Kiongozi Mstaafu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict XVI (95) amefariki dunia katika makazi yake Vatican.
Taarifa ya Vatican imesema "Kwa masikitiko ninawajulisha kuwa Papa Mstaafu, Benedict XVI amefariki leo saa 9:34 katika Monasteri ya Mater Ecclesiae huko Vatican."
Klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia imethibitisha kumsajili gwiji wa soka raia wa Ureno, Cristiano Ronaldo kwa mkataba unaodumu hadi mwaka 2025.
Habari za kusajiliwa kwake zimethibitishwa Ijumaa usiku na klabu hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
#TBCfmUpdates#TBCfm
Hatimaye Lionel Messi anatimiza ndoto ya kulinyakua kombe la dunia baada ya kuiwezesha Argentina kuwa mabingwa.
Hii ni mara ya tatu Argentina kutwaa taji hilo baada ya kufanya hivyo mwaka 1978 na 1986.
#FIFAworldCup#WorldCup2022#MbungiNyumbaniBuuree#TBCfmUpdates#TBCfm
Nahodha wa timu ya Taifa ya soka ya Argentina, Lionel Messi amesema mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia 2022 ni mchezo wake wa mwisho wa Kombe la Dunia akiichezea nchi hiyo.
Haya ni mashindano yake ya tano akiwa na timu ya Taifa ya Argentine lakini hajawahi kutwaa taji hilo.
Picha mbalimbali zikimuonesha mwandishi wa habari na mpiga picha wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mkoani Manyara, Joachim Kapembe, akishiriki kwenye matukio ya kikazi enzi za uhai wake.
Joachim Kapembe amefariki dunia wakati akishuka kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro.
𝗞𝗮𝗽𝗲𝗺𝗯𝗲 𝘄𝗮 𝗧𝗕𝗖 𝗔𝗳𝗮𝗿𝗶𝗸𝗶 𝗗𝘂𝗻𝗶𝗮
Mwandishi wa habari na mpiga picha wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mkoani Manyara Joachim Kapembe amefariki dunia alipokuwa akishuka kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa usafiri wa baiskeli.
#TBCfmUpdates