All people of goodwill and supporters of democracy across the world are relieved to see the trumped up treason charges against Comrade Tundu Lissu collapse, following his acquittal today.
These charges should never have been brought in the first place. Lissu’s only crime was to call for basic reforms to the electoral architecture in Tanzania to guarantee a fair process. He has lost over two years of his life in custody as he fought off the charges.
We encourage Ndugu Lissu, the CHADEMA Party and all our Tanzanian brothers to take heart and remain strong in their pursuit of justice and freedom, in the knowledge that all forces of regression are usually ultimately defeated.
Jason Statham proudly shares pictures of himself and his sugar mama chilling and having a wonderful time together. He doesn't care what the media says.
Truly, age is just a number! ❤️. ➡️➡️➡️
Tanganyika ina HISTORY ndefu kuhusu kosa la UCHOCHEZI
Hii ni mara ya pili kutokea kosa hili kwa mwanasiasa jabari
Mara zote haya makosa yametokea pale ambapo mfumo ulilikomalia madarakani kushindwa kushawishi wananchi na hivyo kuanza kushambulia wanasiasa wenye ushawishi
Kwa sasa anashambuliwa Lissu sababu tuko kwenye hatua za mwisho kupata ukombozi wa pili wa Tanganyika, Kuirudisha Tanganyika kwa Watanganyika
Sura ya Samia ina alama ya Ukoloni kwa Tanganyika, Samia sio Mtanganyika, kama ambayo wakoloni hawakuwa Watanganyika
Mara zote hawa wageni wamefanya mashambulizi makubwa sana kuzuia uhuru kamili wa Tanganyika, Tunataka ukombozi wa pili wa kiuchumi na kisiasa, Tunataka Tanganyika mpya, Tuka karibu na USHINDI #ChangeTanzania
This is misinformation which platform was streaming the case for the family to follow ?
They should kick you out from the furneral , you are running propaganda ''
Leo haya magazeti yote yatapigiwa simu kuambiwa wafute hizi article
tumeshaweka record sawa, mkifuta ni kupoteza muda tu
Hapa ni Samia akiwapiga kamba mabalozi, na hii leo ni ushahidi kwamba mambo wanayoambiwa mabalozi ni uongo, CCM na watu wake hawana heshima na mtu yeyote wala kitu chochote
Kila wanachosema ni uongo,
Jana wameongea uongo mwingi na leo tumepata ushahidi mzuri kwamba hawa wote ni waongo waongo tu
Tanzania’s Suluhu expresses ‘sympathy’ over internet disruptions. https://t.co/iIrsQKBsia
@TheCitizenTz : Samia breaks silence on internet shutdown. https://t.co/SejlFoQlCs
Daily News: No internet disruption, Dr Samia assures diplomats https://t.co/LaPJr8TRWo
Daily Pioneer (AP): Tanzanian President apologises for internet shutdown https://t.co/DGXA6eKYsX
US Interest in Tanzania is not vested upon these criminals, drug dealing regime, it is on its people. To safeguard those interests, kindly sanction these murderers before the country descends into a bloodbath. @USAmbTanzania@MarcoRubio
ALERT: Seikali imeanza kuzima Internet. POLICE nao wameanza kukamata watu maeneo ya Ubungo, Kimara na Mbezi mwisho, wananyang'anywa na simu zao. Vijana kaeni chonjo. Serikali inapika kitu.
Majaji, kwa uamuzi huu mmejivua heshima, mmeondoa kabisa imani ya wananchi kwa mahakama na kuifedhehesha nchi yetu! Dhamiri zenu ziko wapi? Kiapo chenu kina thamani gani? Namshukuru Mungu sina undugu na yeyote kati yenu. Kila mmoja wenu abebe aibu na uwajibikaji wa uamuzi wake. Vyeo vitapita, majoho yatavuliwa, lakini fedheha ya uamuzi huu itawafuata katika historia!
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 502
Mhe. Lissu anaendelea
Anasema uamuzi huu wa kunikuta na hatia na kosa ambalo sikushtakiwa nalo, sikujitetea ni kosa la kutengeneza, effect yake ni kwamba unatoa kinga ya kisiasa kwa wale ambao walihusika mauaji amkubwa ya kisiasa, watatoka na kusema wauaji walishapataikana.
