Salaam.
Wengi mnanitumia na kuniuliza kuhusu hii video ya wanafunzi wa kike yenye mwonekano kama hapo chini. Ufuatiliaji utafanyika na ikithibitika tukio hili limefanyika katika shule ya Tanzania, basi hatua stahiki zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria ZIKIANZIA kwa aliyewarekodi na kwenda kuwaanika mitandaoni.
Iwapo shule hii iko nchini Tanzania, na kwa kuwa nina dhamana ya sheria ya watoto chini ya umri wa miaka 18, uongozi wa shule husika uwasiliane na mimi kwa sms na 0765345777 ili kuepuka kutumia nguvu nyingi na muda mwingi kutafuta ni wapi huku.
Aidha, baadhi ya watu wameitaja shule hii na katika hatua hiyo, nimewasilisha taarifa hiyo kwa Viongozi wa maeneo hayo ili wathibitishe.
Wito; tuache kuwa tunarekodi watu kisha kupakia taarifa zinazowadhalilisha online kwani ni kinyume na sheria. Badala yake na kama inabidi, tufikishe taarifa hizo moja kwa moja kwenye vyombo rasmi au kwa Viongozi wenye dhamana ya kuchukua hatua stahiki.
Ahsanteni.
@tanpol@ortamisemitz@maendeleoyajami