Mtume ﷺ amesema:
"Mwenye kumuamini Allah na Siku ya Mwisho, aseme mema au anyamaze."
— Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim
Maneno mazuri ni ibada; yasipokuwa mema, ukimya ni bora.
Mtume ﷺ amesema:
"Mwenye kumuongoza mtu kwenye jambo jema, atapata malipo kama ya yule aliyelitenda."
— Sahih Muslim (1893)
Tujitahidi kueneza kheri, kwani thawabu zake zinaendelea kwa idhini ya Allah.
Ikiwa dini yoyote ingeshambuliwa
kwa njia ambayo Uislamu unashambuliwa kila siku,ingekwisha zamani sana.Lakini Uislamu bado upo hapa,bado unasimama imara, bado una nguvu na ndiyo dini inayokua kwa kasi zaidi duniani.Hakuna Kheri katika hii Dunia bora zaidi kuliko kuwa Muislamu.
@ABUWSUHAYLAH AI siyo source ya dini. Ni tool tu kama Google au kitabu cha kutafuta taarifa.
Muislamu anatakiwa kurejea Qur’an, Sunnah na maelezo ya Maulamaa wa Ahlus-Sunnah
Barsisa alikufuru, lakini Shetani akamtelekeza. Hatimaye Barsisa akasulubiwa.
Funzo:
Shetani humdanganya mtu kwa hatua ndogo ndogo hadi aingie kwenye madhambi makubwa. Mwisho humwacha peke yake.
Hii ni hadithi ya Barsisa, mja mwema sana kutoka Bani Israil. Hii ni miongoni mwa Isra'iliyaat (hadithi kutoka kwa Mayahudi na Wakristo), na inatumiwa kama funzo kuhusu hila na ujanja wa Shetani katika kumpoteza mwanadamu hatua kwa hatua.
kuwaambia ukweli. Walipochimba sehemu aliyotajwa, walikuta miili ya dada yao na mtoto wake. Wakammkamata Barsisa, naye alikiri kila kitu.
Wakati walipokuwa karibu kumsulubisha, Shetani akamjia Barsisa na kumwambia akikufuru kwa kumkanusha Allah, atamuokoa.
Mtume (SAW) alisema:
"Watu watatu wana haki ya kusaidiwa na Allah: mtu anayepigana jihadi kwa ajili ya Allah, mtumwa anayetafuta kujikomboa, na mwanaume anayeoa ili ajilinde na maasi."
(Hadith – Tirmidhi, Ibn Majah)