Good morning
Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.~1 Yohana 4:20-21
Sulemani aliomba Hekima, Mungu akampa na utajiri. Abraham aliomba Mtoto, Mungu akampa uzao na mataifa.
Nakuombea wiki hii Mungu akupe zaidi ya kile ulichomuomba. 🙏🏾
Majukumu ndio hutufanya tuamke hata kama tumechoka na tuna usingizi. Malengo ndio hutufanya tuchukue hatua za kuachia mashuka kila asubuhi.
Good Morning Wasaka Tonge.
Ingawa mifuko yetu haina kitu, Lakini Mioyo yetu imejaa matumaini. Tunamwamini MUNGU, ambaye hachelewi kamwe anatoa Riziki kwa wakati wake ulio sahihi 🙏🏾
Kama tungelipiza visasi kwa waliotukosea, tungewachafua waliotuchafua, tungewaharibia waliotuharibia. basi leo tusingefika hapa tulipo Kuna nguvu kubwa sana katika kusamehe.
Maisha kila wakati yatakuwa na kupanda na kushuka tunahitaji kutambua hisia zetu wakati wa nyakati ngumu huku pia tukitenga muda kusherehekea mafanikio yetu na mambo mazuri katika maisha. Kunaweza kutusaidia kuzingatia zaidi kile tulicho nacho badala ya kile tulichokosa
Kila siku jikumbushe kuwa wewe sio bora kuliko wengine, Hata hiyo nafasi ama cheo ulicho nacho kuna watu wana sifa kuliko zako, Ila Bahati haikuwa upande wao Tu.
HISTORIA YA BIBLIA - 3
Tuendelee na mfululizo wa sehemu ya Tatu kwenye Historia ya Biblia. Kama hujapitia sehemu ya kwanza na ya pili, pitia kwanza ili twende pamoja. Repost ili wengi wapate kusoma na kujua mambo yalivyo. Biblia inayo historia ndefu sana ya miaka mingi sana.