#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 405
Mahakama inaanza majira saa tisa kasoro alasiri.
Majaji walishaingia, Mhe. Lissu yupo na Upande wa Jamhuri wapo.
Anasimama Nassoro Katuga anasema mchana huu hayupo Ajuaye na Job Mrema na sisi tuko tayari kuendelea.
Mshitakiwa Mheshima Tundu Lissu anasema yupo tayari kuendelea pia.
Shahidi no. 5, John Heche tayari alishapanda zake kizimbani hata kabla hajaitwa, hana muda wa kupoteza 😂
Jaji Ndunguru anamwambia Shahidi nakukumbusha kwamba upo chini ya kiapo.
Mhe. Lissu anasema nikumbushwe nilipoishia ili tuendelee.
Anakumbushwa.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa jambo lingine mlilozungumzia kwenye hivyo vikao?
Heche: Kukomeshwa vitendo vya utekaji nyara, ubambikaji wa kesi za uongo kwa watu kwa ujumla ni kuupitia mfumo wote wa Haki jinai na kurudisha Demokrasia ya kweli.
Mhe. Lissu: Kuhusu ratiba ya mambo hayo mliyokuwa mnayazungumzia?
Heche: Katika mapendekezo yetu tulikuwa na roadmap ya namna ya kukwamua mchakato wa Katiba mpya na ratiba nzima ambayo ilisema mambo yote yangekamilika kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za mwaka 2024.
Mhe. Lissu: Mazungumzo hayo yaliishaje?
Heche: Wakati wote tulipokuwa tunazungumza tulipeleka kwa maandishi ratiba na mapendekezo yetu.
Wajumbe wa CCM walikuwa wanatusikiliza na wanabeba kwamba wanaenda kufanya consultation na Rais ambae aliteua hiyo timu kumueleza hayo tunayozungumza ili tuwe kwenye picha moja.
Kuna wakati Mh. MBOWE NA KINANA wameenda kumuona Rais kwa Pamoja kupeleka mazungumzo tuliyokuwa tumefanya kwenye kikao.
Makubaliano ilikuwa Mbowe na Kinana wafanye Press conference ya pamoja kuelezea walichokubaliana, mazungumzo yaliisha pale tuliposema tujibiwe kwa maandishi kuwa tuandikieni na nyie upande wa CCM na Serikali kuwa kati ya mapendekezo yetu yote yapi tumekubaliana.
Mhe. Lissu: Waliwajibu kwa njia gani?
Heche: Walitujibu kwa njia ya maandishi na kwenye majibu yao walisema kwamba wamekataa mambo yote tuliyokubaliana kwenye vikao hivyo vya Maridhano.
Mhe.Lissu: Hayo majibu waliyaleta lini?
Heche: Siwezi kukumbuka exactly tarehe lakini ilikuwa mwaka 2023 na sisi tuliendelea na ziara zetu kwenda kwa wananchi so mazungumzo yetu na CCM yakaishia hapo.
Mhe. Lissu: Siku ya Tarehe 29/10/2025 wewe ulikuwa wapi na kama ukishiriki kwenye kupiga kura?
Heche: Hiyo Tarehe 29/10 nilikuwa kituo cha Polisi Mtumba Dodoma ambapo nilikamatwa tangu tarehe 22/10 huo huo.
Nilipotoka Polisi nilipata taarifa nyingi kuhusiana na kilichotokea, watu kuuwawa kwa zaidi ya watu 518 na Mzee Joseph Warioba anasema watu waliouwawa ni wengi kuliko waliokufa kwenye vita ya Kagera.
Anasimama Katuga anasema sio kwamba napinga lakini hiyo habari ya Mzee Warioba ni Hearsay Evidence haipaswi kuchukuliwa.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji kama hapingi amesimama kufanya nini? Pia kuna mambo yanasemwa kama ni sheria vile lakini sio sheria kabisa.
Hearsay Evidence inahitaji kuwa Corroborated na ushahidi mwingine, mimi nimebaki na mashahidi wengine watatu kwahiyo atulie tu na mwisho yeye ana nafasi ya kuja kufanya Cross Examination sasa si asubiri aje kumuuliza maswali shahidi.
Jaji Ndunguru: Haya tuendeleee.
Mhe. Lissu: Ahsante. Haya ulisemaje hapo?
Heche: Nilitaka kumalizia kwa kusema hakuna Serikali imewahi kuua watu wengi toka vita vya majimaji hadi leo, hii ndo Serikali imeua watu wengi sana.
