Aliyekuwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG Prof Mussa Juma Assad amesema mtazamo wa watumishi wengi wa umma kuwa hawawezi kufukuzwa kazi kirahisi pamoja na kuendekeza maslahi binafsi ni jambo linaloichelewesha sekta ya Umma kuweza kufikia matarajio na mipango yake katika kuhudumia watanzania.
Prof. Assad amebainisha hayo jana Jumatano Juni 24, 2026 wakati akihojiwa kwenye kipindi cha M/S Podcast kupitia mtandao wa youtube, akikosoa pia utaratibu wa Ofisi za umma kuendekeza unywaji wa chai asubuhi, kwa kusema kwamba Ofisi nyingi za Umma hutumia saa mbili za mwanzo kila siku za kazi kwaajili ya chai na supu, suala ambalo binafsi alilikataa wakati akiwa CAG, akisisitiza unywaji wa chai nyumbani kabla ya muda wa kazi, akisema tofauti na sekta ya Umma, sekta binafsi imefanikiwa zaidi duniani kote kutokana na muunganiko uliopo kati ya utendaji wa wafanyakazi na kiwango cha mshahara wake.
"Na hili ndio tatizo kubwa kuwa hakuna muunganiko kati ya kiwango cha utendaji na mshahara. Mmesikia hapa nilikuwa naongea na mtu wa TTCL, ninatumia internet yao kwa karibu miaka 30 sasa na siwaachi kwasababu nataka waimprove wakati mimi nikiwa bado mteja wao, ninachowaambia siku zote nawaambia mimi ndio ninaewalipa mishahara yenu kwahiyo kuweni na mimi karibu kwasababu kama mimi sina Internet kwa wiki moja ninyi mnatakiwa mkose mshahara. Njooni muhakikishe kuwa nina internet na nilipe!. Sasa mtazamo huu ni tatizo kubwa sana katika utumishi wa umma. Ukiwa mtumishi wa umma anahisi kwamba mshahara ni suala la lazima kwake."
"Ukiwa sekta binafsi, kuna siku nilienda TTCL makao makuu wana karibu eneo kubwa kiasi la maduka, wafanyakazi kama sita wapo pale ukifika pale mteja unazubaa, mpaka mmoja akuite njoo huko. Ingia voda, wamegawanyika idara mbalimbali na wameandika kwahiyo ukiingia unajua wapi uende na wanakupokea kuuliza wakuhudumie nini. Kwahiyo wana ufanisi mkubwa, ukienda utahudumiwa na watakufuatilia na hii ndiyo muunganiko wa utendaji na mshahara kwasababu wanajua kama mteja haangaliwi, mshahara hautakuja." Amesema Prof. Assad.
Msomi huyo amebainisha kuwa tatizo hilo ni kubwa kuanzia kwenye Taasisi, Serikali za Mitaa mpaka serikali kuu, akikosoa pia utaratibu wa unywaji wa chai ofisini kwa kueleza kuwa saa mbili baada ya kufungua ofisi, Watumishi wengi wa umma wanazitumia kwaajili ya kushughulika na unywaji wa chai.
'Saa mbili za mwanzo baada ya kufungua ofisi za umma watu wanashughulika na chai na supu, yaani hata Mkurugenzi Mtendaji mwenyewe saa lake la kwanza kazini anakunywa chai. Unakunywaje chai ofisini? Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia alilikataa hili akataka kila Mtumishi kunywa chai nyumbani kwake. Kwetu mpaka leo ukifika ofisini kitu cha kwanza ni supu. Mimi nilipoteuliwa kuwa CAG niliwaambia mimi chai nakunywa nyumbani, nitakunywaje chai mara mbilimbili. Na hapa nikawa nimetengeneza shida sasa hii ndio shida kwa Ofisi zetu za umma zote, watu wamewekeza kwenye maslahi na faida binafsi badala ya kusaidia kutoa huduma kwa jamii.
@MwanzoTvPlus Ilikuwaje mpaka msajili akawa na mamlaka makubwa hivyo? nani kampa mamlaka makubwa hivyo? sasa kama huyu msajili kichaa mwenye ugonjwa wa akili anapo fanya makosa ya kimamuzi anawajibika vip anapo kuwa amekosea?
@fintanjr_ Mbona wazanzibari wana urai pacha😏 mzanzibari anaweza kuwa mtanganyika ila mtanganyika hawezi kuwa mzanzibari, huoni kivuli cha neno Tanzania kinatumika vibaya?