Bodi ya wakurungezi, Viongozi na Wajumbe wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wamefanya ziara katika Mgodi wa STAMIGOLD kwa lengo la kujifunza na kuongeza uelewa katika uwekezaji wa STAMIGOLD. @MadiniTanzania@STAMICOTZ
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Mhe. Adolf Ndunguru amefanya ziara yake ya kwanza katika mgodi wa STAMIGOLD uliopo wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera tarehe 18/03/2022. @MadiniTanzania@STAMICOTZ
Mhe. Ezra Chiwelesa Mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi, Meneja Mkuu wa Mgodi wa STAMIGOLD na wanawake wa Umoja wa wanawake (UWASTAMI) wakipanda miti siku ya maadhimisho ya wanawake duniani katika kata ya Nyakanazi wilayani Biharamulo Mkoani Kagera
Katika kudumisha mahusiano mema na vijiji vya karibu Mgodi wa Stamigold umekuwa ukishiriki
mahafali mbalimbali ya darasa la saba, kwenye vijiji kama Mavota, Nkukwa, Msalabani na Kaniha
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limezindua vifaa vipya vya kisasa vya uchorongaji na uchimbaji wa madini kwa kutumia vyanzo vyake vya ndani ili kuimarisha shughuli zake na kuanzisha migodi yake yenyewe. Vifaa hivyo vimegharimu Tsh. bilioni 1.7.
@STAMICOTZ@stamigold
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko ametembelea Mgodi wa STAMIGOLD ambao ni kampuni tanzu ya shirika la Madini la Taifa (STAMICO) uliopo wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera kwa ajili ya kujionea shughuli za uzalishaji zinazofanywa na wazawa. @MadiniTanzania
Wanawake wa Mgodi wa Stamigold wamesherekea uzinduzi wa kikundi cha wanawake (UWASTAMI) tarehe 3 July, 2021.
Dunia ingekuwa wapi leo bila mwanamke? Wanawake wana nafasi kubwa katika jamii yetu ya Tanzania na dunia nzima kwa ujumla.
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limetembelea Mgodi wa STAMIGOLD Juni 17, 2021 na kufanya tathmini ya kuleta umeme mkubwa mgodini kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa kiwanda. @tanescoyetu@MadiniTanzania
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungezi ya STAMIGOLD Dr. Venance Mwasse ( watatu kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya STAMIGOLD, Meneja Mkuu wa Mgodi Mh. Gilay Shamika pamoja na menejementi ya Mgodi wakati wa kikao cha bodi kilichofanyika jijini Mwanza,