#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 315
Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika.
Katuga: Mwenyekiti Lissu ana utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mnyika: Sijui
Katuga: Yeye ni raia wa Tanzania.
Mnyika: Ndio
Katuga: Ulikuwa unaufuatilia Mkutano?
Mnyika: Upi?
Katuga: Huo wa tarehe 03
Mnyika: Sehemu kubwa niliufuatilia.
Katuga: Je watia nia wote walifika?
Mnyika: Sio wote ila siwezi kujua idadi ya waliofika.
Katuga: Madhumuni ya kuwaita watia nia ni yapi?
Mnyika: Kuwaeleza watia nia kama viongozi na wanachama kuwaonesha kwanini chama kilifikia msimamo wa No Reforms: No Election.
Katuga: Waliandika waraka wa kutaka kugombea?
Mnyika: Hapana, huo una maelezo yake.
Katuga: Aliyemualika Mwenyekiti wa Chama ni nani?
Mnyika: Alimpigia Amani Golugwa kumualika Mwenyekiti.
Katuga: Akimualika Mwenyekiti?
Mnyika: Alimualika Mwenyekiti na viongozi wengine.
Katuga: Ulisema tulimuandikia risala ya kuja kuzungumza?
Mnyika: Hilo sijasema.
Katuga: Je nyinyi sekretarieti ndio mliyemuandikia cha kwenda kuzungumza.
Mnyika: Msimamo huo ulishakuwepo zamani.
Katuga: Hamjamuandikia risala?
Mnyika: Mwenyekiti hatoi risala, Mwenyekiti anatoa hotuba inayoendana na maamuzi ya Chama.
Katuga: Kwahiyo unamsemea?
Mnyika: Namsemea kwasababu alichokisema ni msimamo wa Chama na alichokuwa anakisema pale ilikuwa ni kwa niaba ya Chama.
Katuga: Kwenye hiyo Hotuba ile sehemu ya kwamba majaji ni maccm uliisikia?
Mnyika: Sikusikia.
Katuga: Mapolisi wanaingia na vibegi vya kura?
Mnyika: Nilisikia
Katuga: Tutaenda kuzuia uchaguzi
Mnyika: Nilisikia
Katuga: Tutahamasisha uasi?
Mnyika: Nilisikia, hotuba nzima na alifafanua.
Katuga: Kama hiyo hotuba umeileta hapa Mahakamani?
Mnyika: Nimeileta kwa maelezo yangu ya mdomo.
Katuga: Katiba yetu ya Chadema inatambua Demokrasia ya Vyama vingi si ndio?
Mnyika: Ndio
Katuga: Uchaguzi Mkuu upo kisheria.
Mnyika: Uchaguzi mkuu halali.
Katuga: Uko timamu shahidi?
Mnyika: Wewe uko timamu?
Katuga: Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Rais upo kisheria?
Mnyika: Uchaguzi halali na wa haki upo kisheria.
Katuga: Uchaguzi wa wabunge madiwani na Rais upo kisheria?
Mnyika: Haupo muda wote. Bali unaitwa kwa mujibu wa sheria.
Katuga: Unajua Uchaguzi Mkuu uko Kikatiba?
Mnyika: Haupo bali umewekwa kwa mujibu wa Katiba.
Katibu Mkuu wetu Mnyika anagonga kwenye ugoko tu mpaka Mzee wa Multiple choice anavuja jasho wakati feni iko on.๐๐๐
Jaji Ndunguru kwahiyo umeuliza nini?
Mhe. Lissu: Swali limeulizwa na limejibiwa.
Katuga: Uchaguzi mkuu unaexist kwa mujibu wa Katiba?
Mnyika: Umewekwa kwa mujibu wa Katiba.
Katuga: Nitakuwa sahihi nikasema kwakuwa uchaguzi huo upo kikatiba Una haki ya kuamini kuchaguliwa na kushiriki uchaguzi huo?
Mnyika: Ukiwa huru haki na halali.
Katuga: Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema mtu yeyote ana haki ya kushiriki kwa Chama chochote mbali na Chadema kushiriki uchaguzi wa haki na halali.
Mnyika: Kwenye uchaguzi wa haki na halali ana haki ya kushiriki.
KAZINI KWA KATUGA LEO KUNA KAZI. ANACHEKACHEKA TU.
Katuga: Kwahiyo haki anayo au hana?
Mnyika: Ukiitishwa uchaguzi huru na haki.
Katuga: Demokrasia ya Vyama vingi ni haki kwa mwanachama wa Chadema kuuzuia uchaguzi uliopo Kikatiba?
Mnyika: Katiba ya Chadema inatoa wajibu kwa wanachama kupambana na ukandamizaji wa kila aina ikiwemo uonevu. Kwahiyo ni Haki kwa Mwanachadema kupinga uchaguzi wa hovyo.
Katuga: Muasisi alikuwa Mbowe ulisema wa No Reforms: No Election?
Mnyika: Muasisi sio mtu ni kikao.
Katuga: No Reforms: No Election ulitafsiri vipi?
Mnyika: Bila Mabadiliko hakuna Uchaguzi.
Katuga: Kwenye hayo maneno kuna neno kwamba tutahamasisha uasi?
Mnyika: Hakuna hayo maneno ila huo uasi ni maana ya huo msimamo wetu.
Katuga: Ila ya nini tena?
Mnyika: Usikasirike sasa, mimi akupa maudhui
Mnyika leo kaamua kumpandisha Katuga kisukari mpaka amekasirika ๐๐๐๐๐
Part 316 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 314
Katuga anaendelea kumfanyia John Mnyika cross examination
Katuga: Ni kweli vyama hivyo vinaweza kuwa na Wanachama wake?
Mnyika: Siwezi kuwa na uhakika na wanachama wa vyama hivyo sina uhakika kama kweli vina wanachama.
Katuga: Hivyo vyama vingine pia vina itikadi yake?
Mnyika: Siwezi kuvisemea angalau ungeniuliza kuhusu Chadema, labda CCM na ACT ningweza kusema lolote.
