Katika Kuikaribisha Eid Elfitri,RC. Kafulila amekaribisha Eid hiyo kwa Mashindano ya Quran ambayo yatafuatiwa na Iftar.Mashindano yamefanyika leo ktk viwanja vya Bakwata - Bariadi.Aidha mgeni rasmi wa Mashindano hayo ni Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Bw. Abdullah Juma.S. Mabodi.
Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Simiyu limetoa Elimu ya Usalama dhidi ya majanga ya Moto. Elimu hiyo ya nadharia na vitendo imetolewa leo na Kaimu Kamanda Mkoa,INSP- Faustin.F.Mtitu.
Mwaka 1 Bila JPM vita dhidi ya ufisadi kazi inaendelea na Rais SSH. Tanzania yapiga hatua kutoka nafasi ya 94 mwaka 2021 mpaka 87 kati ya nchi 180 kwa vigezo 180 mwaka 2022(Transparency International Report, Jan25, 2022).- RC Kafulila
RC Simiyu,Mhe.Kafulila na RAS Mkoa Bi Prisca Kayombo wakiwa pamoja na wajumbe wa Kamati ya usalama Mkoa na wilaya -Bariadi wakati wa ibada ya kumuaga Askari Gervas Gabriel Nzige (miaka 30) aliyefariki kwa ajali ya gari 13/3/2022 maeneo ya Salunda.Marehemu atazikwa kesho Singida.
"Sina na sijawahi kuwa na subira kwa wakandarasi wababaishaji,Nitoe wito Wakandarasi wote mkae mguu sawa, Nitafuta kazi zote zinazosuasua ili kubaki na wakandarasi wenye uwezo wa kutekeleza kazi kwa mujibu wa mikataba wanayosaini"David Kafulila Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Mhe.Kafulila ametoa siku7 kwa Kampuni ya Daska Company Ltd,kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa Barabara ya Byuna/Nkindwabiye/ Halawa barabara yenye urefu wa 14.9km.Thamani ya mradi huo ni Tsh.139.993 mln.Tofauti na hapo mkataba uvunjwe na taratibu zifuatwe kupata kampuni nyingine