Sehemu kubwa ya maamuzi ambayo tunafanya ni matokeo ya vitu ambavyo tunaona, kusikia na kukutana navyo. Hivyo ndivyo ambavyo ubongo wa mwanadamu unafanya kazi. Wasimamizi wa brand wanaweza kutumia udhaifu huo wa ubongo kupenyeza brand zao kwenye akili za walaji kwa njia nyepesi ya kutengeneza vitambulisho vya brand vya aina tofauti. Sio kuishia kwenye logo peke yake au matangazo ya aina moja.
Mteja ambaye anakutana na bidhaa dukani aliyokwisha kutana nayo kwenye mazingira ya nje kabla ya dukani ni rahisi zaidi kuichagua bidhaa hiyo kuliko bidhaa nyingine iliyo na kazi sawa lakini kwa mara ya kwanza amekutana nayo dukani. Ndio maana huwezi kuwaona CocaCola wanapoa. Vile vile ni rahisi zaidi online mtu kufuata tangazo ambalo amekutana na utambulisho mwingine wa brand kwenye mazingira mengine nje kulinganisha na ile ambayo hakuwahi kuona.
Hivyo ndio muundo wa ubongo namna unafanya kazi. Wataalamu wote wa masuala yanayohusu tabia, moja ya mbinu maarufu watakushauri ili kuacha tabia fulani ni kukwambia kupunguza vishawishi vya tabia hiyo ikiweno visual cues.
Kuwabakisha wateja ambao wanatupiwa vishawishi vipya kila siku toka brand zingine ni lazima wasimamizi wa brand kuhakikisha wanaongeza brand visibility kwa namna wataweza, moja ya njia nyepesi ni kutumia brand touchpoints tofauti na kusambaza maeneo mbali mbali.
Hizi ni brand touchpoints zilizo andaliwa kwa ajili ya EastFlow Logistics
Huu ni mfululizo wa Nne katika program yetu ya kuwafundisha vijana wanaopenda Graphics.
@rannygraphics ametuletea Tena ile Masterclass ya Adobe Photoshop na Illustrator kwa siku 11. Kuanzia tarehe 17-28 Feb.
Nafasi zinazidi kupungua, jiandikishe kwa ada ya Tsh 100k tu.
Mkakati mmoja wapo wa kuvunja UMASIKINI katika ukoo wako ni wewe kuanzisha na kutengeneza njia za watoto wako kuendeleza.
Mf:
1. Jenga nyumba Hadi za watoto wako, ili wao waendeleze ulipoishia.
2. Ukifungua Biashara/Kampuni waingize watoto wako ili siku ukifa biashara ziendelee.
3. Wajenge wanao katika mifumo ya Maono, ili waendeleze pale unapoishia.
Watanzania wengi tunazunguka katika mnyororo wa UMASIKINI kwa sababu Kila anaekuja anaanza upya.
Kuna wazazi wanao uwezo mzuri, wana biashara nzuri na kubwa, lakini hawawaingizi watoto wao. Mwisho, unakuta watoto wanahangaika kutafuta kazi na hali wazazi wao wana investment kubwa.
Hapo ndio tunaelewa kwamba Unaweza kuwa Tajiri, lakini Roho ya UMASIKINI inakutesa!!
Jifunze kutoka kwa Wakinga na Wahindi. Utaelewa vyedi.