@_cassianp@Jambotv_ Nakumbuka mwalimu moja ndo katoka jeshini mwaka 1997 alinititembezea kichapo mimi na rafiki angu kisa kuruka dirishani kuingia darasani wakati madarasa yenyewe yalikua hayana madilisha, nilikula mtama nikasgushiwa na ngumi ya mgongo, alafu akasema hapa jeshi tupu ๐ซ๐ซ
@Roma_Mkatoliki Vitu vya kutuletea kwenye wilaya yetu vimeisha mpaka ukatumie pesa yetu kutuletea takataka, inatusaidia nini.hiyo pesa si ukatie wazee hata 100 bima ya 60 kwa mwaka kwa ajiri ya matibabu, walio kupitisha hawakuwa serious ase watu kama hawa wanamchango mdogo sana kwenye Taifa letu
Na kama kweli kuna SUKUMA GANG mimi nawashauli hao sukuma gang waanzishe tu chama chao, waachane na ssm maana hicho ni cha MSOGA GANG na ndipo litakua anguko la ssm
SUKUMA GANG WAMEVURUGWA VIBAYA SANA๐
Hivi huyu anayejiita Askofu Josephat Gwajima anajiona yeye ni nani kwanza? Yaani anapozungumzia kanisa lake lina watu 3.8m ana maanisha kanisa lipi?
Yaani anamaanisha 3.8m gawanya kwa makanisa 2006 maana yake kila kanisa lina wastani wa waumini 1,894? Pale kwenye lile banda lake la mabati pale panaweza kukalisha watu 1,800? Na hilo liko mjini achilia mbali hayo mabanda ya mabati huko mikoani?
Nimemsikiliza sana kwa kurudiana rudia sijamuelewa kwa kweli kama kuna lolote la maana aliloliongea zaidi ya kurudiarudia mambo ya Polepole na kuendelea kuhimiza kuwa sijui Padre Kitima kapigwa nyundo. Sasa aliyesema kila anayesali Katoliki lazima apigie kura CCM nani? Au nani aliyesema kuwa kila mkristo lazima achague CCM nani?
Gwajima kaongelea suala la kukatwa kwa majina ya watu walioshinda ubunge lakini chama kikaamua kupitisha wengine kwa sababu mbalimbali .. Hivi Gwajima anawezaje kuwa kichwa maji kiasi hiki na kusahau kuwa yeye hakushinda kura za maoni kule Kawe mwaka 2020 na aliyeshinda akakatwa jina lake akapitishwa yeye kugombea ubunge. Kwani hili ni jambo gumu kwake kukumbuka? Mbona kipindi kile alishindwa kuona kuwa wananchi wa Kawe walistahili kupewa mtu waliyemchagua na siyo yeye?
Gwajima analazimisha sana kuonyesha kuwa kanisa katoliki lina ugomvi na mgombea urais wa CCM na analazimisha sana ugomvi wake na serikali na hilo analoita kanisa lake uwe wa wakristo wote. Yaani hivi kweli Gwajima anataka kuaminisha watu kuwa yeye ametembelea sijui halmashauri 160 nchi nzima na huko kote ana wafuasi 150,000? Akimaanisha 150,000 x 160 = 24,000,000 ๐
Kwa hiyo Gwajima ana wafuasi 24m nchi nzima ambao akiwaambia wasipigie kura CCM basi hawatakaa wapige kura kwa CCM au?
Unajua huyu mtu ni mjinga muda mrefu sana! Na amekuwa anatumia analoita kanisa lake kumanipulate watu na hao anaoita wafuasi wake. Sasa kweli jameni Gwajima huyu ana wafuasi 24m? Yaani anamaana 67% ya wapiga kura mwaka huu ni wafuasi wake? Ni mtu mjinga tu anaweza kusikiliza hizi porojo na huu ujinga anaoongea.
Siku 10 zilizopita alisema atarudi na kuongea mambo mazito sana na watu hawataamini. Hivi kaongea nini cha maana kwanza ? Au haya ndiyo alisema watu hawataamini kusikia au kuna mengine? Hivi haya aliyoyaongea ndiyo mambo mazito aliyoahidi na kutoa siku 10 kwa serikali kuyatekeleza? Alisema anaipa serikali siku 10 ifungulie makanisa yake la sivyo ataongea mambo magumu sana, haya ndiyo mambo magumu? Huyu na wakili wake Kibatala si walisema aliyeandikiwa barua kufungiwa kanisa siyo wao sasa imekuwaje mpaka leo hawaendi kanisani kufufua watu waliokufa kama walivyokuwa wanafanya mazingaombwe huko nyuma?
Sukuma Gang wanatakiwa wafike mahali wamalize matanga na wakubali kuwa Kambale alishakufa na hakuna jinsi wanaweza wakarudia zile zama kwa kuwa kila zama zina kitabu chake. Leo Gwajima anaongelea mambo ya rasilimali za Tanzania! Au anataka tuseme michongo ya Kambale na mtu fulani walipokuwa wanawafukuza wawekezaji wakiwemo wa madini ili wachukue hizo hisa wao? Au wanataka tusema nani alikuwa nyuma ya sanaa za makinikia ili kufukuza wawekezaji wa kule migodini kwenye dhahabu ili walete kampuni zao na wanunue hisa huko? Tumekaa kimya kwa kuwa marehemu huwa hasemwi lakini mnatulazimisha sana kutaka kuongea mambo ambayo hayana umuhimu kwa sasa.
Hamuwezi mkawa kwenye fursa za kula mema ya nchi peke yenu milele . Zamu yenu ilipita na mlifurahia sana maisha na sasa imekuja zamu ya wengine sasa nongwa za nini? Yaani chokochoko za nini? Yaani mnataka tena mle soseji na mayai peke yenu kwa kuwa wenzenu hawastahili au?
Gwajima na Polepole ni project ya mtu mmoja na script writter ni mtu mmoja ndiyo maana hawaishi kurudia rudia kuongea vitu vilevile kila siku kwa kuwa hawana ajenda ya kusema na kuongea.
Gwajima na Polepole walikuwepo nchi hii wakati Mayanga Contruction ya Kambale inapewa tenda za kujenga mabarabara kanda ya ziwa bila tenda? Walikuwepo wakati Mayanga wanajenga uwanja wa ndege Chato?
#KigogoMediaUpdates
@SuluhuSamia Amani ipi wakati watu wanavunjika mikono na miguu kwenye mwendo kasi, alafu wewe unaagiza magali mapya ya askari polisi ili wawe wanatupiga vizuri, hakuna amani hapo ase
Kama kuchuja wagombea ubunge hadi watatu ni kuua nia za watia nia, je kujipitisha kuwania urais bila kupima mapenzi ya wanachama ni busara?
Kama unataka wengine washindanishwe ili kupata bora, basi kiongozi mkuu anapaswa kuwa wa kwanza kujipima kwa wanachama na si kujipitisha