Wakili Alicia Magabe, ni mke wa Mhe Tundu Lissu, walikutana wakiwa wanafunzi wa sheria UDSM mwaka 1991, na baadaye walifunga ndoa mwaka 1997. Na wamebarikiwa watoto wawili.
Hapa Mhe Adv Alicia anampigania mme wake—mbele ya mkutano wa IDU (@idualliance) 💔
#FreeTunduLissu
#FreeTunduLissuNow!
Lakini kilicho wazi ni kwamba Afrika Kusini imethibitisha kuwa inayo misuli ya kupambana.
Kwa miongo mingi, hakuna taifa lolote la Kiafrika lililothubutu kumfungia biashara Marekani.
Lakini Afrika Kusini imefanya hivyo.
Kwasasa, Marekani lazima watafute vyanzo vipya vya madini, jambo ambalo si rahisi.
Afrika Kusini lazima isake masoko mbadala, huenda ikageukia China, Urusi, au mataifa mengine.
Pia, Mahusiano ya kidiplomasia kati ya mataifa haya mawili yanaweza kudorora zaidi.
Hii ni hatua inayoonyesha kuwa Afrika Kusini si taifa la kubezwa, na dunia inashuhudia historia mpya ikitengenezwa.
Je, Marekani itapiga magoti au itajibu mapigo?
Tusubiri tuone.
The Beatles walikuwa wanapiga kazi vizuri tu mpaka pale John Lennon alipokutana na Yoko Ono.
Mambo yakabadilika.
Yule mwanamke alikuja na falsafa zake, John akabadilika, ukaribu wa kundi ukatoweka, na mwishowe kundi likasambaratika.
Leo hii ukisoma historia ya The Beatles, jina Yoko Ono linatajwa kama sababu moja wapo ya kuvunjika kwao.
Hii ni dalili ya jinsi mwanamke mmoja anaweza kubadilisha historia ya kundi lenye nguvu zaidi duniani.
Baada ya miaka mingi ya mafanikio, Michael Jackson alikuja na kauli iliyoacha wengi midomo wazi.
Kwenye moja ya mahojiano yake, alisimama hadharani na kusema.
"Tommy Mottola is the devil."
Tommy Mottola alikuwa bosi mkubwa sana ndani ya Sony Music. Sasa kwa nini MJ alisema hivyo?
Kwa nini MJ, ambaye alikuwa anamiliki asilimia 50 ya kampuni hiyo, akaamua kusema hadharani kwamba mmoja wa watu wenye nguvu ndani ya Sony alikuwa shetani?
Hili lilionyesha kwamba ndani ya ulimwengu wa muziki, kulikuwa na nguvu kubwa zaidi ya kawaida.
@MariaSTsehai Maria moyo unauma mimi sielewi kazi ya kulinda amani ni ipi kwa askari wetu? Ni amani ipi hiyo? Walinda amani goma imechafuka m23 wameteka mji wawo wametekwa pia kazi yao nini bola warudi nyumbani wakukodisha wamerudi makwao
Rais wa Marekani Donald Trump, ameibuka na mpango wa kuchukua Greenland, kisiwa kikubwa zaidi duniani.
Hii si mara ya kwanza kwa Marekani kutaka kukimiliki kisiwa hicho, lakini mchakato huu unaonekana kuwa wa kipekee zaidi kutokana na hatua za haraka zinazochukuliwa, ikiwemo safari ya mtoto wake kisiwani humo.
Kwa mujibu wa taarifa, kisiwa cha Greenland kimekuwa kwenye rada ya Marekani kwa zaidi ya karne moja.
Kisiwa hiki ni kikubwa sana, kiasi kwamba Tanzania ingeweza kuingia mara mbili.
Lakini, kwa nini Marekani inakitaka sana?
Sababu kuu ni masuala ya ulinzi wa kimkakati na rasilimali zilizopo kisiwani humo.
Kisiwa cha Greenland ni mali ya Denmark, lakini kwa miongo mingi, Marekani imekuwa ikifanya majaribio ya kukimiliki.
Rekodi zinaonyesha kuwa jaribio la kwanza lilifanyika mwaka 1867, wakati Marekani ilipojaribu kununua kisiwa hicho lakini ikaambulia patupu.
Huu ndio mkataba unaomtesa Congo DR dhidi ya Rwanda na wakulimaliza hili ni Congo DR mwenyewe.
Mapema usiku wa tarehe 16/3/1996 viongozi wa Rwanda, Uganda, Sudani kusini na Ethiopia pamoja na kiongozi wa AFDL Laulent kabila walisaini “Makubaliano ya mkataba wa Lemera”.
Mkataba huu ulikuwa na shabaha ya kuigawa nchi hiyo kubwa mikononi mwa Marekani kupitia usimamizi wa Rwanda, Uganda, Sudani kusini na Ethiopia, huku Kenya na Tanzania wakiwa ndio wenyeviti wa kuinjinia mkataba huo wa lemela.
Japo baadae Tanzania ilijitoa kuunga mkono kuigawanya Kongo baadala yake ikaunga mkono msimamo wa Laurent Kabila katika kukataa kuutekeleza mkataba wa lemela, ambao kupitia mkataba huo ilizalishwa operation maalum iliyoitwa "Operation Banyamrenge".
Operation hii ililenga kumuondosha madarakani Mobutu, kiongozi wa muda mrefu wa Kongo na kibaraka wa Marekani ambao mpaka kipindi hicho walikuwa tayari wamemchoka kutokana na mabadiriko ya siasa za dunia.
Katika Makubaliano hayo yalio fanywa kati ya Laurent Desire Kabila na mataifa hayo huku Kabila akiwa kama kiongozi wa chama cha “kuikomboa Kongo” aliyekuwa akitaka kuondosha utawala wa dikteta Mobutu Sese Seko alipewa masharti ambayo yalianishwa kwenye mkataba wa Lemera.
Ambapo moja ya masharti ilikuwa ni kishirikina na wapiganaji wa Kinyarwanda kutoka Rwanda, Uganda na watutsi walio kuwa na makazi mashariki mwa Kongo, na baadae ya mapigano atoe sehemu ya ardhi mashariki mwa Kongo kama shukrani kwa Rwanda na Uganda huku akiruhusu usalama wa taifa hilo kuwa mikononi mwao.
Makubaliano hayo yalifanyika kwenye vilima vya Lemera vilivyoko Kivu ya Kusini katika mji wa Uvira na kujulikana kwa jina hilo, la "mkataba wa lemera" makubaliano hayo yalitaka Kabila, baada ya kuwa rais wa Kongo, aruhusu mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kuwa makazi ya Wanyarwanda wa kabila la Kitutsi.
@halimamdee Najua hamtaweza kutuhadisia mlivyo enda bungeni malizeni muda wenu tu lipieni kadi za ccm mlizo kubaliana huna cha kutuambia utaishia kutusi tu
@freemanmbowetz Haya niliyajua mwamba ni mwana mageuzi tunakushukuru sana hakika huu uchaguzi nifunzo kwa ccm mana wao nikuteuwana tu hawajawahi kuchaguana wajifunze hiki miamba wawili wamepambana mwisho wa siku wanapongezana hakika hii ndio chadema ninayo ijua mungu aibariki Tanzania