Serikali ya Samia imeua watu wengi zaidi ukiachilia historia ya vita vya majimaji, hawa mass murderers watashangilia sana na uamuzi huu kwasababu mmewapa sababu ya kusema aliyesababisha mauaji ya Oktoba 2025 amepatikana na hatia lakini hii haitafunika ukweli.
Serikali ya Mwalimu Nyerere iliuwa watu 37 mwaka 1977 na iliwajibika, Peter Kisumo alikuwa Mkuu wa Mkoa w Shinyanga alijiuzulu, na wengine akiwemo Mwinyi.
Leo watu 518 walioripotiwa kwa uchache hakuna aliyewajibishwa, uamuzi wenu hautaficha hiyo kashfa.
Kwenye sentences guidelines za Mahakama hii, inasema lazima adhabu ya faini itolewe isipokuwa kama ni grave offence, kosa nililoshtakiwa nalo sio grave.
Waheshimiwa Majaji hukumu mnayo, ambayo mmeagizwa muitoe, itoeni nawashukuruni sana.
Jaji Ndunguru anawasha mic anasema tumesikiliza hoja za pande zote na katika kutoa adhabu tumezingatia sababu kadha wa kadha.
Kwanza mshtakiwa umeomba dhamana ili ukate rufaa, tumeangalia hoja ya ugonjwa na kuwa wewe ni mkosaji wa kwanza, hoja ya adhabu ya faini au kifungo.
Kifungu cha 390 hakijatoa adhabu na ukisoma kanuni ya adhabu kifungu cha 35 kinahusika pale ambapo hakuna adhabu.
Adhabu ni kifungo kisichozidi miaka 5 au fani au vyote viwili na hakijaelekeza faini ni kiasi gani.
Tunajua kuwa pale ambapo fani na kifungo vinakuwa vinatolewa first option ni faini.
Tumesoma na maamuzi mbalimbali na mengine ambayo tumeshayasema mfano kuzuia uchaguzi ni kukiuka katiba, ukisoma Ibara ya 30(1) imeeleza kuwa hutakiwa kuingilia haki za mtu mwingine.
Mahakama inatoa adhabu kwa mshitakiwa kutumikia kifungo cha muda wa miaka 4 na una haki ya kukata rufaa.
Majaji wanatoka.
Naomba Repost yako.
Court sentences Tundu Lissu 4 years jail for incitement
Yaani tulinyaka mpango wenu kumfunga miaka 5 - sasa mkataka kutu discredit mkafuata script yote alafu mkasema miaka 4
🙄
Sisi tunataka muachieni! Majaji hawa wamethibitisha hakuna uhuru wa mahakama!
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 501
Wakili wa Serikali kimsingi anasema kwamba matukio ya vurugu za Oktoba 2025 yalitokana na kauli zangu kama nimemuelewa sawa sawa.
Kwenye kesi hii sina hakika kama mmeletewa ushahidi wa hotuba ya Jaji Chande wala yeye hajaja kutoa ushahidi hapa kuthibitisha hizo vurugu zilisababishwa na vurugu za wanasiasa gani.
Mnaambiwa mnitolee adhabu kali kwa kosa ambalo kama lipo limefanyika kwazaidi ya miezi 6 limefanyika baadae mimi nikiwa gerezani, mkikubaliana na hoja hiyo huu utakuwa ni uthibitisho mwingine kwamba huu ni uamuzi wa maelekezo.
Watu kicheko😂😂😂😂😂
Wakili wa Serikali Mkuu anataka muamini projo za mitandaoni, mkikubali utakuwa ni uthibitisho kuwa ni maagizo.
Wakili wa Serikali Mkuu amewaambia vile vile kwasasa hawana taarifa zozote kama hili ni kosa langu la kwanza, maana yake anaashiria kwamba kuna previous conviction, sasa kwavile hana uhakika mimi nitawaambia ukweli, sijawahi kutiwa hatiani na kosa lolote la jinai, wamenishtaki kwa zaidi ya miaka 24 tangu 2002 hawajawahi kunipata, I have never ever been convicted for a criminal offence, kwahiyo mnapofikiria adhabu lazima mjue kwamba mnatoa adhabu kwa mtu ambaye hajawahi kupatikana na hatia.
