Halafu kuna Maria na walevi wenzake wanaosema sijui nchi za ulaya blah blah.. Waweke na vikwazo kwa ndege zao kuja Tanzania basi..
Tanzania utake usitake utakuja tu!.. Yaani wekeni vikwazo tunakwenda China na Russiaπ
Haya mambo kuna watu yanawaumiza sana.. Yaani wanaharakati wanaumia kweli kweli..Yaani hawapendi kabisa hikuona hivi.
Lakini vumilieni tu maana 2030 siyo mbali π
ZIARA YA RAIS SAMIA NCHI URUSI
(SIKU YA PILI) π
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Oleg Yastrebov kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni, 2026.
Rais Mhe. Dkt. Samia ametunukiwa Shahada hiyo ya Udaktari wa Heshima kutokana na mchango wake katika Mageuzi ya sekta ya Elimu, juhudi zake za kuimarisha Diplomasia ya Tanzania, pamoja na mchango wake katika kuimarisha hadhi ya Tanzania Kimataifa ikiwemo kupitia sekta ya Utalii,
#KigogoMediaUpdates
SHINDA uchaguzi halafu uamue nani awe kwenye serikali yako na Chiba.
Kwa hiyo roho inakuuma au? Yaani roho inawauma mtu kusafiri na mama yake? Eeeh basi haya ni mama yenu safirini naye nyie π
We Maria si una mama yako yule mmemtelekeza pale masaki.. Mchukue safiri naye ukipanda Qatar Airways kwenda Canada au? π
Siku ya kwanza ya ziara yangu ya kitaifa katika Shirikisho la Urusi ambapo pamoja na mambo mengine, nimepata heshima ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais Vladimir Putin jijini Moscow.
Kwa pamoja tumepongeza ukuaji wa biashara kati ya nchi zetu uliofikia asilimia 72 katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025. Hata hivyo, kwa kuzingatia historia kubwa ya ushirikiano na uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa yetu, tumekubaliana kuongeza juhudi za kukuza biashara na uwekezaji ili kuleta manufaa makubwa zaidi ya kiuchumi na ustawi wa wananchi wa nchi zetu.
Aidha, kwa lengo la kufungua fursa zaidi kwa wananchi na kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi, tumejadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati, zikiwemo sayansi na teknolojia, elimu, nishati, madini, kilimo, miundombinu na utalii.
Nimeondoka nchini leo kuelekea Shirikisho la Urusi kwa ziara ya Kitaifa kufuatia mwaliko wa Mheshimiwa Rais Vladimir Putin, ikiwa ni ziara ya pili kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya ile ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Oktoba 1969.
Ziara hii ni muhimu hasa tunapoelekea kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 ambayo inataka ushiriki mkubwa wa sekta binafsi. Tutafanya mazungumzo na wenyeji wetu yanayolenga kuimarisha ushirikiano katika sekta za kimkakati zinazogusa maisha ya wananchi.
Aidha, tutashiriki majukwaa ya biashara na uwekezaji na kutatangaza fursa zilizopo nchini, pamoja na kufungua zaidi fursa za masoko kwa bidhaa za Tanzania nchini Urusi.