Part 406 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 404
Makam Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Waeleze ufahamu wako juu ya jitihada za mazungumzo na Serikali kabla ya msimamo wa No reforms, No election?
Heche: Mimi binafsi nilishiriki, nilikuwa kwenye team ya CHADEMA iliyokutana na Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwepo mwaka 2022- 2025 Ikulu Dodoma.
Tulizungumza nae kutokana na malalamiko ya uchaguzi ya muda mrefu hasa uchaguzi wa 2019 na 2020 baadae Chama kilianzisha madai ya kampeni ya Katiba Mpya na mifumo ya uchaguzi wakati huo Mwenyekiti alikuwa ni Freeman Mbowe.
Tulienda Mwanza mwaka 2021 tulifanya Kongamano la kudai Katiba Mpya ili kuwezesha mabadiliko ya Uchaguzi, kama nilivyoeleza Mbowe alikamatwa na mimi nilikamatwa.
Baada ya Mbowe kutokea Ikulu ndio tukaenda kukutana na Rais Ikuku Chamwino Dodoma alikuwepo Mwenyekiti Mbowe, Said Issa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama chetu Zanzibar, Katibu Mkuu John Mnyika, na mimi mwenyewe.
Upande wa Serikali alikuwepo Rais Samia, Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati huo Jaji Eliezer Mbuki Feleshi, Waziri George Simbachawene, Jenister Mhagama sasa ni marehemu ila alikuwa Waziri,
Upande wa CCM alikuwepo Makamu Mwenyekiti wa CCM wa wakati huo mzee Abdullahiman Kinana na viongozi wengine wa CCM siwakumbuki vizuri.
Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu walieleza jinsi ambavyo tumenyanyaswa na kuonewa na uharibifu wa Uchaguzi,
Watu waliokimbia nchi na mambo mengine yaliyotokana na uchaguzi kwenye kile kikao ilikubaliwa kuwa iundwe Team ya watu watano, watano kutoka kila chama na upande wa Serikali.
Hizo team zingeenda kupitia kwa kina mifumo ya uchaguzi, matatizo ya kiuchaguzi na mapendekezo ya mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi kabla ya 2025.
Upande wa Chadema iliundwa team iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Mbowe, Katibu Mkuu John Mnyika, Wakili Jeremia Mtobesya, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama kutoka Zanzibar Mhe. Zeudi Mvano, na mimi John Wegesa Heche nilikuwemo.
Upande wa CCM namkumbuka Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdullahiman Kinana, Andrew Chenge, wawakilishi wawili kutoka Zanzibar siwakumbuki majina yao na kulikuwa na Mawaziri, mwanzo aliingia Jenister Mhagama na baadae akaja Simbachawene.
Hayo mazungumzo yalichukua mwaka mzima na sehemu tuliandika na kupeleka mapendekezo yetu namna ya kukwamua mchakato wa Katiba namna ya kuukwamua, mapendekezo ya kisheria namna ya kuukwamua mchakato wa Katiba, Vyombo ambavyo vingeundwa katika kuhakikisha vinaandika katiba kuanzia mwanzo ikiwemo kuchakata maoni.
Tulipeleka pia mapendekezo ya sheria ya Uchaguzi, mapendekezo ya namna ya kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, tulizungumza kuhusu kesi mbalimbali watu wetu walizokuwa wamebambikiziwa na wengine kufungwa kwa uongo, tulizungumza kuhusu viongozi waliokuwa wamekimbia nchi kwasababu ya usalama wao Makamu Mwenyekiti Mhe. Lissu, Godbless Lema, Ezekia Wenje Dibogo na wengine, madai ya kuwaondoa wabunge 19 (Covid-19) ambao walijipeleka Bungeni kinyume na taratibu za chama,
Tulizungumza kuhusu kufungulia mikutano ya hadhara iliyokuwa imefungwa kwa tamko la Rais Magufuli kinyume cha Sheria, namna ya kukomesha matukio ya utekaji watu.
Mhe. Lissu: Naomba tuahirishe baada ya lisaa na nusu turejee shahidi aje kuendelea na nina uhakika atamaliza leo
Jaji Ndunguru: Wakili wa Serikali
Katuga: hatuna pingamizi
Jaji Ndunguru: tujitahidi tumalizane na huyu shahidi
Kesi inaahirishwa hadi saa nane na nusu
Inapigwa High Coooiuuuurttt
Majaji wanatoka na watu wanatoka.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 402
Makam Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la kuzuia Uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu?
