Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Rais wa Msumbiji Daniel Chapo pamoja na Rais wa Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud, Ikulu Chamwino
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa silaha za jadi Mkuki kutoka kwa Mzee Ndijina Ndilanza Ndilito, mwakilishi wa wazee wa Tanzania Bara pamoja na ngao kutoka kwa Bi. Ubwa Hamis Ally mwakilishi wa Wazee wa Zanzibar kama ishara ya kulinda na kuitetea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kuapishwa katika uwanja wa Gwaride, Chamwino Ikulu mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Siku kubwa, ya kihistoria na ya baraka za Mwenyezi Mungu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na nchi yetu, ambapo nimeungana na Mgombea Mwenza, Ndugu Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi kuzindua rasmi kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Hatua hii ni mwanzo wa safari yetu ya kwenda kwa wananchi kuomba ridhaa ya kuendelea kuwatumikia.
Tunatoka kwenda kwa wananchi kwa sababu kuu mbili; Moja, tumetekeleza kwa mafanikio makubwa Ilani ya CCM 2020 hadi 2025 ikiwemo kuboresha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo ya kiuchumi. Pili, CCM kwa umadhubuti, kuaminika kwake, utendaji wake na historia yake ni nguzo muhimu kwa utumishi na mustakabali wa Taifa letu.
Tumejipanga kuongeza nguvu na kazi katika kuihudumia nchi yetu na watu wake ambapo, katika Siku 100 za Kwanza, kipaumbele kitakuwa kwenye sekta za afya, elimu, ajira, nishati, maji na biashara tukilenga matokeo yenye kuboresha ustawi wa wananchi, hasa wenye kipato cha chini.
Niwatake wagombea na viongozi wote wa CCM, twende kwa wananchi tuwaeleze tuliyofanya na tutakayofanya. Wananchi wengi wana imani na CCM katika ustawi na mustakabali wa nchi yetu. Nguvu na ustawi wa Taifa letu viko kwenye umoja wetu, amani yetu na mshikamano wetu chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
RAIS MSTAÁFU KIKWETE AMSIFU RAIS SAMIA KWA UONGOZI WAKE WA BUSARA NA UZALENDO
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais kupitia CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kiongozi mwenye silka ya uvumilivu, subira na umakini katika kufanya maamuzi.
Dkt. Kikwete amesema Rais Samia hakurupuki katika maamuzi yake, bali hutumia muda kutafakari, kuchambua hoja na kuzingatia vigezo kabla ya kufikia uamuzi wa mwisho.
Aidha, amepongeza juhudi kubwa ambazo Rais Samia amefanya katika kulinda na kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, akibainisha kuwa changamoto nyingi zilizokuwepo zimepungua kwa kiwango kikubwa na sasa Muungano una utulivu mkubwa.
@ccm_tanzania@SuluhuSamia
#SamiaHadi2030 #DiraYaSamia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 27 Agosti, 2025.
Katika safari yangu kwa treni kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro, nimepita Ngerengere ambako nimekuwa na wakati mzuri na wananchi. Nimezungumza nao kuhusu yale tuliyofanya na tunayokusudia kuyafanya, baada ya kupata ridhaa yao katika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba.
Ahsanteni sana Ngerengere.
Hii inaonyesha Utu na Huruma ya Rais Samia kwa kupinga tabia ya hospitali “kuzuia maiti kwa sababu ya deni la matibabu”. Hii inalenga kulinda heshima ya marehemu na faraja kwa familia, hasa maskini wasioweza kulipa gharama mara moja.
#kazinaututunasongambele#sisinitanzania
Rais Samia ameongeza ajira mpya serikalini, hasa katika sekta za afya, elimu, ujenzi na utawala. Ameajiri maelfu ya walimu, madaktari na watumishi wa sekta mbalimbali. Pia, amefanikisha ajira kupitia miradi mikubwa
#sisinitanzania#kazinaututunasongambele#samiamitanotena
@sisiniTanzania Uwepo wa viongozi wote wa sasa na wastaafu unaleta uzito wa kitaifa na kuimarisha mshikamano. Mustakabali wa taifa utategemea zaidi namna vyama vyote, viongozi na wananchi wanavyoshiriki kwa heshima, amani na kufuata sheria kuelekea Uchaguzi wa 2025.