Rais wa Hungary, Katalin Novak akiwasili nchini akitokea Rwanda na leo Jumanne atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.
📸 na @pichadunia#pichadunia
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Hungary, Katalin Novák wakihutubia hadhara Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mazungumzo waliyoyafanya ambayo yamelenga kuwepo kwa ushirikiano kati ya nchi hizi kwenye elimu, utalii na masuala ya jinsia.
@pichadunia
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo akimpokea na kumkaribisha mgeni wake ambaye ni Rais wa Hungary, Katalin Novák alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya pili katika ziara yake nchini.
📸 na @pichadunia#pichadunia
Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa, Naibu Waziri wa Fedha Hamad Chande, Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba, Balozi wa Comoro nchini, Ahamada Mohamed, wakiwa kwenye Baraza la Eid katika Msikiti wa Mohammed VI Kinondoni.
📸 na @pichadunia
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akihutubia Baraza la Eid Al Adha 2023 ambalo kitaifa limefanyika mapema hii leo mara baada ya kumalizika kwa swala ya Eid Al Adha katika Msikiti wa Mohammed VI Kinondoni, Dar es Salaam.
📸 na @pichadunia
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameungana na waumini wa kiiislamu kushiriki ibada ya swala ya Eid Al Adha ambayo kitaifa imeswaliwa leo Juni 29, 2023 katika msikiti wa Mohammed VI uliopo Kinondoni, Dar es Salaam ambapo yalipo makao makuu ya BAKWATA
📸 na @pichadunia
Mzazi akiwa amemkumbatia mtoto wake mara baada ya kuwasili Tanzania kutokea Nchini Sudan ambako mapigano makali yanaendelea kati ya Jeshi la nchi hiyo na askari kutoka Jeshi saidizi.
📸 na @pichadunia
Dkt. Stergomena Tax @DrTaxs akizungumza na Waandishi wa habari katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwapokea Watanzania 206 waliowasili waliowasili leo kutokea Nchini Sudan ambako kuna vita kali inayoaendelea.
📸 na @pichadunia#pichadunia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax amewapokea watanzania 206 waliowasili leo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kutokea nchini Sudan ambako mapigano yanaendelea kati ya Jeshi la nchi hiyo na askari wa jeshi saidizi
Picha kutoka kwenye sherehe za mahafali ya 52, Duru ya tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Katika mahafali hayo, Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan alitunukiwa shahada ya juu ya heshima (honorary causer) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Picha na @pichadunia