Katuga: Mwanachama wa Chadema anapaswa kuheshimu Katiba?
Mnyika: Sahihi.
Katuga: Asiyefuata ni yule anayevunja Katiba ya Chadema?
Mnyika: Ni sahihi.
NB. KATUGA anamuuliza Mnyika kuwa ni form six. ๐ kila saa anaiulizia. Haoni hata aibu amekutana na shahidi form six lakini ana akili nyingi kuliko yeye na anamtesa vya kutosha.
Katuga: Si sawa kwa Mwanachadema yeyote kutokuamini anachokiamini mwanachama mwingine kwa itikadi yake?
Mnyika: Sasa sisi hatujasema tu habari ya vyama vingi kwa maana ya idadi.
Katuga: Kwahiyo mtu kupinga maoni ya vyama vingine ni kuvunja Katiba ya Chadema inayoamini vyama vingi?
Mnyika: Sio kweli maana upo uhuru wa maoni hata kupinga ni haki.
Katuga: Tarehe 03/04/2025 ulikuwepo kwenye Mkutano na nani alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo?
Mnyika: Hakukuwa na Mwenyekiti wa Mkutano.
Katuga: Kwahiyo mkutano wa Chadema hakukuwa na mwenyekiti wa Mkutano.
Mnyika: Sahihi Kabisa, hatunaga mwenyekiti wa Mkutano.
Katuga: Uliwaambia mikutano ipo ya aina gani?
Mnyika: Aina kuu ni mbili yaani Mkutano wa Hadhara na Mikutano ya ndani.
Katuga: Mikutano ya ndani na hadhara kwa mujibu wa Katiba ikoje?
Mnyika: Hakuna aina za mikutano kwenye Katiba ni taratibu za kiutendaji tu.
Katuga: Kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa Chama alikuwa na cheo gani?
Mnyika: Alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama.
Katuga: Huo Mkutano ulikuwa na maudhui gani? Na ulisema ulikuwa wa nani?
Mnyika: Ni Mkutano wa Chama na Mwenyekiti alikuwa Mzungumzaji Mkuu.
Katuga: Hiki Chama chetu kinapoitwa watia nia na Chama wanaenda kuongea na nani?
Mnyika: Watia nia wanaenda kuongea na Chama.
Katuga:Kwahiyo hawaendi kuongea na Mwenyekiti, Katibu, Naibu
Mnyika: Unaongea na Chama kupitia viongozi wakuu wa Chama.
Katuga: Uliwahi kuita waandishi wa habari na kusema mashahidi wa Jamhuri kuwa ni waongo?
Mnyika: Lissu sio muhaini nimewahi kusema mambo ya kuzungumzia kesi sijawahi.
Katuga: Unaposema Mwenyekiti wetu hana hatia na sio muhaini. Haya maoni yako unayatoa kwa mujibu wa ushahidi wa jamhuri au maoni yako?
Mnyika: Kwa mujibu ninavyomjua Mwenyekiti.
Katuga: Wewe ni mratibu wa vikao vyote vya Chama?
Mnyika: Sio kweli.
Katuga: Vikao vya Kamati Kuu unaratibu wewe?
Mnyika: Ndio ni mimi.
Katuga: Hiki cha juzi cha Tarehe. 29/08 ulikiita wewe?
Mnyika: Ndio ni mimi
Katuga: Mwenyekiti wa Kikao anakuwa ni nani?
Mnyika: Mwenyekiti wa Chama kama hayupo anakuwa makamu Mwenyekiti.
Katuga: Kile mlichojadili mlikitolea taarifa kwa umma.
Mnyika: Nafahamu ilitolewa kwa umma taarifa.
Katuga: Mlijadili hii kesi kwenye kikao?
Mnyika: Tulipokea taarifa ya kuwa Mwenyekiti amekutwa na hatia.
Katuga: Bado unasema kuwa Katibu Mkuu ndio mtendaji mkuu?
Mnyika: Ni sahihi.
Katuga: Ni sahihi wanaweza wakatenda au wakafanya utendaji bila Katibu Mkuu kujua?
Mnyika: Wanaweza katika maswala yakawaida ya kiutendaji.
Katuga: Umesema Mwenyekiti alipendekeza na kuthibitishwa na Kamati kuu?
Mnyika: Sio Kamati Kuu bali ni Baraza Kuu.
Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema wewe ni shahidi mwenye interest?
Mnyika: Nina Party interest na Public interest.
Katuga: Kwa hicho ulichokisema na umesema amekuteua. Nitakuwa sahihi nikisema wewe una maslahi?
Mnyika: Maslahi unayosema wewe sio maslahi niliyonayo mimi. Ukitaka kujua maslahi yangu mitakwambia.
Katuga: Ulisomewa yale mashitaka. Unajua aina ya uhaini alioshitakiwa nao mwenyekiti?
Mnyika: Uhaini wa kuitisha serikali kwa kuchapisha maneno.
Part 315 Itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 313
Katibu Mkuu wa Chadema anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mahakama imerejea muda huu saa tisa kasoro alasiri.
Majaji wameingia tayari na Ajuaye Zengeli anasema wako tayari.
Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika anapanda kizimbani.
Anasimama KATUGA anasema atakuwa na maswali machache labda kama wenzangu pia watakuwa nayo
Katuga: Nitakuwa na maswali machache na nafahamu wewe ni mkristu mwema. Kwa Cheo chako cha Katibu Mkuu ni mtendaji mkuu wa CHADEMA?
Mnyika: Ndio
Katuga: Chadema inaongozwa kwa sheria
Mnyika: Katiba, kanuni, Miongozo na Maamuzi ya Vikao.
Katuga: Katiba ni instruement muhimu na unaijua sana?
Mnyika: Naijua kwa kiasi cha Kutosha.
Katuga: Katiba yenu ni document inayopatikana iko public?
Mnyika: Sahihi.
Katuga: Katibu Mkuu anapatikanaje?
Mnyika: Anapendekezwa na Mwenyekiti wa Chama na anathibitishwa na Baraza Kuu.
