Mhasiriwa wa tatu, mwanamke mwingine, alikimbia kutoka kanisani akitafuta kimbilio katika mkahawa, duka lakini aliwindwa na kuuawa, polisi waliongeza. Wengine kadhaa wamejeruhiwa.
#topplusupdates
Watu watatu wameuawa na wengine kujeruhiwa katika kile kinachodaiwa mtu mmoja kuwachoma watu kisu wakiwa kanisani polisi wanasema kama shambulio la kigaidi katika kanisa kuu la Notre Dame katika mji wa Nice kusini mwa Ufaransa Alhamisi hii.
Saa 9:00 asubuhi kwa saa za nyumbani (saa 4:00 asubuhi) mtu mmoja aliyekuwa na kisu alishambulia watu ndani ya kanisa, na kuua mwanamke na mwanamume, polisi wa Ufaransa walithibitisha kwenye vyombo vya habari.
MSAMBATAVANGU ASHINDA IRINGA MJINI: Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Iringa Mjini amemtangaza Jesca Msambatavangu wa CCM kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 36,034 akifuatiwa na Mch. Peter Msigwa wa Chadema aliyepata kura 19,331.
#topplusupdates
PATROBAS KATAMBI ASHINDA UBUNGE SHINYANGA MJINI
- Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo amemtangaza Patrobas Katambi wa CCM kuwa Mshindi wa kiti kwa kura 31,831
- Salome Makamba(CHADEMA) aliyepata kura 16,608 ametangazwa nafasi ya 2.
#uchaguzimkuu2020#topplusupdates
Amesema, kwa ngazi za Udiwani na Ubunge wenye Mamlaka ya kutangaza ni NEC hivyo Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasaidizi wao ndio watatangaza.
#uchaguzimkuu2020#topplusupdates
NEC: MUDA WOWOTE KUANZIA SASA TUTAANZA KUTANGAZA MATOKEO YA URAIS
-
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera amesema, Tume imeanza kupokea matokeo kutoka Majimboni na kuhakiki
-
Msimamizi wa uchaguzi amemtangaza Waitara kushinda kwa asilimia 95 dhidi ya mpinzani wake Heche aliyepata asilimia 10.
#uchaguzimkuu2020#topplusupdates
Mgombea wa Chama cha mapinduzi katika jimbo la Mbeya Tulia Akson ameibuka mshindi katika uchaguzi wa eneo hilo.
Dkt Tulia Akson alimshinda mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha Chadema Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu kwa kujipatia kura 75,225.
Mgombea wa chama cha CUF Shamsia Mtamba ameshinda ubunge wa jimbo la Mtwara vijijini baada ya kupata kura 26,262, dhidi ya mpinzani wake Hawa Ghasia wa CCM aliyepata kura 18,505.
Mchezaji Paul Pogba ambae ni Muumini wa dini ya Kiislamu amejitoa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Ufaransa baada ya kuchukizwa na kauli ya Rais Macron wa Ufaransa kusema βdini ya kiislamu ndio chanzo cha ugaidi wa kimataifaβ #topplusupdates
Waandamanaji kadhaa wa misimamo mikali mjini Rome walikabiliana na polisi ya kuzuia ghasia usiku kucha wakati wa maandamano ya kupinga amri ya kutotembea nje. Polisi mjini Berlin pia waliyavunja maandamano ya kupinga vizuizi vya corona.
#TopPlusupdates
Uhispania imetangaza hali ya kitaifa ya dharura ili kupambana na wimbi la pili la virusi vya corona. Wakati ugonjwa huo ukiendelea kuenea kwa kasi Ulaya.
Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez pia alitangaza amri ya kutotembea nje usiku kote nchini humo isipokuwa kuwa tu katika
Visiwa vya Canary.
Italia ambayo ilikuwa kitovu cha mripuko wa kwanza Ulaya pia iliimarisha vizuizi vya maisha ya kila siku, kwa kuamuru kufungwa kumbi za sinema na mazoezi pamoja na mabaa na migahawa.
Rais Dkt. @MagufuliJP
amezindua kiwanda cha bidhaa za ngozi kilichopo Gereza Kuu la Karanga, Kilimanjaro. Kiwanda hicho kimewekezwa kwa ushirikiano wa PSSSF na magereza kwa TZS bilioni 136. Magereza inamiliki 14%, na kina uwezo wa kuzalisha jozi milioni 1.2 za viatu kwa mwaka.
Awali, Tanzania ilipeleka vikosi vyake kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Msumbiji baada ya kuibuka kwa mashambulizi yaliyotekelezwa na wanamgambo kutoka kaskazini mwa Msumbiji, wanamgambo ambao wamekuwapo tangu mwaka 2017. #topplusupdates
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Simon Sirro amesema magaidi zaidi ya 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya Mkoani Mtwara na kufanya uhalifu ikiwemo mauaji.