Mzee @freemanmbowetz
Wanyama wa porini huua/kupigana kwa sababu zinazohusiana na mahitaji ya kuishi: chakula, kujilinda, kulinda watoto au eneo. Simba anawinda kwa ajili ya chakula siyo mateso, chuki, kisasi
Binadamu ni viumbe katili zaidi ya wanyama. Binadamu anaweza kumdhuru mwingine kwa sababu ya chuki, ubaguzi, tamaa, kulipiza kisasi, madaraka au kwa sababu anaona mwingine hafai kuishi
Kutoka Mikocheni kwenda ilipo Mahakama Kuu ya Tanzania ni umbali usiozidi 5KM. Kutoka Mikocheni kwenda Rufiji ulipo mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni umbali wa 260KM
Unaweza kusafiri kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya saa tano kuhudhuria shughuli za Serikali katili ya CCM lakini huwezi kutumia dakika 10 kutoka kwako kwenda Mahakama Kuu katika kesi ya TAL?
Huwezi kwenda safari ya 5KM kumuona Mwenyekiti wako wa chama, aliyerithi kiti chako katika uchaguzi HURU na HAKI lakini unaweza kwenda 260KM kuungana na watesi wa Mwenyekiti wako?
Nini muhimu zaidi kwako? Ni wewe ulitueleza miradi ya maendeleo haiwezi kuwa mbadala wa haki za binadamu. Leo kuna watu wanatekwa na kupotezwa, wanashtakiwa kwa ugaidi na uhaini. Hujui?
Lakini umechagua nini? Nimekusikiliza ukisema “mradi wa JNHPP usichukuliwe kisiasa kwa kuwa ni mradi unaokwenda kusaidia uchumi”. Umesahau ulitueleza nini kuhusu miradi ya MAGUFULI?
Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kwa sasa ni ‘mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya CHADEMA - ni kutokana na hiki kinachoitwa ‘ustaafu’ wa uenyekiti wa CHADEMA Taifa
Kwa maana kwamba, Freeman Mbowe yupo katika kundi sogozi la WhatsApp na mengine (kama yapo) ambayo wajumbe wa kamati kuu wanajadili kwa hisia zao tofauti masuala mbalimbali ya chama
Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu CHADEMA huwezi kwenda Mahakamani katika kesi ya kiongozi wa chama, lakini unaweza kwenda katika shughuli zinazoongozwa na mwenyekiti wa CCM
Freeman Mbowe umesahau, wakati ukishtakiwa kwa makosa ya uongo ya UGAIDI, Tundu Lissu alikuwa Belgium akijiuguza majera ya risasi. Aliomba kukutana na Rais alipokuwa Brussels
Pamoja na mambo mengine waliyokubaliana, alisema Mwenyekiti Freeman Mbowe aachiwe ndiyo tufungue ukurasa mpya. Tundu Lissu alitujulisha mwenyewe hayo alipozungumza na umma.
Tundu Lissu akiwa na siku 500 gerezani. Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe hujawahi kukanyaga Mahakamani kuanzia Kisutu hadi Mahakama Kuu hata kwa bahati mbaya.
Saa 24 baada ya Mahakama Kuu kusema Tundu Lissu ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya UHAINI ya uongo na uzandiki, Freeman Mbowe unaibuka katika shughuli za Serikali ukiwa na MAWAZIRI.
Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CHADEMA umekataa kabisa kuhudhuria shughuli zozote za CHADEMA lakini unaweza kuhudhuria shughuli unazoalikwa na WATAWALA KATILI wa CCM.
Unahudhuria shughuli za Serikali umeongozana na mawaziri wa Serikali katili ya CCM wakati ambao wanachama na wafuasi wa CHADEMA kwa mamia wamekamatwa na kushtakiwa kwa UGAIDI?
Mzee Freeman Mbowe umesahau haraka. Kuna watu walifungwa gerezani, wengine sasa ni walemavu, wengine sasa ni marehemu kwa sababu ya kupigania jina lako ukiwa kiongozi wa chama chetu.
Umesahau, wakati unakamatwa na Serikali katili ya CCM, 2021, wanachama wa CHADEMA walikwenda kuonyesha ‘solidarity’ na wewe pale KISUTU. Walikamatwa, wakashtakiwa, wakafungwa
Najutia zile siku nilisimama nawe, kukutetea na kunadi jina lako kwa nia njema kabisa nikifikiri unapambania uhuru, haki na mabadiliko ya kweli. Haikuwa hivyo. Ulitudanganya tukishindwa.
Nasema kwa kuwa kwa hiari yangu, niliamua kusimama nawe, kukunadi katika mazingira ambayo ilionekana ni kama kuuza kitimoto Mecca. Lakini sikutarajia tukishindwa, tuisaliti CHADEMA
Wengine sasa tumeelewa kwa kuchelewa sana. Hii chuki haiwezi kuwa ya kushindwa uchaguzi. Lazima kuna mafekeche mengine. Kuna kingine kimeujaza chuki moyo wako. Je, kuna mrija, umekatwa?
Najutia kumpa mtoto wangu jina lako, Freeman.
2️⃣9️⃣
Ni ngumu kumdanganya mtu aliyezaliwa tarehe 29...machale ndo kipaji chao kikuu cha hasira..anaweza hisi umemuibia na hana evidence na akawa sahihi.
Wanachauriwa wazingatie na kukiimarisha sana hiko kipaji kwenye kujikuza kimaisha.
Ni watu wenye hisia na imani kali sana
“I wish I’d be your saliva, so that I could taste your lips whenever…”
“This comes from the deepest part of my heart, this comes from the empty hole in my soul, this comes from the highest point of my spirit…”
Nasinzia Nikikuwaza 🙌🏾
Just because you said something that you didn’t mean, doesn’t mean you won’t reap from it.
Your positive confessions are a prophecy over yourself, but the negative is also true, so; Prophecize what you’re saying about yourself.
Dear Babe(AA)
If I could give you one thing in life, I'd give you the ability to see yourself through my eyes, only then would you realize how special you are to me. I love u 😍
@mpambazi_ Kifungu gani alikitumia kumrudisha mtu bungen na sifa zipi za mtu kutokuwa mbunge/kuvuliwa ubunge maana zilizopo hatuzielew/hazifwatwi
Bunge linaongozwa kwa misingi ipi(katiba ama mawazo na ubabe wao...!)
Aturudishie bunge live maana kuna watu tumelimiis