KAMPUNI YA MELI TANZANIA ni Kampuni ya Serikali ya Tanzania chini ya Wizara ya Uchukuzi. Makao makuu Jijini Mwanza. Inasafirisha abiria na mizigo maziwa makuu
Timu ya Masoko na Uhusiano kwa Umma ya Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) yatembelea Bohari ya Shirika la Mafuta Uganda kujipatia uhakika wa soko la meli ya kubeba mafuta ya MT. Nyangumi pindi itakapoanza kufanya kazi.
Meli hiyo inatarajiwa kuanza ukarabati wake hivi karibuni
Timu ya Maosoko na Uhusiano kwa Umma ya Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) yakutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Uganda Ndg. Benon Kajuna na kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano hasa baada ya kubadili jina kutoka MSCL na kuwa TASHICO)
Wenyeviti jumuiya ya amani na maridhiano Tanzania Kanda ya Ziwa wakiongozwa na Alhaji Sheikh Mussa Kalwanyi(Mwenye kanzu nyeupe) wamefanya ziara TASHICO kwenye mradi wa kimkakati wa ujenzi wa meli ya MV.Mwanza unao unatarajiwa kukabidhiwa Mei 2025 ambapo sasa upo asilimia 96.
U F A F A N U Z I.
Kufuatia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi kuwa tarehe 27 na 28 Januari, 2025 Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Dar es Salaam wafanyie kazi nyumbani kutokana na barabara nyingi kufungwa ili kupisha Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi Barani Afrika, mnajulishwa kuwa Wanafunzi wa shule na vyuo pia mnapaswa kusomea nyumbani kwa siku hizo mbili.
Taasisi za sekta binafsi mnashauri kufanya vivyo hivyo ili kuepusha usumbufu ambao wafanyakazi na wanafunzi wanaweza kuupata.
Kuelekea sherehe za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar maonesho ya 11 ya biashara ya kimataifa yanaendelea katika eneo la Nyamanzi kwenye viwanja vya Dimani Zanzibar. TASHICO yaendelea kupokea wageni na kutangaza shughuli zake.
TASHICO yakutana na Ujumbe kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Maji nchini Msumbiji ili kufanya mazungumo ya ushirikiano wa kusafirisha abiria na mizigo katika ukanda wa mwambao wa Ziwa Nyasa jambo ambalo limepokewa kwa mikono miwili na ujumbe huo na kuwakaribisha TASHICO kutoa huduma katika nchi ya Msumbiji.
TASHICO yakutana na wafanyabiashara na mawakala wa mizigo wanaofanya kazi katika mwambao wa Ziwa Nyasa ili kuimarisha ushirikiano pamoja na kufahamu changamoto na kuweka mikakati ya kutatua changamoto hizo ili kuweza kuzitumia meli za MV. Njombe na MV. Ruvuma katika kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wao wafanyabiashara hao wameishauri Serikali kuona namna watakavyouchangamsha Ushiriba wa Mtwara ili nao waweze kukuza mitaji yao ya kibiashara na kuifanya kimataifa kwa kusafirisha bidhaa kwenda Malawi na Msumbiji kwa kutumia Ziwa Nyasa.
TASHICO yakutana na Wakuu wa Wilaya za Kyela, Ludewa na Nyasa ili kuweka mikakati ya ushirikiano baina ya viongozi hao na Kampuni katika kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi waishio kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa.
Ziara Hiyo imefanywa na timu ya Masoko ya Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) chini ya Mkuu Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma Ndg. Anselm Namala.
Viongozi hao wameahidi kutoa ushirikiano wa karibu katika kufikia azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha huduma za usafiri wa maji katika Ziwa Nyasa.
SERIKALI YAELEZA DHAMIRA YA KUBORESHA HUDUMA ZA USAFIRI ZIWA NYASA
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile imewahakikishia wananchi wa mwambao wa Ziwa Nyasa kuwa meli ya MV. Mbeya II ya Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) itakuwa ikisafiri kila wiki ili kukidhi mahitaji ya usafiri kwa wananchi wa mwambao huo.
