Warumi 8:18-19
"Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu. Kwa maana viumbe vyote vinatazamia kwa shauku kufunuliwa kwa wana wa Mungu."
Ukisoma Story ya Nabii Eliya katika Biblia baada ya kushinda vita dhidi ya karmel (1 Wafalme 19) Malkia Yazebel alimtishia kumuua😂akapata hofu kubwa akakimbilia Jangwani huko
Akiwa amechoka na kukata tamaa akamwambia Mungu “Yatosha sasa chukua Roho yangu” 😊 akiwa na uchovu mzito akalala, Malaika Bwana akamtokea na kumwambia “Amka ule maana una safari ndefu” kuna muda hata uwe umechoka kiasi gani Piga Msosi Lala mengine yatakuja tu 🚶♀️Nisikie Amen huko nyuma 🙏
Ee Mungu, nakushukuru kwa zawadi ya siku hii mpya.
Asante kwa uhai,afya,ulinzi na neema zako zisizoisha.
Ninakabidhi mipango,kazi,biashara mikononi mwako.
Nifungulie milango ya mafanikio,kibali na baraka.
Niongoze katika maamuzi yangu, uniondolee vikwazo na unipe hekima 🙏🏼
KANUNI mojawapo ya Ufalme wa Mungu inasema hivi:
Mtu yeyote aliyemwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake, HALAANIKI. This is liberating.
Uwe na asubuhi njema.