HABARI:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti kimelaani vikali kuendelea kushikiliwa kwa Mwenyekiti wake wa Taifa, Tundu Antipas Lissu, kikidai kuwa hatua hiyo inaambatana na ucheleweshaji wa kesi bila sababu za msingi pamoja na kukosekana kwa uwazi katika mchakato wa kisheria.
Kupitia taarifa ya Mwenyekiti wa Kanda hiyo, Lucas Ngoto, chama hicho kimesema kinasikitishwa na mwenendo wa kesi hiyo kuendelea kucheleweshwa, hali inayozua maswali kuhusu dhamira ya mfumo wa utoaji haki nchini.
“Ni jambo la kushangaza na kuhuzunisha kuona kuwa kesi inayomhusu kiongozi mkubwa wa kisiasa inaendelea kucheleweshwa bila sababu za msingi, jambo linaloibua maswali juu ya uhalisia wa mchakato mzima wa kisheria,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
CHADEMA imesisitiza kuwa Lissu, ambaye ni mwanasheria na mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa, anastahili kusikilizwa kwa haki na kwa wakati, kama ilivyo kwa raia wengine wote.
Chama hicho kimeongeza kuwa kuendelea kushikiliwa kwake kunaathiri si tu haki zake binafsi, bali pia kunadhoofisha misingi ya haki, demokrasia na utawala wa sheria nchini.
Chama hicho pia kimeeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya afya ya Lissu, kikikumbusha kuwa ni mhanga wa tukio la kushambuliwa kwa risasi mwaka 2017, lililomwacha na majeraha ya kudumu yanayohitaji ufuatiliaji wa karibu wa kitabibu. Kimeonya kuwa kushindwa kupata matibabu ya mara kwa mara kutokana na kuzuiliwa kunaweza kuhatarisha afya yake.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ucheleweshaji wa kesi dhidi ya Lissu unaongeza mateso kwake na unaweza kusababisha hali yake ya kiafya kuzorota zaidi iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.
Vilevile, CHADEMA imelaani kile ilichodai kuwa ukiukwaji wa haki za msingi dhidi ya kiongozi huyo, ikiwemo kuwekwa chini ya ulinzi mkali na uangalizi wa kamera muda wote, hali inayodaiwa kukiuka faragha yake. Pia imeeleza kuwa mazingira ya mawasiliano kati yake na mawakili wake hayatoi uhuru na usiri unaohitajika kisheria.
Aidha, CHADEMA Kanda ya Serengeti imetoa wito kwa Mahakama pamoja na mamlaka husika kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa uwazi, bila ucheleweshaji, na kwa kuzingatia misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aliwekwa gerezani kwa mujibu wa sheria, alikuwa na kesi/tuhuma/mashitaka ya uhujumu uchumi. Aliyepigwa ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria gani? Alikuwa na mashitaka/tuhuma gani?
@HabarimpyaTv Course zinazotolewa DIT ni za miaka mitatu tu, Bachelor of Engineering (BEng) na Ordinary Diploma (OD). Kama yupo mwaka wa Nne Maana yake ni kwamba “amesupp”/amerudia mwaka. Ashauriwe ajikite kwenye masomo badala ya kuwa chawa.
@privaldinho Acha utapeli mangi. GSM Group ilitoa bilioni 10 na wote tulimsikia Hersi akitamka hivyo. Hakuna mahali alitamka kuwa GSM foundation imeitolea Yanga. Badala ya kuokoteza vijisababu ombeni radhi kwa moyo mkunjufu bila visingizio na sisi tutawaelewa.
@BobWangwe Kama hii ndio arguement ya mchawi @YerickoNyerereT kuwa sababu ya kuondoka Chadema kwenda chaubwabwa, ni dhahiri kuwa alichelewa kuondoka. Walikuwa wamejimilikisha chama, kwamba wao ni lazima wawe na vyeo makao makuu ya chama as if ni wao tu ndio wanaweza kuwa viongozi.
@ItsTemba Tapeli huyo ale ubwabwa taratibu. Wakati wanabananga katiba na kujitangaza kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu alikuwa anaona sawa, ila baada ya “baba yake” kuangushwa ndio amepata akili!?