Katuga: Mbona unatuchanganya?
Mnyika: Ndio nimekwambia anapendekezwa na Mwenyekiti na kuthibitishwa na Baraza Kuu sio kwamba nateuliwa na Mwenyekiti.
Katuga: Ibara ya 3(5) ya Katiba ya Chama inasema Chadema inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu?
Mnyika: Itabidi nirefresh sasa siwezi kujibu hivyo, nipewe nafasi.
Jaji Ndunguru: Haya angalia.
Mnyika: Ni sahihi Chadema inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi.
Katuga: Dhumuni Kuu ibara ya 4 ya Katiba ya Chama inasemaje?
Mnyika: Kuhakikisha Chama chetu kinashinda Chaguzi na kushika dola kwa njia ya Demokrasia.
Katuga: Kwa jinsi lilivyowekwa ndio kubwa kuliko yote?
Mnyika: Katiba ina madhumuni ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kushika dola sio dhumuni kuu na pekee.
Katuga: Kiwango chako cha Elimu ni kipi?
Mnyika: Ni kidato cha Sita.
Katuga: Huna uelewa wa Sheria?
Mnyika: Kwa vile sijapita law school unaweza kuniita layman.
Katuga: kwahiyo maoni yako ya kisheria unayabagaza tu?
Mnyika: Nina uzoefu wa miaka 23 wa siasa na utendaji na pia nimetunga sheria kwa miaka 10.
Mhe. Lissu: Haya mambo ya kumuuliza kuhusu maoni yake ya kisheria hakuna aliposema hivyo shahidi.
Majaji wanateta pale.
Jaji Ndunguru: Tuendelee.
Katuga: Ulisema wewe ni afisa masurufi?
Mnyika: Masuhuli
Katuga: Wewe ndio custodian wa fedha zote za Chama.
Mnyika: Hapana.
Katuga: Kwani majukumu yako ni nini?
Mnyika: Kuidhinisha matumizi ya pesa na kupokea taarifa za fedha kadri zinavyoandaliwa na wahusika.
Katuga: Unahusika na pesa zetu za tonetone? Na unahusika na kuzipokea?
Mnyika: Mimi ni accounting officer na sipokei pesa.
Katuga: Kama Mdau ameipatia Makamu wa Rais pesa unazipokea wewe?
Mnyika: Chadema haina Makamu wa Rais.
Katuga: Nimekosea hapo.
Hivi wewe ndio unayelipa mishahara?
Mnyika: Mimi sio mlipaji wapo wanaolipa.
Katuga: Kwahiyo usipoidhinisha wewe wanalipwa?
Mnyika: Kwanza Chadema hatuna mishahara tuna posho tu.
Katuga: Usipoidhinisha wanapata:
Mnyika: Inategemea kama hizo pesa zipo. Zisipokuwepo hawawezi kupata chochote.
Katuga: Soma ibara ya nne pia
Mnyika: Kuthamini Demokrasia
Katuga: Kuna vyama havina mrengo wenu?
Mnyika: Sahihi
Katuga: Kuna vyama vingine haviamini katika No Reforms,No Election.
Mnyika: Siwezi kuvisemea.
Katuga: Vyama vingine vya siasa vina wanachama wake?
Mnyika: vyama vipi hivyo?
Katuga: Katiba ya Chama si inasema mnathamini uwepo wa vyama vya siasa. Kwenye hivyo vyama vingi kuna vyama ambavyo vina wanachama wake?
Mnyika: Siwezi kuvisemea vyama vingine ambavyo ni vya mfukoni tu, siwezi kuvijua kama kweli vina wanachama.
Katuga: Vyama vyenye usajili ni vingapi?
Mnyika: 19
Katuga: Vyama 18 vina wanachama wao na itikadi zao?
Mnyika: Siwezi kuvisemea.
Katuga: Ni kweli Chama cha siasa ili kisajiliwe lazima kiwe na wanachama?
Mnyika: Unaweza kuwa na Chama kikishasajiliwa wakahama au kuondoka. Lakini pia kwa mazingira ya sasa msajili anaweza kuvilinda vyama hewa hata kama havina wanachama. Inawezekana.
Part 314 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 312
Katibu Mkuu wa Chadema anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mnyika : Matendo aliyotuhumiwa nayo hayajawahi kutokea na DPP alipeleka hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo na kesi ilifutwa na Mwenyekiti Mbowe alikutana na Rais Ikulu. Toka kuwa mtuhumiwa wa UGAIDI hadi MAPOKEZI IKULU.
Watu wanacheka.๐๐๐๐๐
Na Lissu anasema kwa kejeli kwamba na Mimi itakuwa hivyo hivyo?๐๐๐
Mhe. Lissu: Hayo makesi yote na hii yangu vina uhusiano gani?
Mnyika: Hizi kesi zote ni mwendelezo wa kupambana na Chadema kwa kutumia Mahakama kukwamisha mapambano ya kudai demokrasia ya kweli na mabadiliko katika mifumo ya Uchaguzi. Haya ni matumizi yasiyo ya haki dhidi ya wapinzani ambao ni CHADEMA kutoka kwa Chama dola ambao ni CCM. Lengo lao ni kukwamisha mabadiliko tunayohitaji. Hivyo huu ni mwendelezo wa mambo mabaya ambayo yamekuwa yakifanywa na hawa serikali dhalimu.
Anataka kusimama Ajuaye.
Mhe. Lissu: Subiri namaliza muda sio mrefu. Umenifahamu lini?
Mnyika: Toka 2003 tukiwa wote kwenye sekretarieti, baadae Kamati Kuu na Baadae Bungeni miaka 23 nakufahamu.
Mhe. Lissu: Huyu mtu ni mtu wa aina gani ambae umemfahamu kwa miaka 23?
Mnyika: Toka mwaka 2003 tulipoenda kule Kwembe, nimekufahamu kama mtaka mabadiliko, ni mtu mkweli ambae siku zote umekuwa ni mtu unayetaka mabadiliko. Mimi naamini MASHITAKA HAYA NI GHARAMA UNAYOLIPA KWA KUWA MKWELI NA KUTAKA MABADILIKO NDANI YA TAIFA HILI.
