My AudioMack is at 803 followers
Abeg on this Good Sunday with the LOVE OF GOD
PLEASE FOLLOW MY AUDIOMACK, comment on my music and listen to my 4 songs #Sundayvibes
๐๐ฝClick๐๐ฝ
https://t.co/TtUdiLyNZ7
Nimepigiwa simu na watu wengi wakitaka kujua msimamo wangu kuhusu yanayoendelea. Msimamo wangu ni huu;
1. Naunga mkono #NoReformsNoElection kwa sababu nimechoka kuona watu wakifa, kuumizwa, kugeuzwa walemavu, na wengine kusota gerezani kwa sababu tu ya uchaguzi. Nilipiga kura mara ya kwanza mwaka 2005 nikiwa na miaka 19, na tangu wakati huo nimeona kasoro nyingi kwenye chaguzi. Hivyo basi kabla ya kufanya uchaguzi mwingine turekebishe kasoro hizo kwanza.
2. Maslahi ya uongozi hayawezi kuzidi haki za watu. Cheo chochote kinachosababisha wengine waumie, wauwawe, wafungwe jela hicho sio cheo ni laana.
3. Mwenye hekima hujifunza kwa makosa ya wengine, lakini mjinga hujifunza kwa makosa yake mwenyewe. Kuna vyama vimekataa kujifunza kwenye chaguzi ambazo Chadema ilishiriki na kudhulumiwa. Wanaamini mwaka huu wao hawatadhulumiwa. Wapare husema kenge huwa hasikii mpaka damu zimtoke masikioni.
4. Hatukupoteza muda wetu, jasho letu na damu yetu ili kutafuta ubunge au udiwani. Tulijitoa ili kutafuta HAKI. Hivyo usiogope kukosa cheo kwa kupigania HAKI. Cheo huja na kupita, lakini heshima hudumu.
5. Cheo hukoma, Mali huisha, sifa hufifia, lakini heshima huishi milele. Heri kuchagua heshima, kuliko mali nyingi na dhahabu (Mithali 22:1).
6. Tamaa ya muda mfupi isikufanye ukaharibu heshima uliyojenga kwa miaka mingi. Usiuze utu wako kwa faida ya haraka. Kumbuka dakika moja ya tamaa huweza kujenga majuto ya vizazi na vizazi.
7. Uongozi si cheo, uongozi ni namna unavyohusiana na watu. Usikimbilie kuwa mbele ya watu, kimbilia kuwa na thamani kwao. Cheo si nafasi ya kutukuzwa, ni nafasi ya kutumika.
8. Ukishindwa kudhibiti tamaa ya fedha na cheo, huwezi kuwa kiongozi mwenye heshima, kwa sababu heshima na tamaa havikai nyumba moja.
9. Kukataa uovu leo ni kupanda mbegu ya haki kwa vizazi vya kesho. Ujasiri wa kusema hapana kwa mabaya leo huandika historia ya kesho yenye heshima na matumaini.
10. Mtu mwenye hekima hachagui njia rahisi, huchagua njia sahihi hata kama ni ngumu. Ukiona njia ya mkato isiyo na maadili, jua siyo njia ya mafanikio bali ya anguko lako. Maandiko yanasema iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti - Mithali 14:12
๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Wabunge wote wanaosimama na upande wa wananchi kuwatetea
Wote Serikali ya Samia wanawaona maadui
Hawapewi Nafasi za kugombea ๐ญ๐ญ๐ญ
Oleshangai,olesendeka , Mpina,gambo
Wamekatwa kugombea ili kusiwe na sauti ya mtetezi mmoja @MariaSTsehai@HildaNewton21