Mhe. Lissu anaendelea
Waheshimiwa majaji nafaham mnajua kwamba nina msiba mkubwa sana wa mtu aliyenilea, amenifanya mimi kuwa mwanasheria, kwasabu sikupata nafasi ya kumuuguza, nilikuwa natumaini kuwa Mahakama itaniacha niende nikamzike Mzee Alutte, I was hoping that, inaelekea kuwa hiyo haipo kwenye mahesabu yenu, mnapokuwa mnafikiria adhabu mfikirie na hilo, family obligationdls is a factor kuamua adhabu, huyu mtu amefiwa, Dunia nzima inajua, magazeti everywhere, I was hoping that nitapata nafasi ya kwenda kumzika huyu aliyenilea.
Waheshimiwa majaji leo ni mwaka na miezi 7 niko gerezani, mnapofikiria adhabu kali muitoe msije mkasahau kwamba huyu mtu ameshakaa gerezani kwa kosa ambalo mmelisema wenyewe kuwa sio kosa, halijathibitishwa na wala msije mkasau walichokisema jopo la Majaji watatu wenzenu: Jaji Mruma, Dkt. Longopa na Jaji Rumisha kuhusiana na niliyotendewa gerezani.
Wamesema nimenyimwa fursa ya kuwasiliana na mawakili wangu, Viongozi wenzangu wa chama halali cha Chadema, nimenyimwa fursa hata ya kuomba Mungu. Majaji wenzenu wamesema hayo yaliyotendeka nilinyimwa fursa na haki ya kujitetea, msije mkasau hayo mnapofikiria adhabu kali.
Waheshimiwa Majaji mimi ni raia mwema wa nchi hii, mzalendo wa nchi hii, nimetumikia nchi hii kama Mbunge wa kuchaguliwa na Wananchi mara 2 nimekwenda Jeshini, nimekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria wa nchi hii, mimi sio mpiga kelele, I am a patriotic, ndio maana nimeona na mabalozi wako Mahakamani, wanajua mimi ni patriotic hivyo mnapofikiria adhabu msije mkasahau hoja hii.
Waheshimiwa Majaji gerezani sio mahali pazuri sana, nasema hivyo kwasababu nimeishi kwa siku 577, nakaa kwenye chumba cha sita kwa sita, sio sheraton hotel, unaweza ukasema tu funga kama hujui Gereza ni nini?
Nasema haya kwasababu mimi sio mzima sana, kwenye huu mwili wangu nina operesheni 25, visu vya madaktari, ninatembea na risasi mwilini.
Katika risasi 16 zilizoingia mwilini moja walishindwa kuitoa, ninatakiwa niwe naenda Hospital Ubeligiji, Hospital ya chuo kikuu cha Luven nilikotibiwa baada ya yaliyonikuta miaka 9 iliyopita, nimeshamiss appointment 4 kwasababu ya kesi hii, juu ya yote hayo Majaji nina kisukari huu mwaka wa 6 sasa, kwahiyo mtakapokuwa mnatafakari hiyo adhabu kali, mkumbuke hilo kwamba hali yangu ya kiafya sio nzuri sana.
Waheshimiwa majaji kosa la uchochezi mara ya mwisho nilipoangalia ni kosa lenye dhamana, kama itawapendeza Kwa vile hili kosa lina dhamana, mnipe dhamana ili nikatie uamuzi wenu huu rufaa nikiwa nje kwa dhamana lakini muhimu zaidi pia ili nikamzike huyu aliyelala (Mzee Alute), nilisema sina mpango wa kuomba ila dhamana naomba.
Part 502 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 500
Mhe. Lissu amemaliza kuteta jambo na Mawakili wake, Mawakili wanarudi kwenye nafasi zao.
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nashukuru kwa nafasi, naomba mnisikilize kwa umakini na muandike kwa umakini.
