Ujumbe wa Mwenyekiti Tundu Lissu (Sehemu ya Kwanza)
“Ndugu zangu,
Kwa wiki kadhaa sasa nimewekwa kwenye total isolation — upweke wa kulazimishwa. Wale wafungwa wenzangu waliokuwa nami kwenye selo moja, ambao walikuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo, wametolewa wote; nimeachwa peke yangu.
Selo yangu sasa imewekwa kamera za ufuatiliaji (CCTV) zinazorekodi kila kitu ninachofanya, hadi wakati ninapokojoa au kubadilisha nguo. Sina faragha yoyote tena. Hili si suala la usalama bali ni kudhalilishwa kwa utu wangu kama binadamu.
Naomba jambo hili lipigiwe kelele kwa nguvu zote, kwa sababu ni ukiukwaji wa wazi wa haki za binadamu na ni kosa kisheria chini ya Kanuni za Umoja wa Mataifa za Matunzo ya Wafungwa (Mandela Rules), ambazo zinasema wazi kuwa:
• Utu wa binadamu unabaki kuwa wa heshima hata akiwa gerezani (Kanuni ya 1),
• Upweke wa muda mrefu au unaomnyima mfungwa mawasiliano ni ukatili na mateso (Kanuni ya 43 na 44).
Pia ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 12 na 13, zinazolinda hadhi ya mtu na kumzuia kuteswa au kudhalilishwa.
Niko tayari kuvumilia hali yoyote kwa ajili ya imani yangu katika haki na uhuru wa watu wetu, lakini udhalilishaji wa utu wa binadamu hauwezi kukubalika — si kwangu tu, bali kwa yeyote anayebeba jina la mwanadamu.”
Kwanza wanangu Goma letu la #TEREMSHABUNDUKI pale youtube limefikisha Viewers 1M.
HAWA WATU 1M TUKIINGIA BARABARANI NCHI NZIMA 29.10 TUNACHUKUA NCHI ASUBUHI NA INAWEZEKANA.
Ndugu zangu watanzania, Roma amekuwa akitusemea changamoto zetu kwenye muziki wake kwa muda mrefu sana, na ni msanii ambaye amesimama na sisi hasa kwenye kipindi hiki cha #NRNE/#MO29/#OKTOBA29TUNATOKA !!
Nashauri tumpe maua yake kwa kushow love chochote ulichonacho!!
Buku, Laki, Milioni, Mwanetu Aokote!
Kama kifuta jasho kwa kazi kubwa anayofanya!!
Mimi kama Sativa naanza kwa kutoa Tsh. 150,000 kumsupport mwana.
Ametoa wimbo mpya #Teremshabunduki ni audio tu na inafanya vizuri sanaaaa!!
Anatakiwa kushoot video ya huo wimbo siku ya maandamano ili dunia ikashuhudie mapinduzi ya kihistoria Tanzania, na kila atakayeshiriki maandamano atakuwa kwenye kumbukumbu ya ukombozi!!
Tuko wengi na tunaweza tukiamua.
Napitisha bakuli tushow love kwa Mkatoliki.
🇹🇿
Lipa Namba: 350554642
Jina: ROMA MKATOLIKI
Mtandao: Vodacom-Mpesa
Kutoka - Mitandao yote.
🇺🇸 Cashapp 🇺🇸
$Roma2030
REPOST 500
#TEREMSHABUNDUKI
#MO29
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Kama mimi niliweza kutoka hapa SALAMA na kuzunguka ndani ya MBUGA YA KATAVI yenye wanyama wakali huku damu nyingi ikimwagika baada ya kupigwa risasi ya KICHWA basi na Taifa la Tanzania 29.10 linaenda kuvuka salama kutoka kwenye UTAWALA WA WATEKAJI.
Tutaandamana kulikomboa hili taifa ambalo haliheshimu UHAI wa mtu na HAKI za watu. Tunataka kuanza upya kama taifa na lazima tushinde maana sisi tunaoumizwa na haya wanayofanya watawala ni wengi kuliko kikundi kidogo kinachoneemeka na huu umwagaji damu unaoendelea kwenye TAIFA.
#MO29
#MaandamamoOktoba29
#SiriNiNamba
#TupoWengi
#OktobaTunatoka
#TUTAKUWEPO🫵😎
Tanzanian social media personality Mange Kimambi has called on citizens to take to the streets on Wednesday, October 29, 2025 to free the country from Samia Suluhu's dictatorial rule. It's boiling nicely in TZ.
UJUMBE TOKA KWA JOHN HECHE.
Wambieni watu wetu
Mimi inajulikana kwa Mungu na malaika sina ubaya na nchi yangu naipenda Sana !
Kosa langu hata sasa ni kukataa kuwa msaliti wa mageuzi ili sote katika nchi tuishi utawala wa sheria na kulinda rasilimali zetu , ,
Hapa Jela kwangu ni kama wananipaka manukato Tu sitarudi nyuma kwa makosa ya kutungiwa
Wasiogope na kusononeka wakituona tunateswa
Mungu Yuko upande Wetu
Na vita nimemkabidhi yeye
Ushindi NI wake yeye
John Heche makamu mwenyekiti wa CHADEMA jela mtumba Dodoma
Siku ya tatu 26 Oct 2025