Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiapa Kiapo cha Maadili kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Taifa mara baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepiga kura katika Kituo cha Ofisi ya Kijiji Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 29 Oktoba, 2025
Wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Gwaride, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Dkt. Samia Suluhu Hassan akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, George Mcheche Masaju kuwa Rais wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Taifa mara baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA CCM
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa iliyoketi jijini Dar es Salaam , leo Jumanne tarehe 21 , Okt 2025.
#KazinaUtuTunasongaMbele
#SafariyaUshindi2025
WAGENI WAMEONGEZEKA TANZANIA
Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji imefanikiwa kuongeza idadi ya wageni wanaoingia nchini kutoka 511,243 (Julai 2020 – Aprili 2021) hadi kufikia 1,839,342 katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025.
Ongezeko hili ni matokeo ya juhudi za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchukua hatua madhubuti za kuifungua nchi kimataifa, kukuza diplomasia ya uchumi, na kuboresha mazingira ya uwekezaji na utalii.
Haya ni Mafanikio Miaka 4 ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani.
DKT. Biteko asisitiza wazazi kuthamini nafasi ya familia katika malezi na makuzi ya mtoto
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, ameitaka jamii kuthamini nafasi ya familia katika makuzi na malezi ya mtoto, kama hatua ya msingi katika kudhibiti vitendo vya watoto kukimbia familia zao na kuwa watoto wa mitaani.
Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko ametoa agizo hilo leo Mei 24, 2025, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia na kilele cha Kongamano la Malezi lililofanyika jijini Mwanza.
Ameeleza kuwa ni muhimu kuzingatia malezi bora ya mtoto tangu akiwa tumboni kwa mama hadi anapofikia umri wa miaka 18, na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikitekeleza Programu Jumuishi za Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa kipindi cha 2021 hadi 2026.
Dkt. Biteko amezindua Mwongozo wa taifa wa uanzishaji na uendeshaji wa vikundi vya wazazi vya malezi na matunzo ya mtoto, na mwongozo wa Watoto kwa muktadha wa dini ya Kikristo na Kiislamu pamoja na kuzindua kampeni maalum ya malezi kwa Watoto.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa iliyoketi jijini Dodoma, leo Jumatatu tarehe 26, Mei 2025.
#KazinaUtuTunasongaMbele
#SafariyaUshindi2025
MWENGE WA UHURU WAZINDUA NEEMA YA MAJI TANDAHIMBA – VIJIJI 5 KUFAIDIKA.
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Tandahimba umetenga Shilingi 452,500,000 kwa ajili ya kuchimba visima vitano vya maji safi na salama katika vijiji vya Mivanga, Lyenje, Dinduma, Mchangani na Michenjele, kwa lengo la kuondoa kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza wakati wa utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025, Ismail Ali Ussi, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tandahimba, Falaura Kikusa alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya Programu Maalumu ya Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inayolenga kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya majisafi na salama.
“Mradi huu ni mkakati maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kupunguza adha ya maji katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hii muhimu. Utekelezaji wake ulianza Mei 2024 na unatarajiwa kukamilika Juni 2025 kutokana na changamoto mbalimbali, licha ya mpango wa awali kumalizika Disemba 2024,” alisema Kikusa.
Kikusa alieleza kuwa hadi sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 76, ambapo miundombinu ya maji ikiwemo usimikaji wa matanki ya lita 10,000 imekamilika katika vijiji viwili vya Mivanga na Lyenje, huku usimikaji wa pampu na mifumo ya nishati ya jua ukiwa umefanyika katika vijiji vya Mivanga, Lyenje, Dinduma na Mchangani.
Kwa mujibu wa Kikusa, gharama ya kisima kimoja ni Shilingi 90,500,000 na hadi sasa Shilingi 124,106,686.40 kati ya fedha zilizotengwa tayari zimelipwa. Fedha hizo zinatokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo mpango wa Lipa kwa Matokeo, Mfuko wa Taifa wa Maji na michango ya wadau wa maendeleo.
Aidha, alisema mradi huo umetoa ajira za muda mfupi kwa wananchi wa maeneo husika wakiwemo mafundi, wapishi, na madereva, huku pia ukichochea maendeleo ya kilimo na kusaidia kupunguza magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na kuhara.
Katika kijiji cha Mivanga, kisima kimoja kina uwezo wa kuzalisha maji lita 372,000 kwa siku. Wananchi wa vijiji hivyo wametoa maeneo ya ujenzi wa visima hivyo bila fidia, yenye thamani ya takriban Shilingi 2,500,000.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmed ameishukuru serikali kupitia RUWASA kwa kutekeleza mradi huo muhimu na kusisitiza kuwa umeleta afueni kubwa kwa wananchi waliokuwa wanatumia gharama kubwa na muda mwingi kutafuta maji.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kujali ustawi wa wananchi wa Tandahimba na kuwataka wakazi wa vijiji walionufaika na mradi huo kushirikiana na serikali kuutunza ili udumu kwa muda mrefu.
Mkazi wa kijiji cha Mivanga, Bi. Asha Seleman alisema mradi huo umesaidia kupunguza gharama za maisha kwa wakazi wa kijiji hicho kwani hapo awali walikuwa wananunua ndoo moja ya maji ya lita 20 kwa Shilingi 1,000.
#Sisinitanzania #nchiyangukwanza #matokeochanya #kaziiendelee #kazinaututunasongambele #katibanasheria #mslac #SSH