Heche: Sina ufahamu wa uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye kanuni ya Adhabu
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye Kanuni ya Adhabu.
Heche: Sina ufahamu wa kosa la kukinukisha kwenye Kanuni ya Adhabu
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024??
Heche: Hakuna uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye Sheria hiyo ya Uchaguzi.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024???
Heche: Hakuna hilo kosa la kuzuia uchaguzi
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024
Heche: Hakuna uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2024.
Mhe. Lissu: Shitaka linalonikabili linasema nilitengeza nia ya kuzuia uchaguzi wa 2025, waeleze majaji uwepo wa kosa la kutengeneza nia ya kuzuia uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu???
Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna uwepo wa kosa la kutengeneza nia ya kuzuia uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la kutengeneza nia ya kuzuia uchaguzi kwenye Katiba???
Heche: Hakuna kosa la kutengeneza nia ya kuzuia Uchaguzi kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno Serikali ya JMT kwenye hotuba yangu?
Heche: Hakuna mahali popote ambapo Mhe. Tundu Lissu alitaja Serikali ya JMT.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu uwepo wa maneno Rais wa JMT.
Heche: Hakuna maneno Rais wa JMT kwenye hotuba iliyotolewa na Tundu Lissu
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu uwepo wa maneno Makamu wa Rais wa JMT.
Heche: Hakuna uwepo wa maneno Makamu wa Rais wa JMT.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Waziri Mkuu wa JMT kwenye hotuba yangu ya tarehe 03/04/2025
Heche: Hakuna mahali ambapo alitajwa Waziri Mkuu wa JMT.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Baraza la Mawaziri wa JMT kwenye hotuba yangu?
Heche: Hakuna maneno Baraza la Mawaziri wa JMT kwenye hotuba ya Lissu.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Waziri, Naibu Waziri, Wakuu wa Mikoa au Wilaya?
Heche: Hakuna maneno Waziri, Naibu Waziri, wakuu wa mikoa au wilaya kwenye hotuba ya Tundu Lissu.
Mhe.Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Mkurugenzi wa Mashtaka?
Heche: Hakuna uwepo wa maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya JMT au Mkurugenzi wa Mashtaka.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno halmshauri ya Mji, jiji, wilaya au Serikali ya mtaa?
Heche: Kwenye hotuba nzima hakuna maneno Halmashauri ya mji, jiji, wilaya, kitongoji , kijiji wala serikali ya mtaa.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno Wakurugenzi wa jiji, Manispaa, Halmashauri wala watendaji wa kata, vijiji?
Heche: Waheshimiwa Majaji kwenye hotuba yote Hakuna maneno wakurugenzi wa jiji, manispaa, halmashauri wala watendaji wa kata na vijiji.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno jeshi la polisi, jeshi la ulinzi, jeshi la akiba, mgambo wa jiji, jeshi la wananchi wa Tanzania na maneno ya aina hiyo???
Heche: Hakuna maneno Jeshi la Polisi, Jeshi la Ulinzi, Jeshi la akiba, mgambo wa jiji, Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye hotuba nzima ya Lissu.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka yanamtishia nani?
Heche: Waheshimiwa majaji, hayo maneno ni ya kawaida tu na wala hayajamtishia mtu yeyote.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji maneno niliyokusomea yana kosa gani?
Heche: Waheshimiwa majaji hayo ni maneno ya kawaida kwenye siasa hivyo hayana kosa lolote.
Part 403 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 401.
Makam Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji utofauti wa hotuba yangu ya tarehe 03/04/2025 na hotuba za mikutano ya hadhara na tulipokutana na wadau.
Heche: Hotuba ya tarehe 03/04/2025 ni iileile na hotuba na wadau na mikutano ya hadhara hakuna utofauti labda ni maneno tu lakini alizungumzia matatizo ya uchaguzi na namna ya kuyarekebisha.
Mhe. Lissu: Kuna ushahidi umeletwa hapa kuwa mkutano wa tarehe 03/04/2025 ulilushwa live?
Heche: Mimi nilikuwa ndani kwenye mkutano sina ufahamu kama ulikuwa live au haukuwa live lakini waandishi wa habari walikuwepo kwenye mkutano.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kuhusu recordings za mkutano huo wa Tarehe 03/04/2025 kama uliona kwenye Jambo Tv??
