Kwenye Viwanja vya Mwembetogwa leo Jumamosi Juni 13, 2026,wakati wa Mkutano wa hadhara wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania bara Bw. John Heche, Mwanachama wa Chadema na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Iringa Mjini Mch. Peter Saimon Msigwa amewaomba radhi wananchi wa Jimbo hilo kutokana na maamuzi yake ya kukikimbia Chama hicho na kutimkia Chama Cha Mapinduzi wakati wa Uchaguzi Mkuu, akisema anajutia kwa maamuzi aliyoyafanya yakitokana na ubinafsi uliomfanya kuchukua uamuzi aliouchukua hapo awali.
"Ninyi wananchi wa Iringa ndio mlioniweka kwenye ramani ya siasa Tanzania, nimesimama mbele yenu kwa unyenyekevu mkubwa sana kuwaomba radhi. Nilikimbia vita katikati ya matatizo, sikupaswa kufanya yale maamuzi niliyoyafanya pamoja na kwamba inawezekana niliumizwa ila nilipaswa kuangalia picha kubwa ya kutetea haki za wanyonge, kuwa sauti ya wasiokuwa na sauti, sina maneno mazuri sana, naomba mniwie radhi. Hakuna maisha magumu kama kuishi kwa wakwe, nilikuwa ukweni." Amesema Mch. Msigwa.
Msigwa akirejea historia kadhaa katika Kitabu kitakatifu cha Biblia, amesema awali alijali zaidi "ego" yake, akiahidi kuwa sasa atakuwa kama simba aliyepoteza watoto wake katika kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi CCM kinang'oka madarakani.
ONENI MPUMBAVU HUYU
Hata miezi 6 haijapita Msanii wenu alikuwa anatuambia, “Fanyeni Kazi kumamae zenu, kila kitu serikali serikali, kila siku kulalamika tu”… LEO ndio anakuja kulia baada ya kushtukia ametumika kama CONDOM na kutupwa?!
What happened? Vipi Serikali imeishiwa hela ikaja kukudai kodi nini? Na kidogo Media yako ife.. au? Ooh kumbe haihusiani na Media, mlikuwa mnafanya renovation tu. 🤣
Acha kutupigia Kelele na Mambo yako sijui Serikali haijali Muziki, Sijui Arena imefanyaje. Ulichagua upande, KUFA KIMYA KIMYA HUKO HUKO ULIPOCHAGUA.
Haujawahi kushirikiana na Wasanii Wenzako kwenye group za Wasanii, Haujawahi kutoa ushirikiano kwenye TUMA wala SHIRIKISHO LA MUZIKI. Haujawahi kujadiliana na wenzako kuhusu mambo ya ujenzi na Ukuaji wa Tasnia… Mmekuwa mnajiona mmemaliza kila kitu. Yamewashinda mnataka kuanza kupiga yowe na kutaka huruma ya Wananchi. Well, nyie mmetiwa na kuachwa, sisi wamewaua ndugu zetu so tuna msiba bado (40 haijaisha maana baadhi ya Miili haijapatikana bado). Njoo MSIBANI KWANZA then ndio tutajadili mambo ya mamiziki yenu.
Wewe ndio wa Kulilia MIUNDO MBINU YA TASNIA?! Msanii uliyebebwa na Marais (Kikwete, Magufuli), Serikali, Media (yes Clouds made you), ukawazidi wenzako kwa hatua ambazo hawajaweza kukufikia tena, alafu watu walipolilia Miundo Mbinu ukawabeza, na Walivyotaka kuiwajibisha Serikali ukawakejeli. Ghafla wewe ndio unajua nafasi ya serikali? Au ni baada ya kufeli huko “International”.
Anza wewe kwanza kutengeneza MIUNDO MBINU na Mazingira Rafiki ya Kazi kwa Wafanyakazi wako ili Serikali iige Mfano wako.
Lipa Dancers Vizuri
Lipa Wapiga Bendi Vizuri
Lipa Sound Engineers Wa Maana
Lipa Watangazaji (ili wasigome)
Lipa Artists unaowa sign WCB Vizuri (Including Mkeo hiyo)
Lipa Video Vixens Vizuri
Lipa Waimbaji wa Bendi Vizuri
Kukiwa na Show ya Live hapa leo yako na Yangu, Wapiga Bendi Watachagua kuja kupiga kwangu, maana wanajua Wakazi atawathaminisha kwa Malipo Mazuri zaidi (na hapo wewe unalipwa mara 10 yangu). Bisha?
AND YES, Unajua kwanini mnakumbukwa wakati wa Kampeni tu? Ni sababu Wanejua nyie ni Wapumbavu, msiojitambua wala kutambua Power yenu kama Wananchi na Wapiga Kura, na pia Influence na Leverage yenu kwenye kuishinikiza serikali kuleta Mabadiliko.
So Kiufupi, TOKA HAPA!! 😏
BEBERU
The Leader
Kwamba mnataka watu wakubali kutekwa na kuuwawa kwamba ni jambo la kawaida!!!
Wakikataa utekaji unasema wanaleta vurugu sio?
Yuko wapi Polepole, Mdude, Soka, Kipanya na watu maelfu mliowateka?
Kama wana makosa kwanini msiwashitaki mahakamani?
Mnaiba uchaguzi, watu wakipinga mnasema wana uchu wa madaraka!!!
Kwamba wewe unaeiba kura, kufoji na kuua watu ili ujitangaze bila ridhaa hauna uchu… Lakini anaekuambia rekebisha sheria tushindane kwa haki ndio mwenye uchu sio? Hivi mnaona Watanzania kama vile hawana akili!!!
Kwasababu ya uchu ndio maana mnataka kuchochea udini kwa faida yenu lakini sio kwa faida ya Watanzania..
“Msitufunge midomo wala msitutangazie kwamba Rais amesema Makanisa ya Gwajima yafunguliwe, Kwani nan ambae alifungia makanisa ya Gwajima? Kwanini aliyafungia sababu zilikuwa ni zipi?
Tunataka atueleze kwanza izo sababu?”-;