhoji mashahidi (Cross-Examination) ni nyenzo muhimu zaidi ya kupata ukweli. Bila dodoso, mahakama (au hiyo tume) itakuwa inategemea simulizi za upande mmoja.
Katika sheria, cross-examination inajulikana kama injini kuu ya kisheria iliyowahi kuvumbuliwa kwa ajili ya kubaini ukweli (the greatest legal engine ever invented for the discovery of truth). Hutakiwi kuikwepa.
Bila mtuhumiwa au upande mwingine kupata fursa ya kumhoji shahidi, ushahidi huo unabaki kuwa wa upande mmoja (ex-parte). Tume inakuwa imejenga ukuta badala ya daraja katika kutafuta ukweli na haki.
Ushahidi wa aina hiyo kitaalamu unakosa kile kinachoitwa "Admissibility weight" kwa sababu haujafanyiwa jaribio la moto (fire-testing). Mchakato huo unakiuka misingi ya Haki ya Asili (Natural Justice).
Katika mahakama nyingi, ushahidi ambao haujapita kwenye dodoso huchukuliwa kama ushahidi dhaifu au wakati mwingine hukataliwa kabisa kwa sababu haujafanyiwa majaribio ya ukweli. Haujapimwa.
Dodoso husaidia kufichua uongo, upendeleo, au makosa ya kumbukumbu ya shahidi. Dodoso ndiyo njia ya kupima kama shahidi ni mwaminifu. Je, ana chuki? Je, ana maslahi ya kifedha? Maelezo yake yanalingana?
Bila maswali ya dodoso, uaminifu (credibility) wa shahidi hauwezi kuthibitishwa, na hivyo ushahidi wake hauwezi kuwa na probative value ya kumfunga mtu au kumwajibisha. Majaji wastaafu wanafahamu hilo.
Kupuuza dodoso ni kuubadili mchakato kutoka wa “kisheria” na kuwa wa “kiutawala” au “kisiasa,” jambo ambalo linafifisha dhana ya utawala wa sheria. Ndiyo wamekwepa kuwataja wahusika wa hayo mauaji.
Haki ya Kusikilizwa (Audi Alteram Partem). Hii ni nguzo ya kwanza ya haki ya asili—kwamba hakuna mtu anayepaswa kuhukumiwa bila kusikilizwa. Wametuhumiwa watu na makundi, hawahojiwa.
Right to Hearing: Ikiwa tume ilikusanya tuhuma dhidi ya watu fulani bila kuwapa nafasi ya kujitetea (right to be heard), ripoti au mapendekezo ya tume hiyo yanaweza kupingwa kisheria (procedural impropriety).
Kwa tume inayohusisha majaji wakuu wastaafu, matarajio ya umma na kisheria ni kwamba taratibu hizi zingefuatwa kwa ukamilifu ili kulinda heshima ya mchakato mzima. Badala yake, hatua zimerukwa
Unapokuwa na jopo lenye watu wenye weledi wa hali ya juu (kama Majaji Wakuu wastaafu), tegemeo ni kwamba wataulinda huu mwongozo wa haki ya asili (Natural Justice). Lakini katika tume hii, imekuwa tofauti.
Hao mnaosema walipanga, waliratibu, walifadhili waaandamanaji, mmewafikia na kuwahoji? Huo ushahidi usiokuwa na shaka ni ushahidi wa upande mmoja. Kwanini hamjawafikia waliotajwa, na kuwahoji?
Kitaalamu, Jaji anafahamu, hukumu au hitimisho lolote linalofikiwa bila kushirikisha upande unaotuhumiwa ni batili kisheria (null and void) endapo itatumika kama msingi wa kutoa adhabu/maamuzi ya kisheria.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Narudia tena kusema, mtu yoyote anayekuja na kauli za kusema
🗣️
“KUTOFAUTIANA MTAZAMO SIO UADUI”
Au sijui eti
🗣️
“USILAZIMISHE TUFANANE MTAZAMO NA MAONI”
Mtu huyo ni hana akili na hajui anachoongea!!
