#MAJIBOMBANI
WAZIRI AWESO ATEMBELEA BANDA LA RUWASA
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ametembelea banda la RUWASA katika maonesho ya Wiki ya Mazingira Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Juni 2, 2025.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua mradi wa maji Hungumalwa uliyopo kata ya Hungumalwa, Kwimba mkoani Mwanza Mei 18, 2025 ambapo DG wa RUWASA injinia Wolta Kirita alihudhuria hafla hiyo.
Mradi huo unaotekelezwa na RUWASA unawanufaisha takribani wananchi 24,349 wa kata hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amezitaka Taasisi Mkoani humo kuweka utaratibu wa kufanya tathmini za Kiutendaji na amewapongeza RUWASA kwa kuweka utaratibu wa kuwa na vikao vya aina hiyo ikiwa lengo ni kutathmini utekelezaji wa majukumu yao kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa.
#Repost @ruwasa_tanga with @use.repost
γ»γ»γ»
#majibombani
Mkoa wa Tanga unaendelea na utekelezaji wa miradi 79 ya maji ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa mijini na vijijini.