(✍🏿 na mwandishi wetu wa Dar Es Salaam)
Taarifa kutoka ndani ya kikundi cha CHADEMA zinasema kuwa mwenyekiti wa kikundi chao bwana Aikael Mbowe anapanga kuitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutangaza kuwa wanaandamana nchi nzima ikiwa ni hatua ya kushinikiza kuondokewa kwa miswada ya sheria ya uchaguzi inayotarajiwa kujadiliwa na kupitishwa na bunge la mwezi wa Februari 2024.
Bwana Mbowe mwenye wabunge 19 ndani ya bunge la Tanzania anatarajia kutangaza maandamano hayo na kutoa vitisho lukuki ikiwa ni hatua ya kikundi chao kushindwa kuzuia miswada hiyo kutojadiliwa kwa kuwa wana wabunge 19 tu ndani ya bunge wasio na uwezo na ushawishi wowote na hivyo njia pakee ya kuzuia miswada hiyo kwa mawazo yake na wanakikundi wenzake nikufanya maandamano na kutoa vitisho kwa serikali na utawala.
Bwana Mbowe amekuwa anafanya siasa za aina hii kwa miaka zaidi ya 30 hasa pale anaposhindwa kwenye hoja na masuaka basi yeye na kikundi chake huwa mara zote wanaamua kuandamanisha watoto wa watu na damu za watu zimemwagika sana kwa ajili ya hii michezo anayoifanya huku watoto wake na mke wake na mama yake na dada zake wakiwa majumbani huko Masaki na Machame wamejifungiua ndani wanakunywa mitori na visusio huku watoto wa watanzania wengine wanauwawa na kuumizwa na polisi kwa sababu ya maandamano yake haramu.
Safari hii sasa tunatarajia kumuona Bwana Mbowe akimtanguliza mbele mama yake mzazi ,mkewe na watoto wake akina James na Freelady ili tujue kuwa ana uchungu na nchi hii lakini siyo kuumiza watoto wa watu kwa slogan zao za kuitana “kamanda” sijui nini . Hata watoto wake ni “makamanda” na watangulizwe mbele kwenye maandamano haya anayopanga kuyatangaza.
Hatuwezi kuwa na wanasiasa ambao kila siku wakishindwa hoja na kushindana basi wao wanakimbilia kuandamana na kuchochea vurugu na kutoa vitisho.
Vyombo vya usalama tunawapa taarifa mapema kuwa mtu huyu na kikundi chake cha CHADEMA wanapanga kufanya maandamano nchi nzima na tunajulishwa kuwa wanataka kuwatumia wenyeviti wa kanda kuratibu maandamano hayo.Tumewapa taarifa mapema na MNAJUA C HA KUFANYA.
#KigogoMediaUpdates