Mhe. Lissu: Mheshimiwa Jaji nimemaliza kwa shahidi huyu.
Maneno aliyomalizia JOHN JOHN MNYIKA yamewafanya akina Mama waliopo humu MAHAKAMANI WATOE MACHOZI.
Yamekuwa ni maneno mazito sana na yenye ujumbe mzito, watu wamesikitika sana.๐ฅน
Majaji wanaandika na kwa muda tulionao. Tutakwenda break na kurudi kwenye Cross Examination ya upande wa Jamhuri.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 311
Katibu Mkuu wa Chadema anaendelea kutoa ushahidi wake.
Sasa hii rozali aliyovaa Mnyika huwa inajulikana kama Franciscan Crown Rosary, kwa Kiswahili unaweza kusema Rozari ya Taji ya Kifranzisko (Seraphic Crown).
Tofauti kubwa ni kwamba ina mafumbo saba badala ya mafumbo matano ya Rozari Takatifu ya kawaida.
Mafumbo hayo saba yanahusu furaha saba za Bikira Maria, hasa matukio ya furaha katika maisha yake pamoja na utukufu alioupokea kutoka kwa Mungu.
Kwa kawaida inakuwa na miongo saba (decades), yaani jumla ya Salamu Maria 70, badala ya Salamu Maria 50 za rozari ya kawaida.
Rozali hii ina uhusiano mkubwa na Mtakatifu Fransisko wa Asizi na mapokeo ya Kifranzisko ya kumheshimu sana Bikira Maria.
Jina "Seraphic Crown" linahusishwa na mapokeo ya Wafransisko kama Order of the Seraphic Wafransisko wanahusisha sana utambulisho wao na malaika maserafi na moto wa upendo wa Mungu.
Kuna pia mapokeo maarufu kuhusu Mt. Bernardine wa Siena, ambaye alihusishwa na ibada hii, ingawa historia ya asili yake ina maelezo na mapokeo mbalimbali.
Unaambiwa Lengo lake ni kumheshimu Maria kwa kutafakari furaha saba za maisha yake, na kupitia hizo kumtafakari Kristo.
Kuna pia rozari nyingine zinazohusishwa na Wafransisko, kama Tau Cross rosaries (zenye msalaba wa Tau), na hii ndiyo aina aliyoivaa JOHN JOHN MNYIMA.
Msalaba wa Tau (ฮค) ni alama maarufu sana ya Kifranzisko na unahusishwa na Mt. Fransisko wa Asizi.
Rozali hii yenye herufi โTโ, mara nyingi alama hiyo inahusishwa na Wafransisko (Franciscans) na Tau Cross (Msalaba wa Tau).
โTโ ni Msalaba wa Tau (โ /T), ambao ni alama ya kale ya Kikristo.
Mtakatifu Francis wa Assisi aliupenda sana msalaba huo na kuutumia kama ishara ya toba, wokovu na kujitoa kwa Kristo.
Kwa hiyo, Wafransisko wameutumia kwa muda mrefu kama alama ya utambulisho wa shirika lao.
Kwenye rozali, alama hiyo inaweza kuonyesha uhusiano wake na ibada na mapokeo ya Kifransisko, hasa ibada kwa Yesu Kristo na Bikira Maria.
Je kama unajua zaidi kuhusu Rozali hii tafadhali waseminari mtusaidie maarifa.
Tunaendelea sasa..
Mhe. Lissu: Ukiacha ya Mbeya unakumbuka nini kingine kuhusu madhira mengine?
Mnyika: Tarehe 06/02/2018 aliuwawa Mwanafunzi wa Chuo Akwilina Akwilimi kwa risasi katika tukio hilo ambalo Polisi walishambuliwa risasi tulibambikizwa kesi mimi na viongozi wengine 8 wa Chadema kwamba tumefanya ghasia na kusababisha kifo cha mwanafunzi huyo.
Tarehe 10/03/2020 baada ya ushahidi wa uongo Mahakamani tukahukumiwa kifungo jela au faini ya milioni 300+ tulienda kuanza kutumikia kifungo na baadae watanzania wakatuchangia faini na kutoka.
Tulikata rufaa baada ya kuwa tumelipa ile faini na mwezi June 2021 Mahakama Kuu chini ya Jaji Mgeta ikatukuta kuwa hatuna hatia, ikatufutia hukumu hiyo kati ya mambo ambayo Jaji alisema juu ya mamlaka ya kuheshimu uhuru wa kisiasa na ukosoaji wa kisiasa hata kama utafanyika kwa kauli kali.
Na mpaka leo HATUJAWAHI KURUDISHIWA PESA ZETU MILIONI 300+ leo miaka zaidi ya minne.
Watu wanacheka ๐๐๐
Mhe. Lissu: Wenzako mlioshitakiwa nao ni akina nani?
Mnyika: Mwenyekiti wa Chama wakati huo Mbowe, Katibu Mkuu Mashinji, Salum Mwalimu, Halima Mdee alikuwa Mwenyekiti wa BAWACHA, Esther Matiko na aliyekuwa Mwenyekiti Kanda ya Nyasa Peter Msigwa na Mjumbe wa Kamati Kuu John Heche.
Mhe. Lissu: Kesi zingine unazofahamu za kubambikiza za viongozi wa Chama?
Mnyika: Mwenyekiti wetu aliyepita Freeman Mbowe na Dr. Wilbroad Slaa walishtakiwa kwa kusababisha fujo ambazo zilisababisha kupigwa mabomu na vifo mwaka 2011 na 2012.
Mhe. Lissu: Hizo kesi ziliishaje?
Mnyika: Hawakuwahi kuhukumiwa na kesi zilikuja kufutwa baadae.
Mhe. Lissu: Kesi zingine?
Mnyika: Mwaka 2021 Mwenyekiti Freeman Mbowe nae pia alishitakiwa kwa kosa la Ugaidi kwamba alipanga kulipua vituo vya mafuta na matendo mengine ya kutishia serikali na usalama wa nchi.
