YouTube ni chuo kikuu cha bure, π Miezi 3 nyuma nilijifunza ku-add biashara kwenye Google Location, leo tayari nimepata wateja wawili. Sasa nimehamia Google Ads. Hatua kwa hatua.
Abdul,
Pengine mengi yanayosemwa mitandaoni na mitaani dhidi yako si ya kweli. Lakini ikiwa hata asilimia ndogo tu ya yanayosemwa yana ukweli ndani yake, nakusihi uyatafakari kwa makini na kuchukua hatua mapema.
Historia inatufundisha kuwa wale wanaoshangilia na kupiga makofi juu yetu leo wanaweza kuwa mashahidi wa kwanza kesho mambo yanapobadilika. Nguvu, umaarufu na ushawishi ni vitu vya muda, havidumu milele.
Kumbuka pia kwamba nafasi na mamlaka ya wazazi wetu si ya milele, na wewe bado una safari ndefu sana mbele yako kama kijana. Hekima kubwa ni kujenga heshima, uadilifu na jina jema mapema kabla ya mazingira kubadilika.
Mungu huchelewa wakati mwingine, lakini haki yake haipotei. Ikiwa kuna jambo lolote lisilo sahihi, kurekebisha njia mapema ni busara kuliko kusubiri wakati ambao marekebisho yatakuwa magumu zaidi.
Huu ni ukumbusho wa KIMUNGU, kwa nia njema. Sijui hata kwa nini nimeandika. Lakini kesho huwa inafika.