Yapo masuala tunapaswa woteeeee kuwa na mtazamo mmoja na maoni ya kufanana!!
MASUALA KUHUSU UHAI WA WATU NA HAKI YA KUISHI!!
Yani sisi tunapinga mauaji then ww unatuambia hatupaswi kufanana mitazamo, means wewe huyapingi mauaji? Unataka yaendelee?
Unataka utekaji usipingwe? Unataka tutofautiane mtazamo kuhusu kupinga utekaji? Wewe ni mjinga kabisa!!
Yapo mambo yanapingwa na kila taasisi duniani, so yanapaswa kufanana mtazamo na sio kila mtu awe na mtazamo wake!!
Mauaji/Haki ya kuishi!!
Hili linapingwa na waislamu/wakristo/makabila yote/Katiba ya nchi/Sheria za nchi/Tamaduni/Mila/Mungu/Yesu/Mtume!!
Wote hao wana mtazamo mmoja kuhusu hilo, then wewe uje useme kutofautiana mtazamo sio uadui!!
WEWE NI ADUI TU COZ UKO KINYUME NA KILA TAASISI DUNIANI!
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 167
Tumerudi tayari.
Majaji wameingia, na Mhe. Lissu nae karudi.
Kwa dalili zilivyo naona ni kama Mhe. Lissu hajapatiwa Chakula, sijui lakini ngoja tusikie.
Majaji wanaandika kidogo pale.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude anasema uwakilishi wetu kama ulivyokuwa awali, tuko tayari kama ameshakula labda tumsikilize.
Mhe. Lissu: Mhe. Jaji sijala lakini naomba tuendelee tu ivo ivo maana issue ya mimi kupewa chakula imeshindikana.
Magereza wamekataa kunipatia Chakula. wamesema nitaenda kula Gerezani.
Majaji ni kama wamekasirika au wamechanganyikiwa hapa.
Renatus Mkude amemuita askari Magereza wanaongea ongea hapa sijui wanaongea nini?
Jaji Ndunguru anasema Chakula ni haki ya msingi kabisa na haitakuwa sahihi kuendelea na shauri hili bila mshitakiwa kupatiwa Chakula.
Wenzetu wa Magereza mzingatie kuleta Chakula, itakuwa ni kinyume cha haki za binadamu kumnyima mshitakiwa chakula.
Tunaomba kuahirisha hadi kesho saa tatu asubuhi na mtakumbuka tulisema shauri litasikilizwa hadi saa 11 jioni.
Kuanzia kesho hakikisheni anapata Chakula Mchana.
Nahairisha kesi hii hadi kesho saa tatu kamili asubuhi. 13/02/2026.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 166
Imepigwa High Courtttttt
Majaji wameingia.
Mhe. Lissu alivyoingia anauliza mmekula? Mimi mwenzenu sijala kabisa.
Majaji wamewasha kipaza sauti pale na karani anasoma namba ya kesi.
Anasimama Renatus Mkude anajitambulisha na kusoma anaoambatana nao na kusema Mshitakiwa yupo.
Shauri lilipangwa na tunae shahidi P6 tuko tayari.
Mhe. Lissu anasema na mimi niko tayari. I ngawa sijala mnapofunga watu mjue hilo.
Renatus Mkude anasimama anasema kula ni haki yake ya msingi kama hajala tuahirishe maana kula ni haki yake. nashangaa kwanini hajala.
Mhe. Lissu anasema nimesema niko tayari maana sheria inasema mahabusu anajinunulia chakula na hela zangu wanazo wenyewe za Chakula.
Na huu ndo utaratibu wa wafungwa wote kwenye nchi hii.
Wakienda Mahakamani wanashinda njaaa. Mimi lazima niseme ili mambo haya yabadilike sio kwangu tu na kwa watu wote.
Hawa Mawakili wa Serikali na nyie majaji nafikiri mmekula mchana huu.
