Trellising ni ufungaji wa nyanya kwa kutumia miti , waya na kamba. Zoezi hili hufanyika wiki tatu mpaka nne baada ya kupandikiza kabla maua hayajaanza hayajaanza kuchomoza.
Faida za trellising:
1.kupata mavuno mengi
2.kuvuna kwa muda mrefu
3.upigaji wa sumu kirahisi bila kuathiri mimea kwa kuikanyaga
4.uwekaji wa mbolea kirahisi
5.mzunguko wa hewa mzuri
6.kuepuka maambukizi ya magonjwa mbalimbali
7.kupata matunda yenye ubora na muonekano mzuri
Makovu Meusi kwenye kitako cha Tunda (Blossom Rot)
Ugonjwa huu ni hatari na dalili zake hufanana na zile za mnyauko unaosababishwa na fangasi.
Unashauriwa kutumia mbolea zenye madini ya kalsiamu kupunguza tatizo hili mara tu mmea unapoanza kutoa maua.
MBEGU YA MUDA MFUPI
- Inakomaa kati ya siku 60-75.
- Mavuno yake ni wastani wa gunia 18-24 kwa ekari.
- Inavumilia magonjwa ya virusi vya milia na madoa ya majani.
- Ni chaguo sahihi kwa maeneo makame kama pwani na kanda ya kati.
- Ina punje ngumu.
MKOMBOZI F1
Mbegu bora za mboga mboga kutoka Seed Co
-Inaustahimilivu wa magonjwa ya mnyauko na ukame
-Uzito wa tunda ni wastani wa gram 150
-Hukomaa ndani ya siku 75 mpaka 80 baada ya kupandikiza
- Mavuno kwa ekari ni tani 48 mpaka 55
- Kiasi cha mbegu kwa ekari ni gram 25