Mtoto wa Afrika anastahili zaidi ya kuota ndoto anastahili nafasi ya kuzitimiza.
Leo tunakumbushwa wajibu wetu wa kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora, ulinzi, huduma muhimu na mazingira salama ya kukua na kufanikiwa.
Kila msichana ana haki ya kupata elimu, taarifa sahihi za afya ya uzazi na nafasi ya kutimiza ndoto zake. Kupitia miradi mbalimbali tunaendelea kuwawezesha wasichana kupitia elimu, ulinzi wa haki zao na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na kidijitali.
Vijana hawawezi kusubiri kesho ili wawe sehemu ya maendeleo wanahitaji kushirikishwa leo.
Kupitia kujengewa uwezo, kuendelezwa vipaji, kupewa ujuzi wa maisha na nafasi za uongozi, vijana wanakuwa chachu ya mabadiliko chanya katika familia, jamii na taifa kwa ujumla.
Kupitia majadiliano ya jamii, tunajenga uelewa, kuimarisha ushirikiano na kuchukua hatua za pamoja katika kuzuia na kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Tukisimama pamoja, tunaweza kujenga jamii salama, yenye usawa na heshima kwa kila mtu.
@IpasOrg@GlobalFundWomen
Unyanyasaji wa kijinsia hauwezi kumalizwa na mtu mmoja au taasisi moja pekee. Mabadiliko ya kweli yanatokea pale wazazi, walimu, viongozi wa dini, viongozi wa jamii, vijana na serikali wanapounganisha sauti na nguvu zao kwa lengo moja.
Mtoto wa kike akipata elimu, anapata sauti ya kusimamia maisha yake, uwezo wa kutimiza ndoto zake na nguvu ya kubadilisha jamii inayomzunguka.
Ndiyo maana tunaendelea kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa elimu kwa wasichana, kuondoa vikwazo vinavyowazuia kusoma na kujenga
Kupitia elimu, uhamasishaji, utoaji wa taarifa sahihi, na kujenga mazingira salama kwa wanawake na wasichana, tunaweza kuwa sehemu ya kuzuia ukatili huu na kuleta mabadiliko chanya katika jamii
@IpasOrg@GlobalFund@GlobalFundWomen@HerVoiceFund
Baada ya kila sekunde 3, mwanamke mmoja hukumbana na ukatili wa kijinsia mahali fulani duniani.
Hii si takwimu ya kawaida ni uhalisia unaowaathiri wanawake na wasichana wengi kila siku. Ukatili wa kijinsia huathiri afya, usalama, ndoto na ustawi wa maisha yao.
Wasichana wengi hukosa masomo kisa hedhi kwa kukosa uwezo wa kununua taulo za kike. Hedhi isiwe kikwazo cha elimu; kila msichana anastahili mazingira salama na heshima. Tunaungana kuhimiza upatikanaji wa taulo za kike kwa gharama nafuu.
โ@ipasorg@GlobalFundWomen@HerVoiceFund
Tulipata fursa ya kushiriki kikao kilichoandaliwa kwa lengo la kujadili masuala ya ukatili wa kijinsia, hususani ubakaji na ubakaji unaohusisha ndugu, pamoja na namna ya kuimarisha msaada kwa waathirika.
Katika mjadala huo, tulieleza kuwa bado zipo kesi nyingi sana katika jamii,
ambapo kwa sasa tunaendelea kuwasaidia waathirika 26 kupitia mradi wa Chungu Mastering kwa kuwajengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi ikiwemo mafunzo ya ushonaji na stadi za maisha.
tulisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi mbalimbali katika kuimarisha msaada, utetezi na
uhamasishaji wa jamii, na utetezi wa haki za mtoto wa kike, PGWOCADE inaendelea kuchangia kuhakikisha watoto wa kike wanapata fursa ya kujifunza, kubaki shuleni, na kufikia malengo yao.
@IpasOrg@Yplus_Global@GlobalFundWomen
Elimu ni msingi wa maisha bora, usawa wa fursa, na jamii yenye maendeleo. Watoto wa kike wanapopata nafasi ya kusoma katika mazingira salama na yenye usawa, hujengewa uwezo wa kujiamini, kufanya maamuzi sahihi, na kutimiza ndoto zao.
Kupitia programu mbalimbali za elimu,
Kuwawezesha wasichana na wanawake kupitia elimu ya ujuzi ni hatua muhimu katika kujenga jamii yenyea maendeleo endelevu. Kupitia mafunzo, ujasiriamali na kujengewa uwezo katika nyanja mbalimbali, wanawake na wasichana hupata nafasi ya kujiamini, na kujitegemea.
@ipasorg
mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia malezi bora na ulinzi wa watoto umeendelea kuwa chachu ya mabadiliko chanya. Tunaendelea kutumia nguvu ya ushirikiano huu kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii na kujenga mazingira salama na yenye matumaini kwa kila mmoja.
@ipasor @HerVoiceFund
Viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kujenga jamii yenye maadili, amani na mshikamano. Kupitia sauti zao, jamii huendelea kupata mwanga wa kuzingatia utu, haki na usawa katika maisha ya kila siku. Ushirikiano wao katika kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu masuala