Naomba kuelewa kidg.... Hii inamaanisha waliotakiwa kuendesha wataendelea kulipwa mshahara au wataachishwa kazi kwani watakua watazamaji Tu na wanalipwa?
MAMLAKA ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imetangaza kuwa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) itachukua usimamizi na uendeshaji wa reli hiyo kwa kipindi cha miaka 27 kwa makubaliano yenye thamani ya Dola bilioni 1.4 ambayo yatatoa fursa ya kurekebisha miundombinu ya reli na kuboresha ufanisi wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Mhandisi Bruno Ching’andu amesema sehemu ya uwekezaji utajumuisha ukarabati wa reli, pamoja na ununuzi wa vichwa vipya na mabehewa, hatua inayotarajiwa kuboresha usalama na kupanua uwezo wa usafirishaji wa abiria na mizigo.
Mkataba huu wa miaka 30 utalenga kutoa huduma bora zaidi na kudumisha operesheni za TAZARA huku Serikali za Tanzania na Zambia zikitarajia kuwa mradi huu utaongeza biashara na kuimarisha usafiri kati ya nchi hizi mbili.
Kampuni ya CCECC itasimamia uendeshaji wa reli hiyo kwa miaka 27 ijayo, huku TAZARA ikifanya kazi kwa karibu kuhakikisha utekelezaji mzuri wa mradi huu.
#KitengeUpdates