Kuna wakati unalazimika uutue mzigo chini ili uupange upya upate kubebeka vizuri. Vivyo hivyo kwenye maisha, kuna nyakati huna budi kupukutisha baadhi ya watu katika maisha yako ili upate fursa ya kuwapanga upya waendane na muelekeo wa maisha yako. Kupangua nako pia ni kupanga!
Ukishalazimika kusema 'unanijua mimi ni nani' ujue bado hujafikia huo umuhimu unaojitambulisha nao. Ukishafikia kuwa huyo nani hutahitaji hata utambulisho. Kujiepusha na fedheha hiyo ya kujitutumua mara kwa mara kulinda hadhi, wekeza katika utu. Utu ni utambulisho tosha sana tu!
Wewe ni muhimu kwa wale unaowafaa. Usihamishie umuhimu wako kwa wengine. Hao wengine kabla hujawataka wakupe umuhimu uliozoea kuupata, wape nao fursa ya kuuona huo umuhimu wako waliouona hao wengine katika maisha yao.
Hoja ya uongo inapaswa kujibiwa kwa hoja ya ukweli. Hoja ya uongo ikiachwa ijirudie rudie masikioni mwa watu bila majibu ya kweli ufanya ionekane ni ya kweli. Counter false narratives with factual based narratives. Simple
@tonytogolani Kaka huu ni ugonjwa wa Taifa na nisiongee mengi mana jirani zangu wako kwa mwenyekiti muda huu ugomvi wa watoto wakubwa wamegombana yy kamtolewa mme wa mwenzie siri kuwa kuna mwanamke wa nje kazaa nae na kampangia chumba mme kamkalia kooni jirani yangu maji ya shingo
Mara nyingi maneno yanayozuka katikati ya ugomvi, ambayo yawezekana hata hayahusiani na ugomvi wenyewe, ndio hugeuka kuwa ugomvi mkubwa kuliko ugomvi mlioanza nao. Weka akiba ya maneno unapokuwa na hasira usijejikuta wewe uliyekosewa ndio unalazimika hatimaye kuomba msamaha!