Siasa katika Kaunti ya Kisii ziligeuka vurugu Ijumaa baada ya mapumziko ya msafara wa vuguvugu la Linda Mwananchi kuishia ghasia na mapambano ya ana kwa ana.
#KTNLeoWikendi
Katibu Mkuu wa COTU, Francis Atwoli, amemkosoa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, akimwita kiongozi aliyepoteza mwelekeo na asiye na rekodi ya maendeleo.
#KTNLeoWikendi
Familia moja katika kijiji cha Mugutha, Juja, Kaunti ya Kiambu, iko katika majonzi baada ya jamaa wao wawili kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.
#KTNLeoWikendi
Shughuli ya utambuzi wa miili ya waathiriwa wa ajali ya barabarani iliyotokea Ijumaa eneo la Nyanja imeanza katika Hospitali ya Londiani, Kaunti ya Nakuru.
#KTNLeoWikendi
President William Ruto: The government did not propose any of the taxes that were widely alleged. Specifically, there was no proposal to introduce taxes on freehold land or any land for that matter. There was no proposal to introduce taxes on mitumba, and there was no change to the rental income tax as alleged.
Kitengo cha uchunguzi cha KTN kiligundua mtandao unaouza vitambulisho na stakabadhi muhimu kwa raia wa kigeni ndani ya idara ya usajili na uhamiaji, hali inayoibua wasiwasi mkubwa wa usalama wa kitaifa.
#KTNLeoWikendi
Gavana wa Murang'a Irungu Kang'ata sasa amejiunga na mrengo wa Linda Mwananchi, huku akiendeleza cheche dhidi ya serikali ya Kenya Kwanza.
#KTNLeoWikendi
Rais William Ruto amesisitiza kuwa ataendelea kutekeleza ajenda ya maendeleo aliyowaahidi Wakenya, akisema serikali yake inalenga kuimarisha maisha ya Wakenya licha ya ukosoaji kutoka kwa wapinzani wake.
#KTNLeoWikendi
Muungano wa upinzani umehitimisha ziara yake ya siku tatu eneo la magharibi mwa nchi leo kwa ibada katika Kanisa Katoliki la St. Mary's Kibabii, Kanduyi, kabla ya viongozi hao kuhutubia mikutano ya kisiasa maeneo ya Chwele na Naitiri, Kaunti ya Bungoma, na Kaunti ya Trans-Nzoia.
Wasafiri na wamiliki wa magari kote nchini usiku wa manane wataanza kupata afueni, baada ya Mamlaka ya Kudhibiti Nishati na Petroli (EPRA) kutangaza kupungua kwa bei ya mafuta ya dizeli kwa shilingi 10, huku bei ya petroli ikishuka kwa senti 22 pekee.
#KTNLeoWikendi
Sekta ya elimu ilipata mgao mkubwa wa shilingi bilioni 781.5, ikiwa ndiyo sehemu kubwa zaidi ya bajeti ya taifa. Hata hivyo, nyuma ya takwimu hizo kuna changamoto za ufadhili zinazoendelea kuongezeka.
#KTNLeoWikendi
Ikulu chini ya Rais William Ruto imepigwa kurunzi baada ya ripoti ya Mdhibiti wa Bajeti kuonyesha ilitumia shilingi bilioni 11.6 katika miezi tisa ya kwanza ya bajeti ya mwaka 2025/2026, ikizidi matumizi yaliyotengewa.
#KTNLeoWikendi
Hatma ya washukiwa waliotiwa mbaroni kwa sakata ya kuagiza mafuta nje ya nchi sasa haijulikani, huku wakitarajiwa kufikishwa mahakamani kesho ili kusomewa mashitaka dhidi yao.
#KTNLEO
Wizara ya Kawi ililazimika kutumia mamlaka ya dharura na kupuuza mfumo wa kawaida wa uagizaji mafuta wa G2G baada ya kampuni kuu ya uuzaji mafuta iliyoteuliwa kushindwa kuwasilisha mafuta nchini.
#KTNLEO
Nabii Dkt David Owuor amejipata kwenye uchunguzi kufuatia madai ya miujiza ya uponyaji wakati wa mkutano wake wa mwisho wa mwaka uliofanyika mjini Nakuru.
#KTNLeoWikendi
Maduka ya sare za shule humu nchini yanakabiliwa na changamoto ya kukidhi mahitaji ya sare za shule za Kidato cha 10 huku shule zikitarajiwa kufunguliwa Januari 12.
#KTNLeoWikendi
Rais William Ruto anaendelea kuimarisha vita dhidi ya mihadarati nchini, akiapa kuunda sheria kali za kukabiliana na wauzaji wa dawa za kulevya.
#KTNLeoWikendi
Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, na mkewe Cilia Flores, waliokamatwa, hatimaye walitua nchini Marekani usiku wa kuamkia Jumapili wakiwa chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa vitengo mbalimbali vya usalama, vikiwemo vya kupambana na dawa za kulevya (DEA).
#KTNLeoWikendi