Tundu Lissu ameshinda nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kupata kura 513 sawa na asilimia 51.5, akimshinda aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye amepata kura 482 sawa na asilimia 48.3 huku Odero Charles Odero akipata kura 1 sawa na asilimia 0.1.