Watumishi wa Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam ambako maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani imefanyika kimkoa leo tarehe 01.05.2025
*TFRA, NLUPC Watekeleza zoezi la urasimishaji wa mashamba mkoani Songwe*
Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent, ameridhishwa na utekelezaji wa zoezi la urasimishaji wa mashamba ya wakulima waliosajiliwa mkoani Songwe aliposhiriki kwenye zoezi la uhakiki wa hati miliki .
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA Dkt.Anthony Diallo akizungumza na wakulima wa pamba katika Kijiji cha Nekezi, Chato mkoani Geita walipofanya ziara kujionea matokeo ya uhamasishaji wa matumizi ya mbolea tarehe 18/2/2025. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo, amewataka watumishi wa TFRA wametakiwa kuwa proactive na kuhakikisha wanatatua changamoto za wakulima kwa haraka na ufanisi ili kuleta tija kwenye tasnia ya mbolea nchini.
Wafanyabiashara wa mbolea nchini mnakumbushwa kuuza mbolea kwa bei elekezi iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini au chini yake.
Bei elekezi zinapatikana kupitia:
๐ Tovuti ya Wizara ya Kilimo: https://t.co/cXrtqwc5v9
๐ Tovuti ya TFRA: https://t.co/OeQzIM3IhM
WAKULIMA KANDA YA KASKAZINI KUNUFAIKA NA UGAVI WA MASHINE ZA POS KWA WAUZAJI WA PEMBEJEO ZA RUZUKU
Ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini imeanza kugawa mashine za POS kwa wasambazaji wa pembejeo.