Heche: Niliona kwenye YouTube channel mbalimbali kama Mwanzo, the Chanzo na hata Jambo TV niliona.
Mhe.Lissu: Waeleze majaji hicho ulichoona katika YouTube ya Chanzo, Mwanzo na Jambo TV zina urefu wa muda gani?
Heche: Kwenye Jambo TV ipo kama takribani masaa mawili, Chanzo ipo video ya dakika 45, na Mwanzo Tv kama dakika 60 hivi au lisaa na kitu yaani ziko tofauti tofauti.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno haya (Lissu anasoma maneno ya kwenye hati ya mashtaka… wanasema msimamo huu unaashiria uasi … tutaenda kukinukisha sana sana),
Heche: Ni miongoni mwa maneno ambayo yapo niliyoyasikia
Mhe. Lissu: Waeleze majaji yale uliyoyazungumzia kwenye ushahidi wako kama yapo.
Heche: Yapo maneno hayo niliyoyasema kwenye ushahidi wangu kama vile kuepusha maafa, engua engua ya wagombea na mengine mengi maana ni hotuba ya masaa mengi.
Mhe. Lissu: Shahidi shtaka ambalo nashitakiwa nalo linaeleza kwamba mimi ndio nilichapisha hayo maneno Jambo Tv wewe unasemaje?
Heche: Waheshimiwa Majaji, sio kweli kwasababu Lissu sio mfanyakazi wa jambo TV na kuna Shahidi wa Jamhuri yule wa kwenye kiboksi humu alisema yeye ndio aliyechapisha, anaitwa P ni shahidi wa 17 wa Jamhuri.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji juu ya mimi kufanya chochote kwenye Mkutano huo zaidi ya kuzungumza???
Heche: Mwenyekiti wetu, Tundu Lissu hakugusa kitu chochote zaidi ya kuzungumza, hakugusa kamera wala radio.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la uasi kwenye Katiba ya Tanzania??
Heche: Sina ufahamu wa uwepo wa kosa lolote la uasi kwenye katiba.
Mhe.Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye Katiba ya Tanzania.
Heche: Sina ufahamu wowote wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye Katiba.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye Katiba.
Heche: Sina ufahamu wa uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye katiba
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuhusu uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye Katiba
Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna uwepo wa kosa la kuzuia uchaguzi kwenye katiba.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi?
Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna uwepo wa kosa la kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi kwenye Katiba.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji ufahamu wako kuhusu uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye katiba hii?
Heche: Kwa ufahamu wangu hakuna uwepo wa kosa la kukinukisha kwenye Katiba
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako wako uwepo wa kosa linaloitwa kuzuia watu kwenda kupiga kura kwenye Katiba.
Heche: kwa ufahamu wangu hakuna kosa hilo kwenye katiba.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa kosa la uasi au rebellion kwenye Kanuni ya Adhabu.
Heche: Kwa ufahamu wangu sifahamu uwepo wa kosa la rebellion kwenye Sheria
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako uwepo wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye Penal Code.
Heche: Sina ufahamu wa uwepo wa kosa la kuhamasisha uasi kwenye kwenye Kanuni ya Adhabu
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji ufahamu wako kuhusu uwepo wa kosa la kuvuruga uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu
Heche: Sina ufahamu kuhusu uwepo wa kosa la kuvuruga Uchaguzi kwenye Kanuni ya Adhabu.
Part 402 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 400
Makam Mwenyekiti John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake.
Heche: Lissu alieleza kwa kirefu kuhusu wagombea wa upinzani wanavyoenguliwa kwasababu zisizo za kisheria wala za kikatiba na akaeleza kwamba kwenye uchaguzi wa 2020 ndio ulivunja rekodi kwa wagombea wengi wa upinzani kuenguliwa na hivyo CCM kupita bila kupingwa.
Akatoa mifano kuwa hiyo engua engua inawanufaisha CCM kwasababu hata mgombea wa kitongoji wa CCM hajawahi kuenguliwa, akawa anatoa mfano wa Suzani Limbweni Kiwanga aliyekuwa mgombewa wa Jimbo la Mlimba namna alivyoenguliwa na alikuwa mbunge wa jimbo hilohilo mwaka 2015.