Part 312 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
โผ๏ธPOLISI MWITA MILUMBE ATESWA NA KUUWAWA , NDUGU WAONBA MSAADA.โผ๏ธ
Habari ya kazi kaka Mwaipaya. Mimi, kama mmoja wa wanafamilia, tunaomba msaada wa kutupazia sauti kuhusu Jeshi la Polisi Tanzania.
Mkoani Tanga kuna unyama wamefanyiwa mdogo wangu kwa kutokukubali kuwa upande wa mauaji na utekaji wao. Amekuwa akipinga mpaka akahamishwa kituo cha kazi kutoka Dar es Salaam, Ukonga, kwenda Tanga.
Jeshi la Polisi lilimshikilia ndugu yangu, Mwita Mecky Milumbe, mwenye force namba H.1796, kuanzia tarehe 21 mpaka tarehe 28, tulipopata simu kutoka kwa watu wa karibu naye wa kituo cha Tanga kuwa amefariki kwa kujinyonga.
Lakini hajajinyonga. Wamempeleka msituni, wamemtesa sana wakiwa wamemfunga pingu, ikiwa ni pamoja na kumkata visigino, kumkata pua, kungโoa kucha, kumtoboa macho na kumuingizia chupa sehemu za haja. Kisha wakamrudisha mahabusu na kumtundika kwa T-shirt yake.
Mtu aliyetuandalia taarifa alituambia tusimtaje kwa kuwa tutamuharibia kwa viongozi wake.
Naomba msaada wako kutupazia hili. Yote haya ni kwa sababu ya kupinga utekaji ambao walikuwa wanatakiwa kuufanya yeye kama mmoja wa Special Field Force Unit.
Mpaka sasa wametukabidhi mwili, lakini wamezuia simu zake na wamekatalia kushiriki kwa chochote katika mazishi.
Msiba upo Kitunda Mwanagati, njia panda ya kwenda Kibeberu. Ukiwa hapo panapoitwa Nyangasa, kama unaenda Mwanagati, ukiuliza kwa Mama Mwita utaelekezwa. Mama yake ni maarufu kwa kufuga nguruwe.
Polisi walileta tu mwili na wakaondoka jana jioni Tarehe 30.8.2026 saa 10, na hakubaki hata mmoja.
๐จโผ๏ธWITNESS MURDERED โผ๏ธ #Tanzania
Mwita Mecky Milumbe, policeman with the Tanzania Field Force unit, force number H.1796 was brutally murdered by fellow police after he refused to take part in abductions and killings of critics and opposition members.
The Police detained him 21st to the 28th August. Family couldnโt locate him until the 28th when they received a call from people close to him at Tanga police station that he had died by suicide by hanging himself.
But marks on his body show otherwise - he did not hang himself. They took him to the forest, tortured him severely while handcuffed, including cutting off his heels, cutting off his nose, pulling out his nails, piercing his eyes and inserting a bottle into his private parts. Then they returned him to custody and hung him by his T-shirt
The police took the body and left on 30th August (yesterday) ad left. They have blocked his phones and have refused to participate in any way in the funeral.
Samia Suluhu and her cabal are now killing potential witnesses that is why #SamiaMustGo
(Information relayed via @Twaha_Mwaipaya )
Cc @IntlCrimCourt@AmnestyEARO@hrw@UN_HRC@WorldBankAfrica@IMFAfrica@US_SrAdvisorAF@StateDeptARS@SFRCdems@SenateForeign@SenTedCruz@SenatorShaheen
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 310
Katibu Mkuu wa Chadema anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Kitu gani kilitokea baada ya mimi kukamatwa na kushitakiwa kwa uhaini?
Mnyika: Siku ile ile Tar. 09/04 zilisainiwa nyaraka za kukishitaki Chama na kutaka kizuiwe kufanya kazi zake na kesho yake Tar. 10/04 mahakama ilitoa zuio hilo la kukizuia chama kufanya shughuli zake na matumizi ya mali za Chama.
Pia Msajili wa Vyama vya siasa alikuwa ametuandikia Barua ya kujieleza juu ya uhalali wa Katibu Mkuu wa Chama na Wajumbe wa Kamati Kuu ambao walikuwa wamethibitishwa kwenye Baraza Kuu na baada ya majibishano ya Barua. Aliandika barua na kusambaza kwa umma ya kutotambua uteuzi wa Katibu Mkuu, manaibu wake na sekretarieti ya Chama.
Huyu Msajili pia alituandikia barua ya kuzuia Ruzuku ya Chama na kipindi hicho hicho Tar. 12/04/2025 Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alisema CHADEMA haitaruhusiwa kushiriki uchaguzi kwasababu hajasaini fomu za maadili ya Uchaguzi.
Mhe. Lissu: Nini kiliendelea?
Mnyika: Msajili alituandikia barua ya kutaka maelezo kuhusu kauli za Mwenyekiti hizo za Tarehe 03/04 na aliandika Sisty Nyahoza kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya siasa.
Mhe. Lissu: Barua ya Sisty ilisemaje kuhusu uhaini wa maneno ya Mwenyekiti Lissu?
Mnyika: Hakukuwa na chochote kwenye barua ya Sisty kuhusu maneno ya Mwenyekiti kuwa ni ya kihaini?
Mhe. Lissu: Ulichukua hatua gani baada ya hapo?
Mnyika: Tuliwaandikia majibu kuwa jambo hilo tayari linashughulikiwa na mamlaka nyingine kwahiyo tusubiri matokeo ya mamlaka zingine.
Mhe. Lissu: Umesema ni mashitaka ya uongo waeleze Majaji kwanini?
