Mgeukie mwanamke yeyote karibu yako mwambie, “Tabasamu!”😊😊
Katika wiki maalum ya wanawake, Tanzania Commercial Bank ikitambua nafasi ya mwanamke katika ujenzi wa uchumi, imewaletea akaunti ya Tabasamu iliyoboreshwa zaidi ili kuwajengea uwezo, kuwafanya wajiamini na kujenga maisha yao.
Akaunti ya Tabasamu haina makato ya kila mwezi, inamwezesha mwanamke kupata punguzo kubwa la bima ikiwemo bima ya elimu kwa ajili ya watoto wake na kumpa fursa ya mikopo yenye riba nafuu, anaweza kukopa hadi sh. milioni 150.
Vikundi vya akina mama na akina dada navyo havijaachwa nyuma, kwani Tabasamu ina akaunti ya akiba maalum kwa ajili ya vikundi ili kuvisaidia kufikia malengo ya pamoja.
Tembelea tawi letu leo kufungua akaunti ya Tabasamu kwa gharama ya sh. 5,000 tu.
#TabasamuAccount
#AccelerateAction
#IWD2025
#BenkiInayomwelewaMtanzania
Hodi hodi mji kasoro bahari!
💼Kibegi cha hazina toka kwa CEO kimefika salama kwa babu 👴🏾Milima ya Uluguru. Maandalizi ya TCB Selous Marathon yamebamba!🔥
#MzukaZaidi#TCBSelousMarathon
Hivi karibuni timu zetu kutoka Idara za Uendeshaji (Operations), Usimamizi wa Viashiria Hatarishi na Matekelezo (Risk Management & Compliance), pamoja na Ukaguzi wa Ndani (Internal Audit) ziliungana katika mafunzo ya kitaaluma kuhusu usimamizi madhubuti wa hatari ndani ya taasisi (Combined/Aligned Assurance), yaliyoendeshwa na Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani (Institute of Internal Auditors).
Mafunzo haya yanalenga kuimarisha mifumo yetu ya ndani na kuonyesha umuhimu wa idara zetu kufanya kazi kwa umoja, ili kuhakikisha kuwa viashiria hatarishi vinatambuliwa, vinasimamiwa, na kuthibitishwa kwa njia iliyoratibiwa na yenye ufanisi kwa benki nzima.
Tunaamini ushirikiano wa idara tofauti ni muhimu katika ujenzi wa taasisi imara na inayoaminika kwa wateja wake.
#BenkiInayomwelewaMtanzania
Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Adam Mihayo akiongozana na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Taasisi za Serikali, Bw. Richard Mtapa walihudhuria katika Jukwaa la Wakurugenzi wa Afrika.
Mkutano huo unaofanyika kila mwaka, ulifanyika Kigali nchini Rwanda mwaka huu ulijadili masuala mtambuka ikiwemo fursa za kiuchumi zilizopo barani Afrika, usimamizi wa rasilimali fedha, ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi na nchi na uchumi wa viwanda.
Bw. Mihayo pia alipata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais IFC bara la Afrika, Ethiopis Tafara ikiwa ni mwendelezo wa ushirikiano ambao benki imekuwa na taasisi hiyo ya kimataifa.
#ACF2026
#BenkiInayomwelewaMtanzania
TCB ilipata nafasi ya kuhudhuria hafla ya utiaji saini baina ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Kanda ya Maziwa Makuu (FP-ICGLR) bungeni jijini Dodoma.
Makubaliano hayo yanahusisha uenyeji kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Kwanza wa Wabunge Wanawake Eneo la Maziwa Makuu (WPC).
Benki iliwakilishwa na Bi. Massala Koroso kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Adam Mihayo.
Tanzania Commercial Bank imekuwa mfano wa kuigwa katika jitihada za kuhakikisha inajenga usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika nafasi za uongozi.
#WomenEmpowerment #BenkiInayomwelewaMtanzania
Badilisha mtazamo, jenga uwezo, na jiandae kwa mafanikio baada ya chuo!😊
Jumamosi hii hakikisha unafika chuoni, kujumuika pamoja na wanafunzi wenzako kupata maarifa kuhusu future yako baada ya kumaliza chuo.
