GODILISTERN MALISA ATELEKEZWA MAHAKAMANI MOSHI...!
POLISI na DPP wamuacha solemba Mahakamaya Moshi,Mahakama ya mruhusu @MalisaGJ_ kuendelea na shughuli zake.
Mwanaharakati wa Kijamii,Mkurugenzi wa GH Foundation na mwanamtandao Godilistern Malisa ambaye yupo nje kwa dhamana ya Polisi mkoani Kilimanjaro tangu 08 june 2024 baada ya kukamatwa akiwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu tarehe 06 June 2024 na kusafirishwa hadi Moshi,Kilimanjaro.
June 16 July Godilistern Malisa alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni askari kutoka ofisi ya RCO-kilimanjaro
Mtu huyo alimpa maelekezo Malisa kwamba ameagizwa na Boss wake (RCO) amtaarifu kuwa anatakiwa afike Polisi,Mkoani kilimanjaro kwa ajili ya kupandishwa mahakamani baada ya faili lake kurudi kutoka kwa DPP.
Na kwamba tayari faili la lesi yake limeshasajiliwa mahakamani anatakiwa yeye tu kwa ajili ya kusomewa mashitaka yake.
Malisa na Wanasheria wake walifika Mahakamani,Moshi leo asubuhi baada ya kusafiri kutoka Dar es saalam jana usiku.
Walipo mtaarifu RCO kuwa wapo Mahakamani, RCO aliomba awasiliane kwanz na RPO kwa ajili ya kuendelea na kesi kwakuwa imefunguliwa na kusajiliwa katika mfumo wa mahakama tangu Jumanne.
Hata hivyo maafisa wa Mahakama Moshi waliingia wasiwasi baada ya kuingia katika mfumo wa mahakama na kuingiza majina ya mshitakiwa Godilistern Malisa na kukosa kesi ya aina yoyote mahakamani hapo na wakapitia orodha na Mahakimu waliopangiwa kesi mpya pia wakakosa jina la Godilistern Malisa.
Malisa alimrudia RCO na kumtaarifu mbona hawafiki Mahakamani na hakuna mtu wanaye muona kutoka Jeshi la Polisi wala ofisi ya DPP wakati umesema kesi imefunguliwa toka Jumanne.
RCO hakutoa jibu lolote zaidi ya kusema huenda imefutika katika mfumo.
Maafisa wa Mahakama Moshi wamemruhusu Godilistern Malisa kuendelea na shughuli zake kwakuwa hakuna shauri lolote linalo muhusu kwa sasa mpaka Polisi watakapofungua rasmi.
Godilistern Malisa ameondoka mahakamani hapo pasipo kumuona Polisi wala Mwanasheria yoyote kutoka ofisi ya DPP au Mwanasheria wa serikali pamoja na kupigiwa simu na kuitwa kutoka Dar es saalam.
Godilistern Malisa kwa sasa yupo njiani Kuelekea nchini Kenya kuhudhuria mkutano wa Kimataifa maswala ya matumizi ya Artificial Intelligence katika Cyber security utakao hudhuriwa na nchi 46 kutoka mabara tofauti na mgeni rasmi atakuwa Rais wa Kenya William Samoe Arap Ruto siku ya 20 July 2024.
@mR_cEleBriTyy Fanya uchunguzi wko kwa makini utakuja kugunduwa alichokieleza ni kwl au c kwl anzi juzuu ya kwanza hd mwsho sheikh wngu Allah atufahamishe ktka dini