Huyu atakuwa ni shahidi wa tano yaani PW5 lakini jina lake ni shahidi P6 kwa Mujibu wa yale majina.
Hili jambo limewachanganya sana Majaji wanajadili kule juu sana.
Hii kitaalamu nimeambiwa inaitwa Equivocal plea yana unakubali jambo wakati umechanganya mambo humo ndani, hujakubali direct ndio maana imewavuruga.
Mh. Lissu anasema niko tayari kuendelea lakini mimi sijala.
Majaji wanaogopa.
Jaji Ndunguru: Sasa Mshitakiwa tuambie nani mwenye wajibu wa kukuletea Chakula ni akina nani? Ili tumwambie akuletee Chakula.
Mhe. Lissu: Ni Magereza hawa ndio wana wajibu na Dada yangu yupo hapa wanaweza shirikiana nae.
Jaji Ndunguru: Sasa tu breki dakika 20 ili wakakupatie Chakula.
Inapigwa Courttt kesi inaahirishwa.
Wananchi walioingia Mahakamani wanawaka kinouma. Wanasema hao Magereza na serikali wanamuonea Lissu kwanini hawampi Chakula. Wakinamama wanalia sana.
Yanapigwa sana maombi humu, Watu wamepandisha mori kesi imeahirishwa.
So tukutane baada ya dakika 20.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 164
Anamalizia Mhe. Lissu
Shahidi wa kificho: Hapa Hayapo.
Mhe. Lissu: Ahsante sana. Unajibu vizuri napenda.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji sina swali na shahidi..
Jaji Ndunguru anawaita Mawakili wa Serikali: Je mtakuwa na swali lolote kwa ajili ya re examination.
Ajuaye anajibu kuwa sisi hatuna swali lolote.
Jaji: Sasa shahidi tunakuruhusu tumemalizana na wewe.
Kimlango kinafungwa na Majaji wanaandika kidogo.
Anasimama Wakili wa Serikali anasema tunaomba ahirisho hadi saa nane ili tuendelee na shahidi huyo.
Mhe. Lissu: Sina pingamizi ila waseme shahidi wao ni nani ili nikasome maelezo yake, kama ni wasiri waseme ni P gani pia. Nikasome ili tukirudi niwe tayari nimeshapitia maelezo yake vizuri.
Renatus Mkude Mheshimiwa Jaji tungepata ahirisho hadi kesho ingekuwa jambo jema sana, muda huu hajafika pale ofisini kwetu ndio maana tunaomba ahirisho.
Jaji Ndunguru: jana tulielekeza, tukutane saa nane na mje na mashahidi tafadhali sana.
Kesi imehairishwa mpaka saa nane mchana.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 12, 2026
Jana tuliishia Part 159 so leo tunaendelea na-;
Part 160.
Ni siku nyingine, karibuni tena leo kwenye Darasa la Sheria.
Mhe. Lissu tayari ameingia, kama kawaida Wananchi wamepiga shangwe ile ya Rais! Rais! Rais!
Majaji nao wameingia kama kawaida yao wapo watatu.
Naona Kizimba kimetobolewa kidogo upande wanaokaa Majaji ila kama shaidi ni mfupi hata Majaji hawawezi kumuona ila tuendelee.
Jaji Ndunguru anasema sasa tuendeleee.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude Wakili wa serikali Mkuu anasaidiwa na Ajuaye, Katuga, Ignas, Thawabu, Cathbert na Winiwa Kasawa tunaiwakilisha Jamhuri na mshitakiwa yupo hapa Mahakamani.
Shahidi P11 ana dharula lakini leo tumekuja na P5 leo kama atakuwa tayari tutaendelea.
Jaji Ndunguru anasema Mshitakiwa unasemaje?
Mh. Lissu anajibu anasema kimsingi niko tayari isipokuwa niliambiwa ni P11 sasa nipeni dakika 5 niyatafute maelezo ya huyo P5 niyapate kwanza hapa halafu tuendelee kushughulika nae mimi sina shida kabisa.
