7th Platoon Commander | East and Central Africa | Husdand to #MDioniz | #Proud Dad | @simbaSCTanzania | Mechanical Flight | @airtanzania | Supersonic Speed
Chombo cha habari kikubwa kama @azamtvtz wanaandika ‘upumbavu’ wa kiwango hiki, vipi hao wengine? Kwamba “aliyejeruhiwa kwenye maandamano azikwa”… majeruhi wanazikwa kwa mujibu wa AzamTV? Wanaogopa kusema aliyeuwawa na risasi ya polisi? Vyombo vya habari bado havipo huru.
Watuhumiwa wa ubakaji wakati wakitoka Mahakamani mmoja wao alisikika akimwambia Cameraman kuwa akimaliza kesi yao atamtafuta.
Kwa namna alivyozungumza ni kama Mtuhumiwa anamtishia Mwandishi asifanye kazi yake ya kuchukua habari, Je hii sahihi kwa mtuhumiwa kuzungumza namna hii tena kwa kujiamini huku akiwa na kesi kubwa inayomkabili?
@wasafifm
#KitengeUpdates
WAZIRI MKUU AFUNGA MAONESHO YA NISHATI 2024.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutenga fedha za kutekeleza miradi ya nishati ambapo katika kipindi cha miaka mitatu zaidi ya shilingi trilioni 8.18 zilitolewa.
📍Dodoma
🗓️ 19 Aprili, 2024
Tanzania Mwalimu anayefundisha shule ya Msingi anapewa sh 220,000 mshahara wa kuanzia yaan ni 1.2% ya mshahara wa mbunge maana Mbunge anapata milion 18 kwa mwezi ambayo inaweza lipa walimu 70! Huku mwalimu hana Nyumba wala mala hela ya ziada!
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela alipokwenda nyumbani kwa Mheshimiwa Malecela eneo la Uzunguni jijini Dodoma kumtakia heri ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, Aprili 19, 2024.
Truly a sad day for the families of our gallant soldiers led by our CDF Gen Francis Ogolla that we have lost today in the air crash in Elgeyo Marakwet, a sad day for KDF and a sad day for our nation.
Having worked with Gen Ogolla in the committee of Defence last Parliament and now this 13th Parliament I can attest that he wasn't just a dedicated soldier but also a fine gentleman and a kind hearted man. May his soul and that of all the bereaved rest in peace.
Let's agree that the KDF and Police choppers and fixed-wings are being misused. Do they get enough time in hangars for repairs and maintenance?
General Ogola travelled like an OCPD and tried to inspect every toilet and cattle dip. Surprising!
Let's all tell Kenya Kwanza leaders to slow down on the misuse of KDF resources. Kibaki's people tried the same, and it claimed many lives.
Jana nilipata wasaa wa kupita Mtaa wa Mombasa, Unguja kuwaona majirani zangu wa zamani Bi. Asha Salum na mumewe, Inspekta Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Rashid Zam Ali. Kushoto ni bintiye Bi. Asha pamoja na mjukuu wao. Bi. Asha nilisoma naye darasa moja shule ya msingi na shule ya sekondari kati ya mwaka 1969 hadi mwaka 1973, idadi ya wanafunzi wa kike katika shule zetu nchini ikiwa chini ya asilimia 20.
Kote ninapopita katika nchi yetu naona hatua kubwa tuliyopiga kielimu, tukiishi maneno ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere ya kwamba kwa watu masikini kama sisi, elimu inapaswa kuwa chombo cha ukombozi, na ukitaka kumsaidia masikini somesha watoto wake.
Nafarijika kwamba nchi yetu imepiga hatua kubwa katika kuongeza fursa za elimu hasa kwa mtoto wa kike, na sasa tuna mgawanyo wa darasa kijinsi wa karibu nusu kwa nusu katika maeneo mengi nchini. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, tumeifanya vyema kazi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo madarasa zaidi ya 20,000, na nina imani kwamba kazi inayoendelea ya kuleta ubora na tija zaidi katika mfumo wetu wa elimu itafanikiwa.
Nimewasili nchini Uturuki kwa ziara rasmi kufuatia mwaliko wa Mheshimiwa Rais @RTErdogan. Mwaka huu nchi zetu mbili zinatimiza miaka 45 tangu kuanza kwa uhusiano wetu wa kidiplomasia. Uturuki ni mshirika wetu mkubwa kiuchumi na ni soko la kimataifa kwa bidhaa zetu linalokua kwa kasi, tukiwa na ukubwa wa biashara baina yetu wa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 350 kwa mwaka.
Ziara yangu ni sehemu ya utekelezaji wa sera yetu ya Mambo ya Nje kupitia Diplomasia ya Uchumi, katika kutafsiri uhusiano wetu na nchi nyingine uwe wenye kuleta tija na kuchangia ukuaji wa uchumi wetu.
Naishukuru Seneti ya Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki kwa kunitunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) katika Uchumi. Nimeipokea heshima hii kwa unyenyekevu na shukrani kwa niaba ya wachapa kazi waume kwa wake nyumbani nchini Tanzania. Mimi ni kiongozi wao, ninayofanya na heshima hii ni kwa niaba yao.
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kenya, Jenerali Francis Omondi Ogolla na wanajeshi wengine tisa katika ajali ya helikopta iliyotokea leo katika Kaunti ya Elgeyo-Marakwet.
Natuma salamu za pole kwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, Mheshimiwa @WilliamsRuto, wananchi wote wa Kenya, familia, ndugu, jamaa na marafiki wa wote waliopoteza jamaa zao katika katika ajali hiyo. Poleni sana.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za ndugu zetu hawa mahali pema peponi. Amina.
Mapema leo nimekuwa na mazungumzo mazuri na kaka yangu, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan. Ziara hii ni mwendelezo wa mageuzi kwenye utekelezaji wa sera yetu ya Mambo ya Nje kupitia Diplomasia ya Uchumi. Thamani ya biashara baina ya nchi zetu imekua; kutoka dola milioni 11 mwaka 2003 hadi takribani dola milioni 350 hivi sasa ikichangia katika ajira, miundombinu, afya, viwanda na elimu ya juu.
Katika mazungumzo yetu tulijadili pia masuala ya ulinzi na usalama ikiwemo kupambana na ugaidi na ushirikiano baina ya nchi zetu katika eneo hilo. Tumegusia pia nafasi ya Uturuki kama mwanachama wa G20 katika kuunga mkono ajenda za nchi za Afrika kwenye majukwaa ya kimataifa.
Tutaendelea na kazi ya kukuza ushirikiano huu ili ulete tija zaidi kwa wananchi wa pande zote mbili.