Neema ya Mungu wetu haina mipaka wala upendeleo.Inapofika tu, hubadilisha machozi kuwa furaha na ndoto kuwa uhalisia.Naomba neema hiyo ituguse sote! Nimegundua kuna namna sote tukiweza kumudu mahitaji yetu ya kila siku,inapunguza chuki na wivu wa kijinga.Mungu atusaidie sana!!
Na kwenye hii life, kila mtu ana safari yake.Tunapokuwa safarini, wengine hupunguza mwendo bila sisi kujua sababu. Jukumu lako si kumvuta kila mara ukisema twende! twende! Msikilize kwanza. Vitu vinavyofanya mtu apunguze mwendo ni vingi. Wengine wamechoka,wameumia,au wamefika!!
๐ฐ๐ซ ๐ซ๐๐๐๐๐๐๐ ๐จ๐๐ ๐ท๐๐๐๐๐๐๐ ๐๏ธ
Complete ID Desining And Printing โ
Event ID 10,000/=
ID za maofisini 10,000/=
ID Na kamba ikiwa Printed 15,000/=
Oda kuanzia ID 5
โ๏ธ 0769063447
Sinza Makaburini ๐
Watu wengi sana wanaojitambua huficha nafasi zao za kijamii na kiuchumi,sio kama hawapendi kuombwa msaada,Bali hawataki kuzungukwa na watu wenye upendo na heshima bandia.Kwahyo zoea kuheshimu na kuwajali watu kabla ya kujua nini wata offer kwako,jali utu na thamani ya mtu kwanza!
Usiogope aibu. Watu wengi wameinuliwa kutoka kwenye mambo ambayo jamii iliyaita ya aibu. Aibu ni ya muda, lakini amani na heshima vinaweza kudumu maisha yote.Jifunze kuikabiri aibu maana ndipo mwanga wa changamoto zako ulipo.Ukitingwa ongea,ukikimbia aibu umekimbia mafanikio.
Nilipokuwa mdogo nilikuwa nahoji na kuhukumu sana! Jamaa kawaje tena,mbona alikuwa vizuri tu?Kwa umri wake hakupaswa kuishia vile,Sasa ndoa nayo ni kitu cha kumsumbua mtu kama yeye? Sasa yule naye kile kitu ndio kitu cha kumshinda na ustaa wote ule. Naombeni msamaha,sirudii tena!
Moja ya nyakati ngumu sana maishani;
1.Umefanikiwa,unarudi nyumbani kwenu.Wale watu waliokusupport,ulioishi nao zamani angalau ufurahi nao,lakini hawapo,wamefariki wote!
2.Unaongea na mtu then katikati anakuuliz taarifa za mtu wako wa karibu sana aliyefariki,lkn yeye hajui hilo๐ญ
Nimeona watu waliojitoa sana kwa ajili ya wale wanaowapenda,lakini hakuna lolote walilopata zaidi ya maumivu.Fanya mambo kwa kiasi,mengine fanya kwa ajili yako.Usitegemee shukrani kwa mtu aliyezoea kupewa tu kila kitu na hajibidiishi,siku ukimwambia huna tegemea lawama na chuki
Technolojia ni kama kifaa tu cha kumsaidia mwanadamu kufanya maamuzi sahihi kwa data lakini sio mbadala wa uwajibikaji wa mwanadamu ๐ค .
#Elimikawikiendi
Usiishi kwa matumaini bali ishi kwa maandalizi kana kwamba chochote kile kinaweza tokea na kikitokea kikukute tayari umejiandaa ๐ค .
#Elimikawikiendi
Ukiwa na nguvu, uwezo na nafasi katika jamii, usisahau kuwajenga watu wenye maadili na upendo wa kweli. Usiwape pesa na fursa tu, wape sababu ya kuendelea kukuchagua wewe siku ambazo huna tena cha kuwapa.Thamani ya uhusiano huonekana wakati ambapo hakuna faida yoyote ya kupata!!