Mnyika: Umetuhumiwa kwa uhaini kusema maneno ya kawaida ya kisiasa, wanasema uliitisha mkutano wakati hukuitisha wewe niliitisha mimi na sekretarieti, unatuhumiwa kuchapisha maneno hayo wakati maneno hayo hukuchapisha wewe walichapisha waandishi wa habari. Unatuhumiwa kwa kuwa na nia ya kutenda kosa hilo wakati ulichokifanya ni kutekeleza maazimio ya vikao halali vya Chama na kwanini utuhumiwe peke yako na sio na viongozi wengine. Unatuhumiwa kuhamasisha watanzania kutumia mamlaka yao kudai uchaguzi huru, haki na halali dhidi ya wanaoasi na kuhaini mamlaka ya wananchi ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Baada ya hili jibu watu wote wametabasamu. ๐๐
Na mimi nimeanza kutafakari Rozali aliyovaa John Mnyika, nitakuletea uchambuzi wake muda sio mrefu kutoka kwa mseminari niliyenae hapa.
Mhe. Lissu: Unafahamu vitendo ambavyo nimewahi kufanyiwa kihistoria?
Mnyika: Nafahamu umefunguliwa makesi mengi toka utawala wa Rais Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia.
Na nakumbuka Tar. 11/08/2024 tulipigwa na kufanyiwa matendo mabaya na jeshi la Polii, sina neno zuri la kuelezea lakini tukiwa ofisi za Chadema Mbeya walituvamia na kutupiga na kuturudisha Dar es salaam, waliongozwa na kamanda wa oparesheni Awadhi na RPC.
Walinisafirisha hadi Njombe na baadae hadi Dar es salaam na waliponifikisha Dar es salaam nikiwa nimejeruhiwa waliniambia nijidhamini na wakaninipeleka hadi nyumbani na kwakuwa nilikuwa nimeumia nikaenda hospitali kwa ajili ya matibabu.
Mhe. Lissu: Nini kiliendelea kwangu mimi na Sugu ambae unasema pia ilikuwaje?
Mnyika: Na nyie mlisafirishwa hadi Dar es salaam.
Sasa nimemaliza kuelezewa maana ya rozali aliyovaa Katibu Mkuu wa Chadema.
Pata huu uzi wakati Majaji wanajadiliana jambo kidogo.
Pale Kizimbani JOHN JOHN MNYIKA. Shahidi Na. 02 wa Utetezi anaonekana amevaa kitu kama Rozali hivi ina msalaba lakini sio Rozali ya kawaida. Nimemuuliza mchambuzi mmoja hapa anasema:
Rozali ile ni rozali za shirika la wafransisko wanazovaa wakatoliki (Franciscans)
Unaambiwa Kuna aina maalumu zinazohusishwa na utamaduni wao wa Kifransisko, ingawa si kwamba kila rozari ya Kifransisko ni tofauti kabisa na Rozari Takatifu ya kawaida.
Part 311 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 309
Katibu Mkuu wa Chadema anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Kuhusu Jumuiya ya Kimataifa je?
Mnyika: alitembelea balozi mbalimbali ikiwemo ubalozi wa Marekani. Sina orodha yote hapa.
Mhe. Lissu: Ikawaje?
Mnyika: Baadae tuliitwa ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa hapa Dar es salaam. Tulipofika tukamueleza maana ya No Reforms, No Election na tukamueleza kama oparesheni yetu hiyo inaendana na sheria za vyama vya siasa. Maana alituhoji kutaka kujua maana ya No Reforms: No Election.
Msajili wa Vyama vya siasa akasema haoni shida yoyote ya kisheria na baadaye akaja kutoa kauli kwa umma mbele ya vyombo vya habari Tarehe 10/02/2025 kuwa No Reforms: No Election ni kauli mbiu ya kisiasa haikiuki sheria yoyote.
Mhe. Lissu: Hiyo Tarehe 17/03/2025 nje ya Delegation yako nani mwingine alihudhuria?
Mnyika: Namkumbuka Sisty Nyahoza?
Mh. Lissu: Shost Nyahoza?
Mnyika: Anarudia mara nne nne.. Sisty Nyahoza, Sisty Nyahoza.
Mhe. Lissu: Nilisikia vibaya kama umesema Shost Nyahoza. Basi sawa, waeleze Majaji utekelezaji wa maazimio kwa upande wa umma ilikuwaje?
Mnyika: Tulipanga Mikutano ya Hadhara kanda ya Nyasa yenye mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa na mkutano mkubwa wa ufunguzi ulifanyika Mbeya Tar. 23/03/2025.
Mhe: Lissu: Hiyo Ziara ilikuwa hadi lini?
Mnyika: Iliendelea kuanzia hiyo Tar. 23/03 hadi Tarehe 02/04 tulipopanga kikao na watia nia wa uchaguzi wa Chama.
Mhe. Lissu: Nini kiliendelea baada ya Mkutano wa watia nia?
Mnyika: Tulipanga ifanyike Mtwara, Lindi na Ruvuma. Misafara ya maandalizi ikaanza. Makamu Mwenyekiti wa Chama John Heche alikuwa mmoja wapo hadi Tar. 09/04 kule Mbinga, Ruvuma.
Mhe. Lissu: Sasa ule mkutano na watia nia ulikuwa na utofauti gani na mikutano mingine ya hadhara?
Mnyika: Msimamo wa Chama wa No Reforms: No Election na hoja zetu zilikuwa ni zilezile. Isipokuwa kabla ya Mkutano wa Tar. 03/04/2025 nilikuwa nimepokea waraka wa baadhi ya watia nia waliokuwa na mapendekezo ya kutaka chama kibadili msimamo wake. Kwahiyo katika mkutano wa Tar. 03/04/2025 hoja hizo hizo zilizosemwa kwenye mikutano ya hadhara zilitumika kutoa majibu na kukumbusha juu ya msingi wa msimamo wa Chama wa No Reforms: No Election.
Mhe. Lissu: Nafikiri nikurudishe tena kwenye hayo maneno wanayosema ni uhaini wewe unaelewa nini?