Amesema kuwa katika kipindi cha hivi karibuni meli hiyo ilikuwa ikisafiri mara mbili kwa mwezi kutokana na changamoto za hali ya hewa katika ziwa na kuongeza kuwa kuanzia Januari 2025 meli hiyo itaanza kusafiri kila wiki kama ilivyokuwa hapo awali
“Nitumie nafasi hii kumpongeza Mkurugenzi Bw. Eric na timu yake na Mwakilishi wake Bw. Namala yuko hapa wametuhakikishia kuwa ratiba hii haitakuwa mara mbili tena kwa mwezi bali itakuwa ni mara moja kwa wiki kama ilivyokuwa pale awali na nitumie nafasi hii kutekeleza tuliyokubaliana, tunanataka kuona wananchi wa mwambao wa Ziwa Nyasa wanafurahia uwekezaji ambao Rais Dkt. Samia ameufanya,” Alisema.
Hali kadhalika ameipongeza TASHICO kwa kupokea ushauri kutoka kwa wabunge wa majimbo yanayopakana na Ziwa Nyasa kwa kuiomba kuifufua meli ya abiria ya MV. Songea ili kuongeza nguvu katika kuwahudumia wananchi wa ziwa hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma Ndg. Asnelm Namala alisema kuwa meli ya MV. Songea kuwa ni meli rafiki kwa mazingira ya Ziwa Nyasa na hivyo imewekwa katika mpango wa kuikarabati ili kuweza kuongeza nguvu katika kusafirisha abiria na mizigo kwa Ziwa Nyasa.
“Meli ya MV. Songea ina uwezo wa kuchukua abiria 216 na tani 50 za Mizigo kwa tathmini ambayo tumeifanya tumebaini kwamba pasi na shaka ni meli rafiki sana kwa ziwa hili kwa maana ya umbo lake lilivyo linaweza kustahamili dhoruba na hali ya hewa ya ziwa hili,” alieleza.
Meli ya MV. Mbeya II husafiri kila Alhamisi kutoka Kiwira, Kyela na kufika Mbamba Bay siku ya Ijumaa na kutoka Mbamba bay siku ya Jumamosi na kufika Kiwira siku ya Jumapili.
#tashico
#LakeNyasa
#Mbambabay
WAFANYAKAZI WA TASHICO WASISITIZWA NIDHAMU NA USHIRIKIANO KAZINI.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) wamesisitizwa kuwa na nidhamu kazini pamoja na kushirikiana katika kutekeleza malengo ya Kampuni ili kupata mafanikio yaliyolengwa katika mabadiliko ya Kampuni.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma Ndg. Anselm Namala akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji kwenye kikao hicho cha wafanyakzi 34 wa TASHICO tawi la Kyela amesema kuwa mabadiliko ya jina la Kampuni yanakwenda sambamba na mabadiliko ya maboresho ya mazingira ya kazi kwa wafanyakazi na hivyo kusisitiza wafanyakazi hao kuongeza juhudi katika kutekeleza majukumu yao.
“TASHICO ina mikakati kadhaa ya kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo kukarabati jengo lililopo hapa mjini pamoja na kuongeza vitendea kazi kwa upande wa wafanyakazi wa ofisini pamoja na wafanyakazi wa kwenye meli” alsema.
Aidha alieleza dhamira ya kubadili jina kutoka Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) na Kuwa Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) pamoja na mikakati ya kuboresha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo katika Ziwa Nyasa.
“TASHICO ina mpango wa kuikarabati meli ya MV. Songea ili kuweza kuongeza nguvu katika usafiri na usafirishaji wa mizigo katika ziwa hili maana yake ni kwamba wafanyakzi wataongezeka na hivyo ni lazima kuendelea kuboresha mazingira ya kazi katika Tawi hili,’ Alisisitiza.
TASHICO, TPA, SUMA na Polisi Reli wa kutana katika kikao cha pamoja kujadili mambo ya kiutendaji kazi yanayohusisha huduma za wateja kwa Bandari na meli vituo vya Mwanza, Nansio, Bukoba na Kemondo. Kikao kimefanyika ukumbi wa jengo la TASHICO Makao Makuu jijini Mwanza.