Leo ni siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kuitwa Mhaini, kosa ambalo kwa katiba ya nchi yetu ndio kosa kubwa kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndio kosa pekee lililotamkwa katika katiba, kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, adhabu yake inaweza kuwa kifo baada ya siku 577 za hilo wingu jeusi la adhabu ya kifo kuning’ing’inia juu ya kichwa changu, mmeniita mchochezi kosa ambalo halijapangiwa adhabu.
Mmeniita mchochezi na Wakili wa Serikali Mkuu anahangaika kutafuta adhabu yake ni nini????
Maana yake ni nini waheshimiwa majaji?
Kosa nililoshtakiwa nalo halikuwa kosa na nyie wenyewe mmesema halikuwa kosa, kwahiyo nilikaa siku 577 Gereza la Ukonga bila kosa lolote.
Waheshimiwa majaji kauli yenu kwamba halikuwa kosa mmekubaliana na msimamo wangu na ushahidi wangu.
Kuna kitu kimoja hamjakisema na nitakisema for the record na ushahidi wangu umethibitisha kwamba hii ilikuwa ni kesi ya kisiasa tuu, kugeuza Mahakama ya jinai kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa.
Kwa hukumu yenu ya leo mmethibitisha hilo, ni Political persecution, hivyo inabidi visababu vitengenezwa vya kumfunga huyu mpinzani wao wa kisiasa na visababu vyenyewe ni kosa la uchochezi ambalo nyie Majaji mmelitengeneza, sikushtakiwa kwa uchochezi, nilishtakiwa nje ya uhaini.
Nilishtakiwa kwa kusambaza taarifa za uongo, mmetafuta kosa ambalo halikuwepo, with all due respect mmefanya hivi kwasababu ya maelekezo ya kisiasa, hana kosa ila asiachiwe hivi hivi ataonekana ameshinda, Serikali itaaibika, anayetupa Ujaji ataaibika, ndivyo mlivyofanya leo.
Ninajua mnahukumu, ninajua, I feel it in my heart kwa bahati mbaya sana mmefanya kile ambacho Mahakama kuu ya Kenya ilikifanya mwaka 1954 kwenye kesi ya Jomo Kenyatta.
Mahakama Kuu ya Kenya ilimpata na hatia Mzee Kenyatta ingawa historia ilikuwa inajua kuwa hamna kosa lolote, ndicho ambacho mmefanya leo Waheshimiwa majaji.
Historia haijawa na wema sana kwa Majaji ambao wamegeuza Mahakama zao kuwa mahali pakuadhibia wasiokuwa na hatia ili kuwaridhisha walioko madarakani kwasababu mnaadhibu mtu ambaye mnajua hana hatia na Dunia inajua hana hatia.
Waheshimiwa Majaji Wasiokuwa na hatia kama mimi huwa hawaombi msamaha, unaomba msamaha kama una hatia au kama umekosa.
Huombi msamaha unapokuwa huna hatia, nataka niwe very clear kuwa haya nitakayoyasema yasichukuliwe kuwa naomba msamaha, I am completely innocent lakin kwa vile Wakili mkuu wa Serikali amezungumza naomba nimjibu,
Kwanza kabisa, amesema kwenye kifungu cha 35 ambacho amekiombea adhabu kali amesema adhabu ya juu ni kifungo cha miaka 5 au faini au vyote viwili.
Sheria inapotoa adhabu ya aina hiyo faini au kifungo, Mahakama inatakiwa ifanye nini? katika kesi ya Salum Shaban vs R (1985) TLR 71 ambapo Mahakama hii ilisema pale ambapo Bunge limetoa option ya faini au kifungo, Mahakama lazima itoe kwanza adhabu ya faini kwanza.
Kwahiyo mnapotafakari adhabu kali iliyoombwa na Wakili Mkuu wa Serikali msije mkasahau msimamo huu wa kisheria ikiwemo kesi ya Alice Nyawira Ndungu vs R Criminal Appeal No 40 of 2022, Elias Ndikumana vs R Criminal Appeal No 39 of 2022 na mashauri mengine mengi ambayo nina uhakika mnayafaham.