Mnyika: Hayo ni maneno ya kisiasa yanayotumika kuhamaisha umma ili ukatae kwa maana ya kuasi, umma uone uchaguzi una uozo mkubwa, unanuka na umma uwezo kukataaa. Uchaguzi uweze kuharibika, na umma uchukue hatua za kuzuia uchaguzi usio wa halali.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji baada ya huo mkutano wa Tar. 03/04 ulilijulisha jeshi la Polisi kuhusu maneno hayo?
Mnyika: Sijawahi kuwaambia chochote.
Mhe. Lissu: Je ulitoa maelekezo yoyote kuhusu tuhuma hizi kwa maafisa wa Chama?
Mnyika: Sikutoa kabisa.
Mhe. Lissu: Je jeshi la Polisi limewahi kukuhoji chochote kuhusu maneno hayo?
Mnyika: Sijawahi kuhojiwa lolote na jeshi la Polisi.
Mhe. Lissu: Je una ufahamu wowote wa hatua alizochukuliwa yeyote kati ya wale waliokuwepo pale makao makuu?
Mnyika: Hakuna mtia nia yeyote aliyekamatwa wala kuhojiwa na Polisi.
Mhe. Lissu: Je ufahamu wako kuhusu hatua alizochukuliwa mwandishi wa habari yeyote?
Mnyika: Sina taarifa za kwamba kuna mwandishi yeyote alichukuliwa hatua kwa jambo hilo kwa hiyo naweza kusema hakuna mwandishi aliyekamatwa wala kuhojiwa kuhusu kutenda makosa ya kusambaza na kuchapisha picha taarifa za mkutano huo.
Mhe. Lissu: Unasema ulipanga huo mkutano, ulitoa pesa na kusimamia maandalizi yote. Walichukua hatua gani polisi dhidi yako?
Mnyika: Hakuna hatua yoyote dhidi yangu au mtu mwingine yeyote ndani ya sekretarieti ambae alikamatwa au kuhojiwa kuhusu taarifa hizi au kuandaa mkutano na kikao hicho.
Mhe. Lissu: Je kuna mtu yeyote aliyeshitakiwa kwa kushiriki mkutano, kupanga au kuhusika na mkutano huo wa Tar. 03/04 hayupo huyo mtu mwingine.
Part 310 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 308
Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Baada ya hapo nini kilitokea?
Mnyika: Tarehe 10 December, 2024 tuliitisha Mkutano na waandishi wa Habari Makao Makuu ya Chama Mikocheni ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe aliyatangaza maazimio hayo kwa umma.
Mhe. Lissu: Nini kilitokea baada ya hapo?
Mnyika: Chama kiliingia katika maandalizi ya Mkutano mkuu wa Chama na kupokea mpango wa chama kwa miaka mitano. Na Tar. 20/01/2025 nilipeleka taarifa ya Kamati Kuu kwa Baraza Kuu la Chama iliyopendekeza pamoja na mambo mengine maazimio yale 10 ikiwemo la No Reforms: No Election
Mhe. Lissu: Ili iweje?
Mnyika: Ili maazimio yale yasiwe tena ya Kamati Kuu bali yawe ya Baraza Kuu. Pia, Baraza Kuu liyapeleke kwenye Mkutano Mkuu ili maazimio hayo yawe ni maazimio ya Mkutano Mkuu wa Chama na sio ya Baraza Kuu pekeee. Na Baraza Kuu la Tarehe 20/01/2025 liliridhia mapendekezo yote mawili.
Lissu: Baada ya Baraza Kuu nini kiliendelea?
Mnyika: Tar. 21/01/2025 Niliwasilisha taarifa ya Baraza Kuu kwa Mkutano Mkuu juu ya utendaji wa Chama kwa miaka mitano. Na ndani ya taarifa hiyo nilipeleka mapendekezo ya Baraza kuu ambayo yalihitaji kwenda kupata Baraka za Mkutano Mkuu.
Anaendelea JJ. Mkutano Mkuu kupitisha maamuzi ya kutaka kufanyika mabadiliko ya Kisheria na Kikatiba kabla ya Uchaguzi wa 2025 yenye kuwezesha kuwepo na uchaguzi huru na haki na kwamba bila mabadiliko hayo hakuna Uchaguzi. No Reforms: No Election.
Mhe. Lissu: Nani aliyekuwa Mwenyekiti wa Vikao vyote hivyo?
Mnyika: Mwenyekiti Freeman Mbowe wa wakati huo ndio aliongoza vikao vyote hivyo.
Mhe. Lissu: Nini kilitokea baada ya Mkutano Mkuu kupitisha azimio hilo?
Mnyika: Iliendelea agenda ya Uchaguzi Mkuu wa Chama ambayo iliendelea hadi Tarehe 22/01/2025 na katika Uchaguzi huo alichaguliwa Mwenyekiti Mpya wa Chama, Tundu Lissu na Makamu Wenyeviti Wawili ambao ni John Heche, Makamu Mwenyekiti Bara na Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Mzee Said.
Mhe. Lissu: Mkutano Mkuu uliamua nini kuhusu utekelezaji wa maazimio yake?
Mnyika: Utekelezaji uanze mara moja baada ya uchaguzi kukamilika.
Mhe. Lissu: Nini kilifuata?
Mnyika: Siku hiyo hiyo ya Tar. 22/01 Baraza Kuu lilikaa na Katibu Mkuu wa Chama, John John Mnyika aliteuliwa na manaibu katibu wakuu wote waliteuliwa. Na Baraza kuu lilipokea mapendekezo pia ya wajumbe wa Kamati Kuu wa kuteuliwa na Mwenyekiti na kuthibitisha uteuzi wao.
NB. JOHN JOHN MNYIKA ni Maktaba inayotembea yani Mhe. Lissu hakukosea kumteuwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama, anateleza kama hataki tu.
Mhe. Lissu: Nini kiliendelea sasa kuhusu maazimio ya No Reforms, No Election?
Mnyika: Niliitisha retreat na vikao vya sekretarieti, Viongozi wakuu na Kamati Kuu ya Chama vilivyofanyika Bagamoyo kuanzia Tar. 31/01 hadi 04/02 kwa ajili ya utekelezaji wa azimio hilo la No Reforms: No Election.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji mpango wa utekelezaji mlioufikia kwenye vikao hivyo?
