Simba ya kipindi cha pili dhidi ya Fountain Gate, ya 4-3-3 yenye Ahoua, Abraham na Maema inaweza kuwafanya Simba kuwa tishio zaidi kwenda mbele
Nafasi za kutosha zimetengenenzwa, lakini wachezaji wote bora walikuwa maeneo ya kutoa ubora wao akiwemo Mpanzu alieanzia zaidi pembeni
Mwalimu Romain Folz anajua muda na namna ya kufanya mabadiliko. Kila mechi mpaka sasa akifanya mabadiliko lazima athari ipatikane
Mabadiliko ya leo yameibadilisha sana mechi licha ya Pamba kuja kama walivyofanya kipindi cha kwanza
Hii ni ishara ya mwalimu anaejua kuusoma mchezo
Kwa unaetaka kupata undani wa kiufundi na kiuchezaji wa timu za ligi kuu, gazeti la Ligikuu_xtra litakupa maandiko ya kina kuhusu timu na wachezaji unaowapenda wa ligi ya Tanzania
Lakini fuatilia ukurasa wa @ligikuuxtra unaoambatanisha video fupi zenye uchambuzi yakinifu zaidi.
Jeuri ya pesa ndio imemleta Selemani Mwalimu kwa mkopo Msimbazi. Pale Wydad, Mwalimu analipwa $2500, takribani Milioni 6 na nusu kwa mwezi.
Mo kampa mshahara Milioni 15 kwa mwezi na Signing fee Milioni 120 kwa huo mwaka mmoja. Fadlu pia kamhakikishia game time ya kutosha klabuni
Hii ndio barua kutoka Umm Salal kwa ajili ya uhamisho wa Mzize. Ofa ni Dola 900,000 itakayolipwa kwa awamu mbili. Barua imetoka kwa mkurugenzi wa ufundi, Abdulaziz Bin Saoud Al Thani, ndugu na Mwenyekiti, Abdulaziz Bin Abdulrahman Al Thani na ilijibiwa siku 4 baadae na Yanga.
Yanga walishaikubali kitambo ofa ya Umm Salal kwa ajili ya Clement Mzize. Tatizo liko kwa msimamizi ambae dili hakulileta yeye kwaiyo ikifanyika biashara hii hakuna atakachopata.
Mavambo ana stamina ndogo kama Box to Box Midfielder.
Mavambo kuna mchezaji pale, ana hold na kukokota mpira vizuri shida ni nishati yake na ndio maana anachelewa kwenye matukio mengi ya kukaba lakini hata ya kushambulia.
Hata uzuri wake ulikuwa wa vipindi, sio dakika zote 90.
@mee_nicodemus Bro hivi sasa angalia hata Ulaya namba 10 wengi ambao wanafukuziwa, Bayern walikuwa na Muller sasa Musiala, City wamemchukua Cherki, Liverpool wamemchukua Wirtz, Arsenal wanahusishwa na Eze. Wote hao Wana kitu kimoja kinafanana, ni 'Elite Dribblers'
Yanga haihitaji namba 10 mwingine. Vilabu vingi vikubwa hivi sasa vinatafuta namba 10 ambao wanaweza 'kudribble' na kutafsiri nafasi kwa haraka.
Yanga wana wawili, Pacome Zouzoua na Max. Watenge bajeti nzuri kupata hata mawinga wawili wenye ubora watakaowasaidia sana kimataifa
Sajili bora kabisa za Injinia ndani ya Yanga ni za viungo wa chini wa nje. Aliwaleta Aucho na Bangala ambao wamelipa vizuri sana
Pacome mwenyewe alisajiliwa kama kiungo wa chini kuwa mbadala wa Bangala.
Kwa Mussa Bala Conte muda utaongea lakini nampa faida pia Injinia hapa.
PRESHA🥶👋
Kennedy Musonda ameshindwa kuibeba presha ya kuwa Mshambuliaji tegemezi kwenye klabu kubwa kama Yanga...
Kuondoka kwa Mayele msimu juzi ilikuwa ndio nafasi yake nzuri kujimilikisha nafasi hiyo lakini ikawa afadhali ya wengine mbele yake. Na confidence yote ikapotea.
Azam wameachana na Winga mzuri sana ndani ya Gibril Sillah, ni vile amekosa nyota ya kuzungumziwa sana lakini ana kila kitu.
Finisher mzuri sana ndani na nje ya box mwenye utulivu mkubwa sana. Uhatari unaofanana pembeni na katikati ya uwanja. Sijiulizi kupata ya winga kama hii.
Ligi yetu imeruhusu wachezaji ambao hawako timamu hata kwa asilimia 85 kuendelea kuonekana bora na ndicho alichoondokea Aziz msimu uliopita.
Aziz amekwenda Wydad physically akiwa chini licha ya kiwango alichoonesha akiwa na Yanga. Sasa anatakiwa kuwa 100% fit kutoa kilicho bora.
DYNAMIC PRESSER💨...
Kwangu bila mpira kwenye Build up ya mpinzani kwenye pressing hakuna zaidi ya Mudathir Yahya kwenye ligi yetu...
Kile anachoweza ku-offfer hasa timu ikiwa haina mpira kwangu hakuna mjadala kabisa kuhusu uhitaji wake kwa misimu mingine kadhaa.
DUKE 'MACHINE' ABUYA...
Binafsi kwangu amekuwa ndio kiungo bora wa chini wa Yanga msimu huu... Abuya anakupa karibu kila kitu, nishati, passing, na mikimbio ya mwisho kwenye boksi...
Sanaa yake ya kuzuia bila mpira ni bora sana, hakuna faulo wala kadi za ovyo, UNDERRATED.
KIVUMBI CHA PUMZI...
Hiki kiungo cha Abuya, Max na Muda kwa pamoja ni bonge la balaa kwa mpinzani... Hizo ni Engine tatu bora zaidi nchini na zote ziko uwanjani kwa wakati mmoja...
Kiungo cha mpinzani kinamezwa mazima kwenye upande wa nishati, ufundi ndio battle yao inayobaki.
DICKSON JOB MVP WANGU🥇...
Huyu ndio mchezaji pekee ambaye amekuwa na performance nzuri kwenye kila mchezo wa ligi msimu huu...
Na juu ya muendelezo wake amefuta makosa mengi sana ya kiulinzi ya wenzie msimu huu...
Lakini hata kwenye michuano ya kimataifa na CRDB, Job🔝🔝🔝