CHETI CHA PONGEZI
Ofisi ya Rais -TAMISEMI imeitunuku Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe cheti cha pongezi kwa kufikia kigezo kilichokubalika (KPI) cha ufaulu mtihani wa Taifa Darasa la Saba 2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Ndg. Emmanuel Sherembi anawatakia wanaukerewe na watanzania wote kheri ya Sikukuu ya Eid al-Fitr tusherehekee kwa pamoja huku tukimshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka ya kuhitimisha funga na ibada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani
Nawatakia Watanzania wote kheri ya Sikukuu ya Eid al-Fitr, tukimshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa baraka ya kuhitimisha funga na ibada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Eid Mubarak
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cde. Mhe. Christopher Ngubiagai akiambatana na viongozi na watendaji mbalimbali, leo Aprili 08, 2024 atafanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika kata tofautitofauti wilayani hapo.
Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe tunakupongeza Mhe. Said Mtanda uliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa kuendelea kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuhamishia Mkoa wa Mwanza kuendelea na nafasi hiyo ya Ukuu wa Mkoa.
Karibu sana
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Ndg. Emmanuel Sherembi kwa kushirikiana na Menejimenti na Watumishi wote wa Halmashauri hiyo anawatakia wakristo nchini Heri ya Ijumaa Kuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Ndg. Emmanuel Sherembi kwa kushirikiana na Menejimenti na Watumishi wote wa Wilaya hiyo, anaungana na Watanzania wote kukupongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka 3 madarakani, tunakutakia kazi njema
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe inaungana na watanzania wote kumuombea Hayati John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Tano aliyeaga Dunia Mwaka 2021, Pumnzika kwa Amani
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Hassan Bomboko Machi 13, 2024 amekabidhi rasmi Ofisi kwa Mkuu Mpya wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Emily Ngubiagai. Aidha, Mhe. Ngubiagai alimtembelea Mhe. Pius Msekwa Spika Mstaafu wa Tanzania nyumbani kwake kata ya Nkilizya Ukerewe
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Ndg. Emmanuel L. Sherembi anawatakia wananchi wote wa Wilaya hiyo na watanzania kwa ujumla mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa ramadhani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mhe. Joshua B. Manumbu anawatakia wananchi wote wa Wilaya hiyo na watanzania kwa ujumla mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa ramadhani.
Baraza la Madiwani, Menejimenti na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe tunakupongeza Mhe. Christopher Emily Ngubiagai kwa kuaminiwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Karibu Sana, Kazi Iendelee
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Ndg. Emmanuel L. Sherembi anawakaribisha wadau kushiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo kiwilaya yatafanyika Machi 06, 2024 katika Ukumbi wa Millennium Plaza uliopo kata ya Nansio kuanzia saa 3:00 Asubuhi.