#PICHA Matukio Mbalimbali katika Mkutano wa Hadhara wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga – Februari 28, 2025.
Matukio haya yaliyovutia wengi na kuwahamasisha wananchi wa Tanga. Wananchi walijitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara.
#PICHA Matukio Mbalimbali katika Mkutano wa Hadhara wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga – Februari 28, 2025.
Matukio haya yaliyovutia wengi na kuwahamasisha wananchi wa Tanga. Wananchi walijitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara.
TANGA INARUDI YA VIWANDA, UTALII NA AJIRA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. @SuluhuSamia ameeleza matamanio yake kuiendeleza Tanga, akisema kuwa serikali yake imeanza hatua za kurejesha Tanga kuwa kitovu cha viwanda na kukuza utalii wa fukwe, historia, na utamaduni.
Leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. @SuluhuSamia amegawa boti 35 za uvuvi na boti saidizi 60 kwa wavuvi wa Wilaya ya Pangani kwa mkopo, Boti zinauwezo wa kubeba tani 3 hadi 5 za samaki, hatua hii ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kuboresha sekta ya uvuvi nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. @SuluhuSamia ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Daraja la Mto Pangani na barabara ya Bagamoyo hadi Tanga yenye urefu wa KM 256.
Rais alieleza mradi huu wa miundombinu utasaidia sana kukuza fursa za kiuchumi, kiutalii, na biashara.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kumrejesha nyumbani Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba,
Akiwa ziarani Februari 24, 2025, mkoani Tanga, Rais Samia alisema:
“Mwanangu Januari arudi kwa Mama… nilimpiga kikofi, nikamfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa Mama.”
NI LAZIMA TUUZE CHAKULA NJE- DKT. SAMIA
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema ni wakati wa Tanzania kulima chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi ya chakula ikiwa ni pamoja na ziada ya kuuza nje ya nchi.
Dkt. Samia ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara, wilayani Korogwe.
DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO HAYA
RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemuagiza Waziri wa Afya, Jennister Mhagama kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga.
"Kuna fedha zipo, naomba Waziri zirekebishe hii Hospitali hapa ," alisema Dkt. Samia.
RAIS SAMIA AZINDUA BWAWA LA KIHISTORIA!
RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo February 24, 2025, amezindua bwawa la umwagiliaji la Mkomazi, lenye thamani ya shilingi 18. Billioni, ambalo litatumika kwa kilimo cha umwagiliaji kwa majira yote ya mwaka, ikiwemo kiangazi.
RAIS SAMIA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA DKT. PINDI CHANA
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana kupitia upya kanuni za fidia kwa wananchi wanaoharibiwa mazao na kudhuriwa na wanyamapori.
"Nikuagize Waziri kupitia upya kanuni."
RAIS SAMIA AIPONGEZA LUSHOTO UTUNZAJI WA MAZINGIRA
RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wananchi wa Lushoto mkoani Tanga, kwa namna ambavyo wamekuwa mahiri kwa utunzaji wa mazingira.
"Hata hali ya upumuaji hapa Lushoto ni nyepesi, kwa hiyo nawapongezeni sana".
MBUNGE wa Bumbuli, Mhe. January Makamba amemshukuru Rais, Dkt. Samia kwa namna alivyomuamini katika nafasi ya uwaziri kwa wizara mbili tofauti.
Aidha, Mhe. Makamba amesema katika kipindi alichofanya kazi na Rais Samia, alijifunza mambo mengi ya kiuongozi.
UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI BUMBULI WAZINGATIA WENYE MAHITAJI MAALUM
UJENZI wa jengo LA kisasa la Halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto, Tanga, ulioguarimu kiasi cha shilingi Bilioni 6, likiwa na vyumba 72, umezingatia kupatikana kwa huduma kwa watu wenye mahitaji maalum.
RAIS SAMIA AIPONGEZA TAMISEMI!
RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza TAMISEMI, kwa kusimamia ujenzi na ukamilikaji wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto, mkoani Tanga.
Aidha, Rais Samia amesema lengo ni kusogeza huduma kwa wananchi
RAIS AZINDUA JENGO LA HALMASHAURI BUMBULI: "JENGO HILI NI LA WANANCHI, HUDUMA ZOTE ZITAPATIKANA HAPA"
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumatatu, Februari 24, 2025, amezindua jengo jipya la Halmashauri ya Bumbuli, mkoani Tanga.
RAIS SAMIA NA ZIARA YA KISHINDO MKOANI TANGA
RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo, February 24, 2025, anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu na mwendelezo wa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali hapa nchini, pamoja na kuzungumza na wananchi.
RAIS SAMIA NA UFUATILIAJI WA MIRADI!
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na ziara katika maeneo mbalimbali hapa nchini, ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayoendelea kujengwa hapa nchini.
MBUNGE TARIMBA APELEKA SALAM NZITO KWA DKT. SAMIA!
MBUNGE wa Kinondoni, Mhe. Abbas Tarimba amemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufikisha salamu za pongezi wa Rais, Dkt. samia, kuwa hakuna anachodaiwa Kinondoni.
Ameshukuru kwa ujenzi wa daraja Jangwani, Tsh. 1.3 Trillioni.
MBUNGE SAASHISHA AKATA MZIZI WA FITINA!
MBUNGE wa Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe amebainisha namna ambavyo Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyowaheshimisha wanawake katika kuongoza maeneo mbalimbali.
Mafuwe amesema mambo mengi makubwa yamefanyika chini ya Dkt. Samia, kazi imeisha.
MBUNGE WA VITI MAALUM, MKOA WA SHINYANGA, MHE. LUCY THOMAS MAYENGA AMETAKA KUJUA NI LINI SERIKALI ITAREKEBISHA NJIA ZA KUPITA WAGONJWA (WALK WAYS) KATIKA KUTUO CHA AFYA CHA SONGWA, WILAYANI KISHAPU. SIKILIZA NONDO HAPA.