Kuna maneno yamezungumzwa hapa na Wakili Mkuu wa Serikali, amejigeuza kuwa shahidi, amesema kwamba haya makosa ya uchochezi yamekuwa ni makosa mengi sana kwa mujibu wa taarifa za polisi, na kwa mujibu wa hotuba ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman.
Part 501 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 499
Jaji Ndunguru anasema kwamba Mahakama inaamini kwamba mshtakiwa alikuwa na notice ya kosa dogo hivyo alikuwa na nafasi ya kujitetea na ushahidi wote uliotolewa umejikita kwenye uchochezi na alichochea umma kuzuia uchaguzi wa 2025
Kwa mujibu wa kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu Mahakama imeridhika kwamba Lissu alitenda kosa la uchochezi kwa mujibu wa kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu.
Hivyo Mahakama hii inamtia hatiani kwa kosa hili la Uchochezi.
Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka
Anasimama Katuga anasema Kamba kwa mujibu wa kifungu cha 339 cha CPA mahakama hii inaweza kupokea mpaka ushahidi kwenye kutoa proper sentence.
Upande wa Jamhuri tunajua adhabu ina malengo mojawapo ni kutoa onyo kwa mtu aliyetenda kosa ili asirudie kosa hilo au makosa mengine na linakuwa onyo kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa hilo ambalo mshtakiwa ametiwa hatiani.
Upande wa Jamhuri mbali na kutokuwa na previous records za mshtakiwa za makosa ya nyuma, kwa mujibu wa taarifa zilizopo polisi kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu wenye kutenda kosa la kuchochea umma wa watanzania kwa maslahi yao binafsi either ya kisiasa au ya kiuchumi.
Vitendo ambavyo mara zote vinaharibu amani ya nchi, vinaathiri uchumi wa nchi kwa maana ama vinapelekea uharibifu wa mali za umma zikiwemo na mali binafsi.
Hivi vitendo vya kichochezi vinaathiri uchumi wa nchi na vimepelekea umma wa watanzania kuwa na hofu kuwa kutakuwa na matukio ya uvunjifu wa amani hivyo wanashindwa kufanya shughuli za kiuchumi.
Waheshimiwa vitendo vya kiuchochezi vinaathiri uchumi wa wananchi na hili ni kosa kisheria, wakati mnatoa adhabu tunawaalika katika hotuba halali ya Jaji Chande na Tume yake baada ya kufanya uchunguzi bila kuchagua upande wowote walisema sababu za vurugu wakati na baada ya uchaguzi wa 2025 zilisababishwa na kauli za baadhi ya wanasiasa.
Kifungu cha 35 kinatoa general punishment ambayo adhabu yake ni miaka 5 hivyo tunaomba mahakama hii iangalie athari ambazo zimetokea kutokana na kauli ambazo mshtakiwa ametiwa hatiani pamoja na hotuba ya jaji chande.
Taarifa ya Chande inaonyesha hasara inayotokana na uchochezi uliotokana na kauli hizo.
Tunaomba adhabu kali Waheshimiwa majaji ili iweze kukidhi nia ya adhabu kisheria.
Waheshimiwa kifungu hiki kinasema adhabu kubwa ni miaka 5 au pamoja na faini.
Ni faini kiasi gani ni Mahakama kuangalia athari kutokana na athari zilizotokea. Ni hayo tu.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kama analolote la kusema?
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nina maneno ya kuzungumza ila naomba dakika 5 nifanye consultations na mawakili wangu ili niweze kuzungumza hayo ninayotaka kuzungumza.
Jaji Ndunguru:Sawa
Part 500 itaendea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost.
‼️POLICE ARE TAKING AWAY PEOPLE’S PHONE ON THE STREETS‼️
I have a lot of messages of police raking away phones from people on the streets! This means they are preparing to commit atrocities
They have also restricted social media like they did last year during the atrocities @OHCHR_ESARO@AmnestyEARO@hrw@StateDeptARS@FCDOGovUK@Europarl_EN@commonwealthsec - you blinked @SGCommonwealth