Mnyika: Tulipitisha mpango wa kutoa elimu kwa umma kupitia mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali ya nchi, tulipitisha mpango wa kuwatembelea viongozi wa dini, sekta binafsi na taasisi zingine za kijamii. Tulipitisha mpango wa kuzungukia vyombo vua habari na kukutana na wahariri wa vyombo vya habari, tulipitisha mpango wa kushawishi jumuiya za kimataifa na jumuiya za kikanda, tulipitisha mpango wa kukutana na wadau mbalimbali ndani ya Chama.
Mhe. Lissu: Utekelezaji ukawaje huo?
Mnyika: Mwenyekiti alianza ziara akiambatana na viongozi wengine. Mfano alikutana na Shekhe Ponda Issa Ponda. Kwa watu mashuhuri alikutana na Jaji Joseph Sinde Warioba na kwa upande wa kuvihusisha vyombo vya habari Mwenyekiti alifanya mkutano mwezi February kuelezea maazimio ya Kamati kuu ya Bagamoyo na Baadae Tarehe 02 March alikutana na Wahariri wa Vyombo vya habari.
Part 309 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
OFFICIAL STATEMENT REGARDING MY LAWSUIT AGAINST META.
Because this matter is now before the American courts, I have been advised not to comment publicly on the details of the case. My attorney is available to provide clarification and comment where appropriate.
Though I am only one person with limited resources, I am prepared to stand and fight giants.
โIf that fight means confronting powerful American technology companies over alleged deceptive and fraudulent conduct, conduct that I allege led to the suppression of evidence concerning the mass killing of thousands of protesters on October 29, 2025, as well as the suppression of information about kidnappings, forced disappearances, and the arbitrary imprisonment of government critics, the silencing of the media, illegitimate elections, and corruption in my native country, Tanzania, then I will fight with everything in me.
I expect Meta to come at me hard, a human rights defender facing a company with vast resources. But I do wonder what might look different if that same determination and those same resources were devoted to resisting foreign-government pressure targeting a United States human rights activist or, at the very least, if the public were given greater transparency and whole truth about how such foreign government requests targeting U.S. citizens are handled.
Californians deserve better. The American public deserves better. Tanzanians deserve better. The world at large deserves better.
I have done what I believe I must do. Now the matter rests in the hands of God and the American courts.
END OF STATEMENT
Link to the lawsuit : https://t.co/jFZM68ArrG
For those who may not fully understand how devastating Metaโs alleged actions were for the people of Tanzania, Iโm sharing this link to CNN journalist Larry Madowoโs Instagram, where he speaks about it. https://t.co/kDLme0hkiQ
@LarryMadowo just won 2026 NABJ SALUTE AWARD FOR GROUNDBREAKING TANZANIA INVESTIGATION INTO THE OCTOBER 29 KILLINGS OF PROTESTORS.
Wako wapi?
Hilo ni swali linaloendelea kusumbua familia za Watanzania waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha.
Leo, dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Waathirika wa Kutoweshwa kwa Nguvu, kumbukumbu zinarejea kwa watu 83 ambao, kwa mujibu wa TLS, walidaiwa kutekwa au kupotea nchini Tanzania kati ya 2016โ2024. ๐น๐ฟ
Nyuma ya kila mmoja wao kuna familia inayosubiri majibu, ndugu anayesubiri kurudiwa, na mzazi anayekataa kuamini kwamba mpendwa wake hatarudi.
Wako wapi? Nani anawajua walipo? Na familia zao zitapata lini majibu?
Hawa si namba. Ni maisha ya watu. Ni familia. Ni maumivu yanayoendelea. @SuluhuSamia utawajibishwa kwa hili hata kama c leo
Nimejifunza kitu kimoja mapenzi sio kwa ajili ya Smart People, tafuta zimwi Lako moja pambana nalo mpaka likutoe damu ๐Mtaishi ila wote mkijifanya mko smart mtalia ๐ถโโ๏ธ
๐จ META TOOK THE ORDER. TANZANIA HID THE BODIES๐จ
@Meta@Instagram@facebook@WhatsApp @zuck
You blocked Shangazi Maria Sarungi @MariaSTsehai and Mange Kimambi @mangekimambi the voices that documented Tanzaniaโs October 2025 massacre.
A US company taking a Dar es Salaam order to bury the dead is not acceptable.
Open the accounts. Immediately.
#TanzaniaMassacre
Msiangaike na Jusa , yeye anaona kwamba Samia amemlipia kisasi ndio maana anaongea uoumbavu
Watanganyika kuitaka Tanganyika yao haitakiwi kuwa tatizo kwa ACT
Jusa yuko kwenye furaha amelipiwa kisasi kwa damu zilizimwagika ndio maana hoja yake anakwepa kabisa kusema, Watanganyika wanataka nchi yao baada ya kushuhudia Mauaji makubwa yatokanayo na Mzanzibari.
Na kweli wazanzibar kama Jusa si mnaona wanafurahia, anaongea kwa mbwembwe kabisa kwamba wacha tupelekewe moto.
Huyu ni saddest ambaye moyo wake una kisasi cha muda mrefu.
Cha ajabu ni kwa nini anakomaa tubaki kwenye mateso ya Samia, kama Wazanzibar walidai Zanzibar yao huko nyuma kama anavyosema, hizo sababu walizotoa kudai Zanzibar hazipo tena ?
Mwisho, kwenye uchaguzi wa october 25 huko Zanzibar wananchi wameisusa ACT wakapigwa, ni chama kilichokufa hata huko Zanzibar, wameamua kula asali za CCM maana wamepoteza mvuto, awawezi dai Zanzibar yao kama zamani sababu hawana nguvu ya kisiasa kufanya hivyo
"Niliwahi kumsikia Mwalimu Nyerere akisema vijana wanapaswa kuwa waasi dhidi ya mifumo kandamizi lakini sikuwahi kusikia amekamatwa kwa kauli hiyo" John Mnyika mahakamani