Ngoja nitafute hayo maelezo yake vizuri.
Jaji Ndunguru anasema sasa sisi tunakupa dakika 10 sio tatu na unaruhusiwa kukaa pia sio lazima usimame sana hapo.
Lissu anajibu hakuna shida kabisa Waheshimiwa Majaji.
Mheshimiwa Lissu ametafuta kidogo makabrasha yake hapa amepata hayo maelezo amekaa kuyasoma na amemaliza anasema tunaweza kuendelea Waheshimiwa majaji.
Jaji Ndunguru tunamuomba shahidi.
Anasimama Renatus anasema shahidi ataongozwa na Wakili Ajuaye Nzengeli Wakili wa Serikali.
Anasimama karani anateta jambo na Jaji anashuka chini kuongea na Mawakili wa Serikali.
Anarekebisha mitambo pale.
Tunasubiri kuona nini kinaendelea.
Anaingia askari mmoja kwenye kile kizimba, anapelekewa kipaza sauti huyo shahidi.
Kile kizimba kimefunguliwa kidizaini ambayo Majaji wao wanadai wanamuona.
Jaji anasema tutamuuliza kuhusu umri wake na dini yake kabla ya kutoa ushahidi wake.
Umri wangu ni miaka 33.
Dini yangu ni Muislamu.
Huyo ni Shahidi P5 Ambae ni shahidi wa nne (4) kwa maana ya (PW 4) lakini jina lake alilobatizwa ni P4.
Ajuaye anasimama anasema shahidi unanisikia hapo?
Unaishi Wapi?
Naishi Kibangu, Ubungo Mkoa wa Dar es salaam.
Shahidi ana lisauti fulani ningesema linafanana na la nani ila acha niache.😂
Anasema anafanya kazi ya Machinga, mjasiriamali, saa nyingine naosha magari.
Unauza bidhaa gani?
Nauza viatu, saa zingine nauza soksi.
Shughuli zangu nafanyia Mchikichini, Kariakoo, Posta ya zamani, Feri hadi Posta Mpya.
Ajuaye anaendelea kumuhoji hapa na shahidi anajibu kama ninavyowaeleza.
Elezea sasa bidhaa zako unachukulia wapi?
Shahidi wa kificho ; Ilala Boma, Sokoni..
Eleza tar. 04/04/2025 ulikuwa wapi?
Shahidi wa Kificho: Nilikuwa Posta ya zamani Garden eneo la NBC Bank nikiwa naperuzi mitandao ya kijamii kwenye simu yangu?
Ajuaye: Sasa eleza ulikuwa unaperuzi kwenye mtandao gani?
P5: Facebook, Whatsapp na Youtube, nilikuwa naperuzi kwa kutumia simu yangu aina ya smartphone sonny experior Galaxy
Sasa wataalamu wa simu mtatusaidia hapo hiyo aina ya sim sie wengine hatufahamu zaidi. Acha tuendelee kumsikiliza shahidi.
Anaendelea hapa.
Wakati naperuzi niliona video ndogo ikimuonesha Tundu Lissu, niliona video Facebook.
Ni kama Majaji wamechoka wanamshangaa Shahidi, sisi hatumuoni lakini sura za majaji ni kama wanakunja.
Niliingia faceebok kwanza lazima uwe na account na bando la kutosha. Mimi niliingia kwasababu nilikuwa tayari nina account yangu.
Maswali anayoulizwa shahidi na Wakili wa Serikali na Majibu yake ni kama anajibu kwa kusoma mahali maana kuna muda anajibu jibu ambalo haliendani na swali.
Video ilikuwa ya Tundu Lissu, mimi namfahamu kwa kutumia vyombo vya habari na mitandaoni.
Wakili wa Serikali : Na wewe binafsi unamfahamuje?
P5 : Na mimi namfahamu.
Basi nikubadilishie swali, Tundu Lissu ni nani?
Shahidi: Tundu Lissu ni mwanasiasa.
Part 161 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.