MAKATAZO YA KUFUNGA SIKU YA 'EID ๐
Amesema Mtume wa Allaah swalla llaahu 'alayhi wasallama:
"HAKUNA [ni haramu] KUFUNGA KATIKA SIKU MBILI : [Eid] ALFITRI NA [Eid] AL ADH-HA"
๐ [Swahihul Bukhary - 1995]
๐ค *MAUTI* ๐
"UMMA UMEKUBALIANA JUU YA KUWA KWA HAKIKA MAUTI HAYANA UMRI MAALUMU, WALA MUDA MAALUMU, WALA UGONJWA MAALUMU; NA HIVYO BASI MTU ANATAKIWA AWE KWENYE UTAYARI NA HILO HALI YA KUJIANDAA KWA AJILI YA HILO"
โขโขโขโขโขโข
โ๏ธAl 'allaamah Abuu 'Abdi llaahi Al Qurtubiy
๐ค *ZIFAHAMU NYUMBA MBILI* ๐
_...
Amesema Al imamu Alhmad _rahimahu llaahu:_
*""DUNIA NI NYUMBA YA MATENDO, NA AKHERA NI NYUMBA YA MALIPO, HIVYO BASI AMBAYE HATOFANYA MATENDO [MEMA] HAPA [DUNIANI], ATAJUTA HUKO [AKHERA]"*
โขโขโข
๐ *Al Zuhdu Lil Bayhaqiy - [282]*
*"FAQIIH (mwenye ufahamu wa elimu ya dini) NI AMBAYE ANAMCHA ALLAAH HATA IKIWA CHACHE ELIMU YAKE, NA JAHIL (asiyefahamu elimu ya dini) NI AMBAYE ANAMUASI ALLAAH HATA IKIWA NYINGI ELIMU YAKE"*
____
โ๏ธ Al imamu Mujahid _rahimahu llaahu_
*๐ Al Bidaya wa Al Nihaya - [1/228]*
*๐ FADHILA ZA KUFUNDISHA WATU KHERI๐* ๐
๐ *HADITHI:*
Amesema Mtume wa Allaah _swalla llaahu 'alayhi wasallama:_
*"MWENYE KUWAFUNDISHA WATU KHERI, KILA KITU HUMUOMBEAYE MAGHFIRA/MSAMAHA, MPAKA SAMAKI BAHARINI(nao humuombea msamaha)"*
*๐ Swahihul Jami'i - [5883]*
๐ *HADITHI:*
Amesema Mtume wa Allaah swalla llaahu 'alayhi wasallama:
_*"HWENDA MFUNGAJI ASIWE NA (FUNGU) LOLOTE KATIKA FUNGA YAKE ISIPOKUWA NJAA TU, NA HWENDA MSIMAMAJI ASIWE NA (FUNGU) LOLOTE KATIKA KISIMAMO CHAKE ISIPOKUWA KUKESHA TU"_
๐ Swahihu Ibni Majah - [1380]
๐ค Maelezo: Hii ina maana kuwa mtu anatakiwa achunge sana kwenye ibada zake, kwanza azitekeleze kwa ikhlasw pamoja na kuzingatia utaratibu sahihi wa ibada hiyo pasina kuchanganya na vitu vyenye kuharibu ibada hiyo.
Amesema Al Fudhwaylu bnu 'Eyadhw _rahimahu llaahu:_
*"MSIWE MFANO WA CHUNGIO, LINATOA UNGA SAAFI, NA LINASHIKILIA [LINABAKIWA] NA PUMBA [TAKATAKA], MNATOA MANENO YA HEKMA KATIKA VINYWA VYENU NA INABAKIA CHUKI NA HASADI KATIKA VIFUA VYENU"*
๐ [Swifatu Al swafwa - 457]
Amesema Shaikhul Islam Ibnu Taymiya _rahimahu llaahu:_
_*"Kuomba maghfira [istighfaar] ya mtu ni muhimu zaidi kuliko dua zote"*_
_______________
๐ Jami'ul Masail - [6/277]
MKE MWEMA โ๏ธ
Mke mwema atakayekuwa kitulizo kwa mumewe, muhimu kuwa na vitu hivi vitatu: (3).
1. Amtii mumewe katika yale yasiyokuwa ya maasi.
2. Akinai na kukubaliana na hali ya mumewe.
3. Awe na kauli nzuri na mumewe.
Amesema Mtume wa Allaah _swalla llaahu 'alayhi wasallama:_
"USIMSHIRIKISHE ALLAAH NA CHOCHOTE, HATA IKIWA UTAKATWAKATWA VIPANDE AU UTACHOMWA MOTO"
_
๐ *[Swahihul Adab Al Mufrid - 14]*
Bonyeza link ๐kujiunga na channel yetu
https://t.co/92DLIbarQB
Kweli kabisa.
Shida nyoyo zimebebwa na kutawaliwa na KIBRI hakuna mtu anapenda kushuka na kujua kosa lake na kuomba SAMAHANI.
Allaah atuongoze na kutuhifadhi.