Alitoa ifano ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2024 kuwa ulivunja rekodi zote za engua engua na kwamba hata kama tutaenda kwenye Uchaguzi na tukaenguliwa wote sasa hapo tutakuwa tumeshiriki nini, hivyo haikuwa na maana ya sisi kushiriki halafu tukaenguliwa wote.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji nilisema nini kuhusu mawakala wa vyama na wagombea?
Heche: Lissu alieleza kuwa wakala anapaswa kuwa muwakilishi wa mgombea na Chama chake lakini sasa taratibu zimewekwa ngumu kuanzia namna ya kuwaapisha na kupewa utambulisho, wengi wanakuwa wanafungiwa nje wanazuiliwa kuingia kwenye vituo na wengine kukamatwa na polisi na hivyo wagombea na Chadema kukosa mawakala kwenye vituo.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini kuhusu yanayotokea siku ya uchaguzi?
Heche: Lissu alieleza namna ambavyo usumbufu unakuwepo siku ya uchaguzi, namna ya wapiga kura kupata majina yao, mara jina halionekani , mara limewekwa kituo kingine.
Alielezea pia namna ambavyo kura zisizo halali zinavoingizwa kwenye vituo vya kupigia kura, namna ambavyo mawakala wananyimwa fomu za matokeo na fomu za kujaza malalamiko wanayoyaona kwenye vituo vya kupigia kura lakini pia namna ambavyo majumuisho yanavyofanyika na kura kutangazwa ambazo sio halali.
Shahidi anakumbukumbu ni kama ile Hotuba yote ya Mhe. Lissu ipo kichwani.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini kuhusu kupinga mambo haya mahakamani???
Heche: Lissu alieleza namna ambayo ni ngumu na watu mbalimbali wamejaribu kupinga mambo haya kupitia njia za Kimahakama.
Lakini pia alieleza namna ambavyo hata ushahidi ni mgumu kuupata maana unakuwa umeharibiwa, ugumu wa fomu za matokeo maana zinakuwa zinaharibiwa na wasimamizi wa uchaguzi, alieleza pia gharama kubwa ambazo zinatakiwa kulipwa na wagombea au walalamikaji wanapotaka kufungua kesi ambavyo wanakuwa hawawezi.
Akaeleza pia wingi wa kesi ambazo zingefunguliwa mfano wakati wa uchaguzi wa 2024 ambapo vijiji tu ni zaidi ya elfu kumi na saba ambavyo uchaguzi uliharibiwa kwahiyo isingekuwa rahisi kwa Chama kufungua kesi akamalizia kwamba kupitia kesi ya Mtikila Mahakama ilisema kwamba matatizo ya kisiasa yanapaswa kutatuliwa kisiasa sio lazima yaende Mahakamani.
Waheshimiwa majaji alisema pia kwamba kupitia kesi ya Dr. Amani Walid Kabourou ilisema kwamba uchaguzi ambao sio huru na haki sio Uchaguzi.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nilisema nini kuhusu hoja ya kuahirisha uchaguzi wa mwaka jana??
Heche: Waheshimiwa majaji Lissu alisema kwamba sisi kama chama tuko tayari Uchaguzi usogezwe mbele yafanyike kwanza mabadiliko ya kikatiba na kisheria yatakayoruhusu Uchaguzi huru na wa haki ili kuepusha maafa kama mauaji, utekaji, watu kujeruhiwa na kwamba Uchaguzi ukisogezwa mbele wananchi watapata haki ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Part 401 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Aliko Dangote and Donald Trump started business almost same year but Dangote is now far richer than Donald Trump.
Donald Trump got a “small loan” of $1 million from his father in 1975.
Aliko Dangote also got "small loan" of about $1 million from his uncle in the late 1970s.
But here’s the crazy part most people miss. Trump’s $1 million was already massive wealth in America at the time while Dangote’s reported ₦500,000 in the 1970s was so powerful that, because the naira was stronger than the dollar back then, it was worth roughly $1 million
Yes, Nigeria’s currency once traded ABOVE the dollar.
Two businessmen, two family boosts, two completely different economies.
One went into Manhattan real estate. The other started trading sugar, cement, and commodities in Lagos. Today, Donald Trump became President of the United States while Aliko Dangote became Africa’s richest man.
The lesson here is most billionaires don’t start from absolute zero. What separates them is what they BUILD after the opportunity lands in their hands.
And maybe the wildest part of this story is realizing how powerful Nigeria’s economy once looked in the 1970s compared to today.