#YouthEmpowerment#FinancialLiteracy#Genemers
#BenkiInayomwelewaMtanzania
Jumamosi hii, Benki ya Biashara Tanzania (TCB) ilipata fursa ya kukutana na kuzungumza na wanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kupitia mada ya elimu na usimamizi wa fedha kwa genemers, ambao ni kundi la wanafunzi wanaojiandaa kwa masuala ya ajira na ujasiriamali baada ya chuo.
Mazungumzo yalihusu masuala ya kibenki, uelewa wa masuala ya fedha, kukuza taaluma, na fursa zilizopo katika sekta hii. Ilikuwa furaha yetu kukutana wanafunzi wenye shauku ya kujifunza, kuuliza maswali, na kujiandaa kwa hatua inayofuata ya safari yao.
TCB Bank tunaamini kuwa, kuwawezesha vijana na maarifa ni kutengeneza jamii inayojitegemea.
#TCBBank #YouthEmpowerment #FinancialLiteracy #UDSM #Genemers
Nadhani unakumbuka nani alikuwa akikutunzia hela yako ulipokuwa mdogo😂
Leo tunasema asante mama kwa kutufundisha nidhamu ya pesa toka utotoni.
#HappyMothersDay#BenkiInayomwelewaMtanzania
TCB inaendelea kuwa karibu na Jumuiya za Watanzania waishio nje ya nchi, ikiimarisha mshikamano na kudumisha uzalendo wetu popote tulipo duniani.
Leo, tumepata fursa ya kuungana na Watanzania nchini Uholanzi katika maadhimisho ya Siku ya Utamaduni wa Tanzania, siku ya kujivunia mila, utamaduni na umoja wetu kama taifa.
Tukitambua kuwa umoja na mshikamano ni sehemu ya utambulisho wetu, TCB tunaendelea kuhakikisha Watanzania wa Diaspora wanapata huduma salama, rahisi na zenye kuaminika za kibenki, mahali popote walipo.
#TCBNyumbani
#DiasporaBanking
#BenkiInayomwelewaMtanzania
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mhe. Hassan Idd Mwamweta @hassanimwamweta Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani kwa kuupokea ujumbe kutoka TCB ulioongozwa na Bi. Lilian Mtali, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati katika Kliniki ya Diaspora nchini humo.
#TCBNyumbani
#BenkiInayomwelewaMtanzania
Hii ni zamu ya Ujerumani!🇩🇪 Benki yako pendwa inakuja Berlin kukutana na wewe. Tumekuandalia mambo mazuri ikiwemo bima ya kusafirisha mwili (body repatriation insurance cover). Usipitwe nafasi hii adimu.
#TCBinBerlin#TCBNyumbani#BenkiInayomwelewaMtanzania
Tunasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Afisa Uhusiano Tawi la TCB Masasi, Bw. Bruno Richard Helanya kilichotokea jana Masasi.
Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, wafanyakazi wenzake wa Tawi la Masasi na TCB kwa ujumla, pamoja na wote walioguswa na msiba huu mzito.
Mungu amlaze mahali pema peponi. Amina🕯️
#Tanzia
#BenkiInayomwelewaMtanzania
Amini katika ndoto yako, jiambie unaweza, anza safari yako.
Sisi benki yako tunakusikiliza na kukupatia msaada sahihi wa kifedha. Unahitaji msaada gani ili upige hatua moja mbele? Muda sahihi ni sasa!
#NdotoYakoNini?
#BenkiInayomwelewaMtanzania
Kama kuna mtu anajuta kuchelewa kupata Popote Visa Card ni huyu! Ona anavyoenjoy mwenyewe😂😂
Wahi kadi yako ya Popote Visa ujionee maisha yalivyo upande huu🕺🏽💃🏾
#PopoteVisaCard#BenkiInayomwelewaMtanzania
Twenzetu tukahesabiwe mapemaaa!😅
Msimu wa tatu wa Tamasha la Utalii la Same linaanza kesho tarehe 10 hadi 12 Aprili mkoani Kilimanjaro. TCB Bank tutakuwepo kama moja ya wadhamini, karibu tuungane pamoja kujivunia fahari ya maliasili na utalii.🏔️🌳
#MakeSameGreen
#SameUtaliiFestival2026
#BenkiInayomwelewaMtanzania
Leo tunamkumbuka Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume aliyetutoka miaka 54 iliyopita. Tunaendelea kuenzi mchango wake mkubwa katika kuijenga Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Tunawatakia mapumziko mema.
#KarumeDay#BenkiInayomwelewaMtanzania